Kesi ya Mbowe: Mchezo wa Paka na Panya kwa Maslahi ya nani?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,449
2,000
Jaji, polisi, mawakili wa serikali, na ofisi nyingine za umma zote ziko against Mbowe kwenye hii kesi, na zinapeana ushirikiano wa kutosha, hapa Mbowe lazima afungwe, no way out for him.

Ni wazi kuwa si kwa mfumo huu uliopo tena.

Mwanzo mpya si hiari tena.
 
citizensindevelopment18

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
1,164
1,500
Ni mshangao mkubwa haya kutokea kwa upande wa serikali yenye kupaswa kuupata uhalali wake kutokea kwa wananchi wanaoilipa kodi.

Ni mshangao mkubwa zaidi kuwa walioko huko serikalini tunaowalipa mishahara na marupurupu wanaweza kufikia kucheza na haki za wananchi kwa kiwango hiki.

Kwamba tumefikia kupageuza mahakamani kuwa mahali pa kuchezea mchezo wa Paka na panya (hide and seek) kinara wa mchezo akiwa serikali zikihusianishwa haki za watu ambao labda hata hawana hatia?

"Ya namna hii si ndiyo yaliyo msukuma Hamza kujichukulia sheria mikononi?"

Kwamba serikali haitaki nyendo za askari D/C Msemwa kuhakikiwa kwa mustakabala wa haki?

Haya yakitokea nchi zingine zinawavesha askari wake ma camera mwilini kurekodi matukio yanayowahusisha?

Kwamba serikali haitaki nyendo za maaskari Kingai, Mahita, Goodluck, Jumanne, nk zihakikiwe kuthibitisha uhalali wa madai yao dhidi ya watuhumiwa?

"Tangu lini askari hawa wakawa malaika?"

Kwamba kwenye mchezo wa Paka na panya huu kuna watu huenda hata wameuwawa, wamepotezwa, wamefanywa vilema, wameumia, wanaumizwa, wanateswa, nk?

"Kwamba haya yakitokea waratibu wa kadhia hizi mko majumbani mwenu mkila raha na kugongeana bilauri na wake au waume zenu kwa gharama zetu?

Hivi ni ndoto, au ndiyo jinamizi lenyewe?

Kwamba tulidhani ninyi na sisi tulihitaji kuujua ukweli ili kila mtu aubebe mzigo wake mwenyewe, lakini kumbe ninyi mna nia ya kuuficha?

Kwa hakika hatuwaelewi ni nini hasa mnachokitaka.

Kwa hakika kwa hali kama hizi itakuwa ni sahihi kutakana radhi wazi wazi:

"Tusije kulaumiana."
unazunguka kama pia. Sema usikike
 
Kalunya

JF-Expert Member
Oct 5, 2021
3,688
2,000
Hii kesi ni biashara kwa watu hadi wamalizie maghorofa yao ndo itaisha,unajua wanalipwa posho ngapi kwa siku Ili kuendesha?
Wapo watu kazini kubuni mbinu za kutafuna kodi zetu
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,449
2,000
nakuomba sana bwana au sijuii biii babati ,usikometi kwangu,,maana naona una heng over ya mimba ya aliyekutuma.

Ni neno "mchaga" mkuu? Nadhani pale ni typo alimaanisha "mchanga."

Kwa uelewa wangu Babati ni mmoja wa makamarade wa mstari wa mbele kabisa.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
37,338
2,000
😁😁😁
AIgmal.jpg
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,449
2,000
Kwanini Babati atusi wachaga.Hivi hebu atuambie nilipi kabila lake.

Iangalie sentensi yake nzima. Kulikuwa na neno mtoto.

Haiingii akilini kuwa alimaanisha "mtoto mchaga." Ninaona "mtoto mchanga" ndicho alichomaanisha.

Nikusihi kiungwana kuirejelea sentensi ile mkuu:

IMG_20211130_085856_152.jpg

Cc: Babati ikikupendeza kwa ufafanuzi zaidi.
 
pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
13,391
2,000
wenye madaraka waliobariki ukatili huu, wanaosimamia ukatili huu, wanaotoa ushahidi wa uongo ktk ukatili huu, laana hii itakuwa juu yenu na watoto wenu, mtakuwa watu wa ukiwa ktk maisha yenu, watoto wenu watakuwa wageni ktk ardhi yao. laana itawatafuna milele na jehenamu itakuwa makao yenu.
 
Eeh mola wetu ukazipokee sala zetu
 
mliberali

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
9,737
2,000
Ni mshangao mkubwa haya kutokea kwa upande wa serikali yenye kupaswa kuupata uhalali wake kutokea kwa wananchi wanaoilipa kodi.

Ni mshangao mkubwa zaidi kuwa walioko huko serikalini tunaowalipa mishahara na marupurupu wanaweza kufikia kucheza na haki za wananchi kwa kiwango hiki.

Kwamba tumefikia kupageuza mahakamani kuwa mahali pa kuchezea mchezo wa Paka na panya (hide and seek) kinara wa mchezo akiwa serikali zikihusianishwa haki za watu ambao labda hata hawana hatia?

"Ya namna hii si ndiyo yaliyo msukuma Hamza kujichukulia sheria mikononi?"

Kwamba serikali haitaki nyendo za askari D/C Msemwa kuhakikiwa kwa mustakabala wa haki?

Haya yakitokea nchi zingine zinawavesha askari wake ma camera mwilini kurekodi matukio yanayowahusisha?

Kwamba serikali haitaki nyendo za maaskari Kingai, Mahita, Goodluck, Jumanne, nk zihakikiwe kuthibitisha uhalali wa madai yao dhidi ya watuhumiwa?

"Tangu lini askari hawa wakawa malaika?"

Kwamba kwenye mchezo wa Paka na panya huu kuna watu huenda hata wameuwawa, wamepotezwa, wamefanywa vilema, wameumia, wanaumizwa, wanateswa, nk?

"Kwamba haya yakitokea waratibu wa kadhia hizi mko majumbani mwenu mkila raha na kugongeana bilauri na wake au waume zenu kwa gharama zetu?

Hivi ni ndoto, au ndiyo jinamizi lenyewe?

Kwamba tulidhani ninyi na sisi tulihitaji kuujua ukweli ili kila mtu aubebe mzigo wake mwenyewe, lakini kumbe ninyi mna nia ya kuuficha?

Kwa hakika hatuwaelewi ni nini hasa mnachokitaka.

Kwa hakika kwa hali kama hizi itakuwa ni sahihi kutakana radhi wazi wazi:

"Tusije kulaumiana."
Serikali inatetea uhalali wa uhalifu, watuhumiwa wanatetea haki na uwajibikaji hii ndo serekali dhaifu ya wahuni wa polepole
 
Ninaweza

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
11,145
2,000
Poleni kwenu mnao iamini serekali, ....hamkuwahi kuelewa kupitia hata kwa wale wanao ambiwa ...." Tuonesha kaburi la Babu wa babu na Bibi yako"..........ni mambo yale yale. Kwa kifupi ni kuwa bado hatujastaarabika hata kuweza kutembelea kwenye prescriptions tunazo jiwekea wenyewe, hatuna standards.
 
Kutokea tulipokuwa awamu #4 siyo siri tokea awamu #5 mwendo umekuwa "nose dive." Na bado!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom