Kesi ya Mbowe: Mchezo wa Paka na Panya kwa Maslahi ya nani?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,449
2,000
Ni mshangao mkubwa haya kutokea kwa upande wa serikali yenye kupaswa kuupata uhalali wake kutokea kwa wananchi wanaoilipa kodi.

Ni mshangao mkubwa zaidi kuwa walioko huko serikalini tunaowalipa mishahara na marupurupu wanaweza kufikia kucheza na haki za wananchi kwa kiwango hiki.

Kwamba tumefikia kupageuza mahakamani kuwa mahali pa kuchezea mchezo wa Paka na panya (hide and seek) kinara wa mchezo akiwa serikali zikihusianishwa haki za watu ambao labda hata hawana hatia?

"Ya namna hii si ndiyo yaliyo msukuma Hamza kujichukulia sheria mikononi?"

Kwamba serikali haitaki nyendo za askari D/C Msemwa kuhakikiwa kwa mustakabala wa haki?

Haya yakitokea nchi zingine zinawavesha askari wake ma camera mwilini kurekodi matukio yanayowahusisha?

Kwamba serikali haitaki nyendo za maaskari Kingai, Mahita, Goodluck, Jumanne, nk zihakikiwe kuthibitisha uhalali wa madai yao dhidi ya watuhumiwa?

"Tangu lini askari hawa wakawa malaika?"

Kwamba kwenye mchezo wa Paka na panya huu kuna watu huenda hata wameuwawa, wamepotezwa, wamefanywa vilema, wameumia, wanaumizwa, wanateswa, nk?

"Kwamba haya yakitokea waratibu wa kadhia hizi mko majumbani mwenu mkila raha na kugongeana bilauri na wake au waume zenu kwa gharama zetu?

Hivi ni ndoto, au ndiyo jinamizi lenyewe?

Kwamba tulidhani ninyi na sisi tulihitaji kuujua ukweli ili kila mtu aubebe mzigo wake mwenyewe, lakini kumbe ninyi mna nia ya kuuficha?

Kwa hakika hatuwaelewi ni nini hasa mnachokitaka.

Kwa hakika kwa hali kama hizi itakuwa ni sahihi kutakana radhi wazi wazi:

"Tusije kulaumiana."
 

IKUNGURU IJIRU CHUKU

JF-Expert Member
Feb 27, 2021
415
500
Kaka hatari yake ni kubwa kushinda wanavyo fikiria.Tunajenga jamii kubwa sana ya visasi.mama kaa kimya,hivi tuna viongozi kweli ,au tuna watawala na si ni watawaliwa?

Nahisi makubwa yaja,Tuendelee kupaza sauti labda ipo siku sauti yetu itasikika Nyikani.nahuzunika nasikitika,najaribu kuangalia niupi mustakabali wa taifa hili kesho yake.

Kila siku kwenye maisha yetu kuna “Majibwa” ambayo yametumwa kukutoa kwenye mstari,na kuihakikishia kuwa tanzania hii wao ndio mabwana nasi ndio watwana.
 

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
5,902
2,000
IMG_20211112_160343.jpg
 

IKUNGURU IJIRU CHUKU

JF-Expert Member
Feb 27, 2021
415
500
Kwa hakika ni suala la muda tu
Kuna hatari yanukia,Hivi uje uhukumiwe,,ukijikagua toka juu kichwani mpaka miguuni ,kwa kiri yako ya moyo,,kuwa hujawahi hata fikiria kufanya uhalifu hata wa kumchanja mtu na wembe,Theni unahukumiwa eti wewe ni Gaidi

Hivi mtu kama huyu akipata nafasi si anavyaa mabomu na kujilipua na watu kadhaa,,?? Hivi Tunadhani mataifa yanayo pigani ,yaliumbwa na Mola yakiwa yanapigana? Ukandamizaji na uoneaji ndio unaopelekea machafuko.TUJIHADHARI YASIJE FIKA HUKO.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
53,730
2,000
Kuna hatari yanukia,Hivi uje uhukumiwe,,ukijikagua toka juu kichwani mpaka miguuni ,kwa kiri yako ya moyo,,kuwa hujawahi hata fikiria kufanya uhalifu hata wa kumchanja mtu na wembe...
Hata watoto wake hakuna mchaga mwenye akili timamu atampigia kura wala kumpenda bibi ushungi
 

Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
6,625
2,000
Ni mshangao mkubwa haya kutokea kwa upande wa serikali yenye kupaswa kuupata uhalali wake kutokea kwa wananchi wanaoilipa kodi...
Unashangaa serikali hii ambayo imeshiriki mauaji ya raia wasio na hatia na kufunga miili kwenye viroba na kuitosa baharini! Huyu mama kesha sema kuwa yeye na mwendawazimu yule walikuwa kitu kimoja
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,878
2,000
Jaji, polisi, mawakili wa serikali, na ofisi nyingine za umma zote ziko against Mbowe kwenye hii kesi, na zinapeana ushirikiano wa kutosha, hapa Mbowe lazima afungwe, no way out for him.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,449
2,000
Jaji, polisi, mawakili wa serikali, na ofisi nyingine za umma zote ziko against Mbowe kwenye hii kesi, na zinapeana ushirikiano wa kutosha, hapa Mbowe lazima afungwe, no way out for him.

Kama mada ilivyohitimishwa - huko mbele ya safari:

"Tusije tukalaumiana."
 

Marco Polo

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
4,310
2,000
Kutwa kujivika ushungi kujidai mwenye haki na anayefuata maadili huku akichezea kodi zetu tunazikamuliwa kupitia kwenye tozo na kubariki mateso ya wasiokuwa na hatia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom