Kesi ya Lema kuna mkono wa Rais Magufuli?

Kesi ya Lema kuna mkono wa Rais Magufuli?

Maneno aliyoongea Lema ni mazito sana kwa mamlaka ya nchi. Sidhani kama kuna Mahakama italichukulis suala hili kimzaha mzaha. Je una hakika gani kama alichoongea Lema ni maono? Je hakuna mikakati yoyote ya chadema kutaka kumuua Rais? Kwa hakika katika nchi zingine mtu kama Lema angeshasahaulika kabisa. Hapa kwetu demokrasia inatufanya rusitekeleze ipasavyo sheria za nchi

Uwe na akili Siku Moja Moja wewe!! Kwani mahakama ndiyo iliyofungia nayo madai? Umesoma na kujua kwa nini amerudishwa rumande?
 
Dawa ya zuzu ni kulizuzua tu.
Kuna watu wanamihemko ya kuchochea hata pasipo kuwa sababu, tuliona walianza na uchwara mara kile.

Yaani mnatuchanganya tu ngoja atiwe adabu. Ndoto zote za kijinga tungesimulia si tungekamatana ugoni hapa.

Ngoja asote rumande
Sahihi
 
Lema amewekwa Rumande kwa zaidi ya Mwezi sasa. Ati Kosa lake ni Pale aliposema Kuwa, " Magufuli anajifanya ni Mungu na asipobadilika Mungu atamuua Kabla ya 2020. Pia Bungeni ambapo kuna immunity akasema tena Kuwa aliona Maono kuwa, Mungu atamuua Magufuli kabla ya 2020. Sasa Kama imani ya Lema ni sahihi au La, Huwezi Kumpeleka mtu Rumande kwa Kusimulia ndoto aliyoota hata Kama ameota kuwa Tanzania yote italipuliwa na Super volcano mwezi Ujao. Na Pia huwezi kumweka Mtu Jela kwa Kuwa anakiri kwa Imani yake Mtu anayejitia yupo juu ya sheria (Kama anavyojitia Magufuli) Kwa imani yake Mtu huyo anajifanya Mungu na Kwa imani yake Mtu huyo Mungu atamuua.

Lema angekuwa na hatia kama angalisema Kuwa anapanga Kumuua Magufuli Kabla ya 2020. Hapo wala Nisingemtetea. lakini kwa aliyosema Kumpeleka Rumande ni Ushenzi, na Ukowadi.

Naona Tanzania imegeuka Nchi ya wanaojifanya Miungu, hata huyu Kunguni Mkuu wa Mkoa Makonda akasema Juzi Kuwa ati akisema Yeye ni Mungu Kasema. Niseme tuu Biblia inasema Kuwa Lolote Tulifungalo Duniani, Limefugwa Mbinguni, na Lolote Tutakalolifuungua Duniani Litafuunguliwa Duniani. Nina huzuni ya Kufa kwa uonevu unaofanywa Nchini, Hasa kwa Ndugu Lema ambaye he has never hurm no one! Katika Maisha yangu sijawahi Kufunga na Kuomba ninilolitamani kwa Mzigo au Huzuni ya Kiasi hiki, Mungu asinisikie, Sasa Mini nitafunga siku 3 Kuomba kinyume na Ushetani na Unyama wa Uonevu Tanzania. Kama lema na Wengine wanao onewa Kisiasa Bila Kujalk Chama hawataachiwa By Monday. Nitaomba Mungu awanyanyue Watu fulani Na wakinyanyuka tu Nchi nzima itajua.
LEMA ANAVUNA MATUNDA YA KUROPOKA . AKITOKA HUKO ATAKUWA NA NIDHAMU YA ULIMI. HAJAONEWA NA MTU YEYOTE.
 
Jamaa anaropoka sana ngoja apate adamu sijui hicho ndo wananchi wake walichomtuma chama anakiweka mbele kuliko wananchi wake.
Kama Kuropoka tu kunamfikisha Mtu Rumande basi, Magufuli anaropoka utadhani amemeza Kengele ya kuchunga Ng,ombe naye tumpeleke Rumande?

1) Ningelikuwa mimi ndio Mwenyekiti halafu wanajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wakaimba wana imani na sijui nana, siku hiyo hiyo ngewapoteza hata Nusu.
2) Hata mtu ufuge ndevu unyoe uchaguzi Haurudiwe ... Mpe Jecha Tuzo
3) Mtu anakukatalia mkono halafu unasaini akatibiwe
4) Tunatumia Kodi ya wananchi Kuwasomesha Vila-za
5) Masaburi alikuwa na wake Wanne watano, Natamani kama mini na Kikwete tungekuwa na...
..

..
..

Kuropoka kwingi Tu. Lema anaongea Kwa Hekima, Mpaka akiongea Bungeni Wabunge wote wawe CCM au Upinzani wanatulia wanamsikiliza. Kama Ujasiri wa Kusema Kweli Ni Kuropoka na. Mimi nataka Kuropoka huko sana tu! Ila huu wa Kumeza Kengele no!
 
habar comrades,

Najaribu kuwaza tu! na nimejiuliza kwa nn mahakama inamnyima Lema dhamana wakati kesi yake inastahili dhamana?..je kesi yake ni ya mauaji mpaka mahakama imnyime dhamana?..hapa kweli hakuna kaarufu ka order kutoka juu?

Wanasheria wenu wa field walikata rufaa nje ya muda tena bila kusudio la kukata rufaa, wamebwagwa mahakamani imekuwa "order kutoka juu" Kweli mataahira hawatoisha nchi hii...
 
mtajiuliza sana hawamu hii,awamu hii aipendi ujinga,acha sheria ifuate mkondo wke,mwehu mmoja awezi kuharibu amani ya nchi ambayo watanzania wanaitunza kwa muda mrefu sana

Hii awamu ndo inongoza kwa ujinga kuzidi awamu zote lejea kuchapisha noti mpya kudhania watu wameficha pesa
 
Maneno aliyoongea Lema ni mazito sana kwa mamlaka ya nchi. Sidhani kama kuna Mahakama italichukulis suala hili kimzaha mzaha. Je una hakika gani kama alichoongea Lema ni maono? Je hakuna mikakati yoyote ya chadema kutaka kumuua Rais? Kwa hakika katika nchi zingine mtu kama Lema angeshasahaulika kabisa. Hapa kwetu demokrasia inatufanya rusitekeleze ipasavyo sheria za nchi
Sahihi ngoja aonje joto la jiwe
 
Jombaa unauliza nzi chooni!

Wambali alivyomchinjia kafulila baharini alipewa ujaji kiongozi.

Yule hakimu huenda anataka ujaji,na nafasi zilitoka na anataka!
 
Lema kwishiney nan mjinga nampumbavu akamuandamanie fala labda mke wake na watt wake maana ndo alikua anawalisha
 
Dawa ya zuzu ni kulizuzua tu.
Kuna watu wanamihemko ya kuchochea hata pasipo kuwa sababu, tuliona walianza na uchwara mara kile.

Yaani mnatuchanganya tu ngoja atiwe adabu. Ndoto zote za kijinga tungesimulia si tungekamatana ugoni hapa.

Ngoja asote rumande
Unaonaje ukiiachia mahakama ije hatimae itoe hukumu baada ya kusikiliza kesi. Swala la dhamana ni tofauti kabisa na adhabu ya kosa. Kwa hulka na makuzi yako waweza kuwa unajisikia furaha haki ya wengine kupata dhamana inapochezewa, lakini sio busara kupotosha swala hili.
 
Ubaya mmoja katika hayo maono yake hakuona kama atanyea ndoo miezi miwili
 
Kuomba Kwa kutishia sio kuomba. Kikawaida hatumuombei mtu Mabaya. Mimi nakushauri Raisi ni mtu wa kumuombea mema Mungu amfanikishe, maana Mungu asipomsaidia Wengi tutapata shida.
Hakuna mwanamaombi yoyote aliye WA Kweli anaweza kumuombea Rais WA nchi anayoishi yeye Mabaya. Ukiona Huyo ujue ni mwanamaombi WA kisiasa.
Unataka kutuambia kuwa Musa hakumwombea mabaya Farao ? alipo wakalia Waisrael ?
 
Nawewe kwa kujipendekezaaa!

Siko humu JF kumfurahisha Mtu wa CCM au wa CHADEMA na UKAWA yao au Rais Dkt. Magufuli au Waziri Mkuu ' aliyejiuzuru ' Lowassa bali nipo humu JF kusema ukweli na siku zote nitakuwa ' neutral ' katika ' utetezi ' na ' ujengaji ' wangu wa ' Hoja ' ninazokutana nazo humu humu. Yawezekana Wewe ni ' Mgeni ' kwangu kwani humu humu huwa ' nakosoa ' pia ' mapungufu ' ya Rais ' Kiutendaji ' au ya ' Taasisi ' zake na pia mara kwa mara huwa nakuwa Mtu wa kwanza tena hadi najitaja kuwa ni Mwana CCM lakini huwa ' napongeza ' mambo ' mazuri ' ya ' Upinzani ' na hadi ' kuwasifu '. Narudia tena yawezekana ukawa ni mgeni kwangu GENTAMYCINE hivyo ' sikulaumu ' sana Mkuu. Siendeshwi na sipelekeshwi na Mtu yoyote halafu siishi kwa ' kujipendekeza ' katika ' Siasa ' bali ' Utaalam ' wangu wa ' kutukuka ' wa mambo kadha wa kadha ya ' Kitaaluma ' ndiyo unaniweka ' mjini ' na naendesha ' maisha ' yangu bila ' matatizo ' na nimeridhika pia na haya haya maisha yangu ya kiasi niliyonayo na nadhani yananitosha mno.
 
sisi kina gogo la shamba tulishasema Lema amejiwekea heshima kubwa ya kutetea haki,vyovyote watakavyomfanyia lazima ataibuka mshindi na wale wote wanaomfanyia hila mwisho wao utakuwa haibu kubwa mbele ya jamii
Dua la kuku
 
Moja ya Kanun kubwa sana za kuwaza ni kuwaza toward and backward. Yaaani kwa kwenda mbele na kurudi nyuma. Ukichagua kuwaza kwa kwenda mbele peke yake utakosea sehem flan na ukiwaza kwa kurud nyuma peke yake utakosea kabisa.

Kesi ya Lema imechukua mitazamo mipya kila siku. Na nmekuwa siku zote nilisikitika kwa hili.

Jana nikawaza kwa kurudi nyuma. Alikosea nini?alisema kuwa rais blah blah blah... Atakufa kabla ya 2020 . nikajiuliza hii inatija gani kwa Taifa?ndoto au maono haya?je alienda kumwambia rais jambo hilo?kumwonya kama ambavyo alipaswa kufanya kinabii.

Lakini nikajiuliza lema ameanza lini kuwa anapokea maono au unabii? Halaf huu uwe ni wa pili na watatu n.k? Je mungu gani anayemtumia Lema kuona maono haya? Yana tija gan kwa Taifa ikiwa si ya kweli?

Sikuona sabab ya lema kuteseka jela kwa jambo kama hili.halikuwa na msingi na si jambo la muhimu sana. Utabiri wa kifo huwa unakuwa sahihi kama ukitaja na mazingira ya kifo au kipindi cha kifo.kila mtu atakufa na maono ya kuwa asipobadilika atakufa kabla ya mwaka 2020 ni vague. Maana yake asipokufa itaonekana alibadilika.

Otherwise sioni kesi yenye tija hapo kwa lema na serikali kwa ujumla.tungetaman awekwe ndani kwa kuwateteta wananchi wa eneo flan.
 
Unaonaje ukiiachia mahakama ije hatimae itoe hukumu baada ya kusikiliza kesi. Swala la dhamana ni tofauti kabisa na adhabu ya kosa. Kwa hulka na makuzi yako waweza kuwa unajisikia furaha haki ya wengine kupata dhamana inapochezewa, lakini sio busara kupotosha swala hili.
Hata Magufuli anajua hana Kesi, Serikali ovu zinatumia Rumande na Pingamizi la Dhamana kwa Lengo la kumtesa mtu wanayejua katika kesi ya msingi hawana uwezekano wa kushinda, Hivyo wanampeleka mtu Rumande_ kisha wanafanya mchezo wa 1) Kupinga dhamana 2) Kudai upelelezi haujakamilika!
 
Back
Top Bottom