Kesi ya Lema kuna mkono wa Rais Magufuli?

Kesi ya Lema kuna mkono wa Rais Magufuli?

Itakuwa laana ya kumuandama Lowassa kama mnavyowaambia wa upande wa pili.

Ukiongea ujinga kwa hoja ya ndoto/maono,you'll pay the price.

Wanasheria wa serikali wakiendelea na huu umakini,mtamsingizia sana Magufuli awamu hii.
 
Kumbe Wazungu ama hakika hawakukosea kutuita sisi Waafrika ' manyani / masokwe ' na huku ' wakitudharau ' kwani inaonyesha walifanya ' utafiti ' wao mkubwa sana na wakajitosheleza kuwa sisi Waafrika tuna ' tatizo ' kubwa tena la kiasili la kuwa na very ' hopeless ' IQ. Hivi kwa ' akili ' za kawaida tu Rais Dkt. Magufuli anaingiaje katika hiyo Kesi ya Lema? Je Rais ndiyo Hakimu? Je Rais ndiyo aliyemtuma huyo Lema wenu ' awehuke ' vile? Ungetumia platform hii kumsihi huyo Lema wako kuwa alichokuwa anakifanya siyo healthy politic bali ni uhuni mtupu na kuwasihi wengine jinsi ya kufanya Siasa zenye ' tija ' na faida kwa Mama Tanzania ningekuona wa maana mno. Nimekudharau sana Mkuu na ' samahani ' kwa hilo.
ukimdharau MTU ujue hata wewe kuna mtu ana kudharau kwani wewe sio bora au hata wewe hujui mambo mengine tu ambayo wengine wana yajua. punguza jazba kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake hata kama hayatosikilizwa
 
Ukifikiria sana kesi ya Lema, hakika hata machozi yanaweza kukulenga lenga........

Inawezekanaje mahakama ing'ang'anie kumnyima dhamana kama vile Lema ana murder case?

Hivi kumbe ukipata maono na kuyaweka hadharani, kwa mahakama zetu tayari una murder case?

Mbona hata Bwana yule kwenye mazishi ya Masaburi, alitamka hadharani kuwa Lowasa atakufa, JK naye atakufa na yeye mwenyewe naye 'alijitabiria' kifo?

Mbona 'maono' hayo ya Bwana yule hayakuonekana kama murder or treason case?!

Ila hayo matamshi ya Lema ndiyo yanachukuliwa kama treason or murder case!!!

It is obvious haiwezekani mahakama ikomae kiasi hicho kumnyima dhamana Lema dhamana ambayo ni haki yake kisheria kama siyo 'order' toka juu..........

Hata hivyo hakuna kitu chochote hapa duniani kilichokuwa na mwanzo kikakosa kuwa na mwisho.....

Uko sahihi.
 
Kwa hiyo unataka kulazimisha watu wakufuate wewe??
We ndo mwenye akili ya kujua mkosaji na mtenda haki??
We nani kwanza??

Mimi ni GENTAMYCINE a.k.a Le Grand l'animateur et Charismatique. Je una swali lingine sijui Mkuu?
 
habar comrades,

Najaribu kuwaza tu! na nimejiuliza kwa nn mahakama inamnyima Lema dhamana wakati kesi yake inastahili dhamana?..je kesi yake ni ya mauaji mpaka mahakama imnyime dhamana?..hapa kweli hakuna kaarufu ka order kutoka juu?
Dhamana iko wazi! Tatizo Mawakili wa Lema
 
Itakuwa laana ya kumuandama Lowassa kama mnavyowaambia wa upande wa pili.

Ukiongea ujinga kwa hoja ya ndoto/maono,you'll pay the price.

Wanasheria wa serikali wakiendelea na huu umakini,mtamsingizia sana Magufuli awamu hii.
Hakuna cha umakini hapo,ni uonevu tu.
 
soon I sababu ya kuhangaika na ndoto za watu na isitoshe ndoto nyingi huwa hazina ukweli kwa kuwa nyingi huwa ni reflection ya kile mtu husika anachokiwaza,labda ndoto ambayo huwa inatimia ni pale unapoota kuwa unakojoa tu.Hiyo lazima kukicha utaanika matandiko tu
 
Ukifikiria sana kesi ya Lema, hakika hata machozi yanaweza kukulenga lenga........

Inawezekanaje mahakama ing'ang'anie kumnyima dhamana kama vile Lema ana murder case?

Hivi kumbe ukipata maono na kuyaweka hadharani, kwa mahakama zetu tayari una murder case?

Mbona hata Bwana yule kwenye mazishi ya Masaburi, alitamka hadharani kuwa Lowasa atakufa, JK naye atakufa na yeye mwenyewe naye 'alijitabiria' kifo?

Mbona 'maono' hayo ya Bwana yule hayakuonekana kama murder or treason case?!

Ila hayo matamshi ya Lema ndiyo yanachukuliwa kama treason or murder case!!!

It is obvious haiwezekani mahakama ikomae kiasi hicho kumnyima dhamana Lema dhamana ambayo ni haki yake kisheria kama siyo 'order' toka juu..........

Hata hivyo hakuna kitu chochote hapa duniani kilichokuwa na mwanzo kikakosa kuwa na mwisho.....
kwani dhamana inatolewa bila wahusika kujenga hoja? sasa kama wamefanya makosa hata yakutojua ni lini siku sahihi ya kukata rufaa unataka mahakama ifanye nini? watu wanakosea hata sehemu ya kupeleka maombi ya dhamana yao sasa unataka wasaidiwe nini wale wasomi mawakili? mahakama si baba wala mama wa Lema mpaka imuonee huruma.
 
Mbunge wa Ilala Azzan Zungu anaumwa tumuombee amelazwa JKHI, Muhimbili.
 
Serikali iliyoshindwa kuongoza nchi,huanza kugombana na wananchi wake.Lema haja ua mpeni dhamana acheni uonevu.Hii nchi ni yetu wote sipendi Ujinga uliyo kithiri.
 
Huo ndo ukweli Tanzania hatuna amani ila tunauoga kwa sababu hata saizi ingekua kunauwezekano wa kufungua mioyo yetu ungekuta zaidi ya 90% wanasononeka hawana aman mioyoni mwao.
 
Hizi thread za lema zinatosha sasa,zimekua nyingi sana...yeye si kaamua kua mtafsiri wa ndoto,mbona haoti lini atatoka mahabusu!?
Mkuu ndoto mpaka mtu uote au Mungu akuoneshe inaelekea Mungu bado hajamuonesha.
 
Tatizo ni dikteta uchwara eti asiyejaribiwa...tujifunze kuita koleo kwa jina lake.
Sikatai, ila mengine tutakua tunalemaza akili zetu kwa nguvu zetu wenyewe. Mazingira ya mwanzo kabisa ya kuiondoa dhamana ya Lema ni kweli hayapo sawa, kila kitu kilionyesha kuwa pana zaidi ya nguvu na hoja za kisheria. Lakini yote yaliyofuata baada ya hapo tumeshuhudia namna wanasheria hao wanavyofundishwa taratibu za kimahakama na mwisho kumgharimu Lema.
 
Back
Top Bottom