Gereza si kaburi hata hivyo MH.Lema alishakamilisha kila kitu hapa duniani sio kama vijana wapiga zomali tu wasiokuwa na mbele wala nyuma hawana hata katoto ka kusingiziwa na kutwa nzima wako Lumumba kutafuta japo mia mbili ya kula.
Lema anakila kitu ana watoto, ana maisha mazuri watoto wake wataishi vizuri, kwa hiyo kumfunga Lema leo hujayafunga mawazo yake bali kuna mtu flani anaandaliwa kuja kuwa jasiri zaidi ya Lema ambaye pengine ni Allbless Godbless Jonathan Lema ambaye ameushuhudia udharimu anaofanyiwa baba ake au kijana yeyote anayeshuhudia udharimu huu sasa chini ya Rais Magufuli.
Hata makabulu walimuuwa Steven Biko but leo mawazo ya Steven Biko yamefufuliwa na kijana machachali Julius Malema, na leo hawapumui na kijana anazidi kupata uungwaji mkono mkubwa wa watu wa south Africa. Ni suala la mda tu.