Ni "jamii ya wendawazimu'' pekee ambayo hoja hujibiwa kwa tusi ama kejeli. Baraza la Jamii (kama Jamii Forum inaweza pata tafsiri ya moja kwa moja ya kiswahili), linatuhusu sote tuliomo ndani ya "Jamii" mbalimbali ambazo hekima, busara na hata matusi huzifanya kuwa jamii. Lakini, kuwepo kwa matusi ama kejeli ndani ya jamii hizo HAKUTUFANYI TUONEKANE WANAJAMII HASWAA bali matusi ama lugha hizo za kejeli hututofautisha na wanajamii wengine na kuonesha kiwango cha kustaarabika tulicho nacho (sioni ajabu kuona post hii inajibiwa kwa tusi kwani ndio "jamii" ninayoizungumzia).
Ukiitazama kwa undani hoja ya mtoa mada, haihitaji jibu la kuanzia mahakamani tu bali nje ya mahakama kwa kulitazama "kosa" lililomuweka rumande na namna mahojiano ya kisheria dhidi ya mawakiri wa pande zote mbili yalivyochukua mkondo wake juu ya "kosa" hilo na maamuzi yaliyotolewa baadae.
Labda tujiulize (najua umeisha jiuliza);
Je, Lema pekee ndiye wa kwanza kutoa matamshi ya kumtabiria mtu kifo?
Kama Lema si wa kwanza, yule wa kwanza alichukuliwa hatua gani kwa matamshi ambayo hayakiwa ya "kimaono" kama ya Lema bali yaliyotoka katika vinywa vikavu vya watoaji wa kauli hizo dhidi ya mtu X ama Y kuwa "atakufa ndaani ya muda wa siku, wiki ama miezi michache"? Ama hizo hazikuwa kauli za "uchonganishi" (Ref. Uchaguzi uliopita)?
Kama Lema ndiye wa kwanza, sheria inasemaje kuhusu "imani, utabiri" (Daudi alitabiriwa kifo kwa kumchukua mke wa mpiganaji wake lakini "udaudi" wake haukutumika kubadilisha blue kuwa njano bali alitubu)?
Ukipata majibu ya huto tuswali n mengine utakayo yapata; njoo nayo barazani bila kejeli na matusi, mjibu mtoa hoja.
Alichokitoa mwenzetu ni mawazo yake ambayo unahiari ya kuyapokea kwa kuchangia for ama kuyakataa kwa kwenda against. Sasa humu kila hoja unayoikataa huikatai kwa hoja bali "matusi na kejeli". Hapo ndipo utakapogundua kuwa "NYUMA YA ID ZETU ZISIZO NA MAANA KWA WENGINE ILA KWETU PEKEE, NDIKO TABIA ZETU ZILIKOJIFICHA".