Kesi dhidi ya JamiiForums: Meneja wa OILCOM (T) LTD atoa ushahidi, vielelezo vyake vyapingwa... Shauri laahirishwa

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
Wakuu,

Leo Kesi namba 456 inayowakabili Maxence Melo na Micke William imeendelea tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu mbele ya Hakimu Thomas Simba kwa kusikilizwa Shahidi wa tatu na wa nne katika kesi hii.

Tayari shahidi wa kwanza kwenye kesi hii alishafanyiwa mahojiano na kutoa ushahidi wake. Alikuwa ni kaimu ZCO, Ndg. Ramadhani Kingai (Soma Yaliyojiri katika Kesi namba 456: Jamhuri dhidi ya JamiiForums - Oilcom na Uchakachuaji/Ukwepaji kodi bandarini Dar na pia soma Sehemu ya II: Jamhuri vs JamiiForums kuhusu Oilcom na Uchakachuaji mafuta/Ukwepaji Kodi bandarini Dar

Shahidi wa pili alisikilizwa wiki iliyopita na unaweza kusoma hapa: Kesi namba 456 (Jamhuri vs JamiiForums): Shahidi akiri mshtakiwa namba 2 yupo kimakosa...

Shahidi wa tatu amesikilizwa leo na unaweza kusoma hapa: Kesi dhidi ya JamiiForums: Shahidi adai waliomba taarifa za mteja bila kutaja ni kwa mujibu wa sheria gani

Shahidi wa pili kwa leo (Shahidi namba nne) ni mfanyakazi wa Oilcom (T) Ltd na anaitwa Ndg. Usama Mohammed, ana umri wa miaka 31 na ni mwislamu kwa imani. Ameapishwa kwa kutumia Quran na ameahidi kuongea ukweli mtupu.

Shahidi anaongozwa na Wakili wa Jamhuri, Mutalemwa Kishenyi na washtakiwa wanawakilishwa na Mawakili Jeremiah Mtobesya, Peter Kibatala na Jebra Kambole.

Wakili Kishenyi: Unafanya kazi gani?

Shahidi: Mimi ni Meneja wa mauzo ya rejareja wa kampuni ya Oilcom (T) Ltd.

Wakili Kishenyi: Ofisi zenu ziko wapi?

Shahidi: Kurasini, jijini Dar es Salaam

Wakili Kishenyi: Umekuwa na hicho cheo tangu lini?

Shahidi: Tangu mwaka 2012

Wakili Kishenyi: Hebu iambie mahakama, tarehe 13/02/2016 majira ya jioni unakumbuka nini kuhusu shauri lililopo mahakamani?

Shahidi: Nilipigiwa simu na Bosi wangu wangu Fuwad Omar Mbarak kuwa kuna taarifa zilizoandikwa kwenye mtandao wa Jamii Forums zenye lengo la kuchafua kampuni yetu.

Wakili Kishenyi: Zilikuwa zinahusu nini?

Shahidi: Ushuhuda: Jinsi mafuta yanavyoibiwa bandarini Dar

Wakili Kishenyi: Baada ya kupata taarifa, ulifanya nini?

Shahidi: Niliingia kwenye mtandao wa JamiiForums kuthibitisha ukweli wa kinachosemwa. Baada ya kuthibisha na kuyasoma, nilimpa mrejesho Bosi wangu kuwa ni kweli kuna uzi huo.

Wakili Kishenyi: Baada ya mrejesho nini kilifuata?

Shahidi: Alinishauri nifanye utaratibu wa kulifikisha hili suala Polisi. Wakati najiandaa, ukatoka uzi mwingine siku ya 15/02/2016 wenye kichwa cha habari: “USHUHUDA: Hii ndiyo michezo hatarishi ya kampuni ya mafuta ya Oilcom”. Mwandishi aliendelea kuichafua kampuni ya mafuta ya Oilcom.

Wakili Kishenyi: Aliyekuwa akiichafua kampuni alikuwa anaitwa nani?

Shahidi: Kwa mujibu wa huu mtandao, alikuwa anaitwa Fuhrer

Wakili Kishenyi: Ulichukua hatua gani?

Shahidi: Baada ya uzi wa pili, hatua tuliyochokua ni kulifikisha jambo hili Polisi na nilifika Polisi kuandika maelezo yangu kuhusu kadhia hiyo na maelezo yangu yalichukuliwa na afande Peter juu ya taarifa zinazoichafua kampuni yetu na kumpa documents ambazo niliziprint kutoka katika huo mtandao. “Nili-print screen”

Wakili Kishenyi: Uliongeza au kupunguza kitu chochote?

Shahidi: Sikuongeza wala kupunguza kitu chochote.

Shahidi anaangalia nyaraka (documents) zilizotoka kwenye bahasha aliyokuwa nayo Wakili Kishenyi na kuzitambua. Wakili anaiomba mahakama ipokee nyaraka hizo (printout) kama sehemu ya ushahidi.

Upande wa utetezi unapinga kupokelewa kwa ushahidi kwa sababu havijakidhi vigezo vya kisheria kutokana na 'electronic process' kwa uamuzi wa Jaji Robert Makaramba.


…Baada ya mapumziko ya saa 1 hivi, mahakama inaendelea…


Wakili Kibatala(Utetezi): Ushahidi wanaotaka kuutoa unaangukia katika Electronic Evidence Act na Kuna masharti ya kisheria kwa Mahakama kupokea Electronic Evidence. Vigezo hivyo vitano(amevitaja vyote) ambavyo vyote lazima viendane kwa pamoja viliwekwa na shauri la commercial case no 10 ya mwaka 2008 kati ya Lazarius Mirisho Mafie Vs Gasper Kilenga alias moiso Gasper uamuzi wa Mheshimiwa Jaji Makaramba.

Shahidi hajajengewa foundation kabisa ya kukidhi hivyo vigezo na vinatakiwa kuzibwa na Shahidi na sio vinginevyo, pia Haipo katika original form, hiyo ni nakala(copy) na kwa misingi hiiyo miwili tunapinga ushahidi kupokelewa.

(Ubishi kidogo unatokea kati ya wakili wa Utetezi na wakili wa Jamhuri)

Wakili Kishenyi: Mapingamizi la Wakili msomi Kibatala hayana uzito kwenye ombi la kupokea kielelezo. Upokeaji wa Electronic Printout unaongozwa na Sheria namba 18 ya Electronic Transactions Act (Amevitaja vifungu na kujibu mapingamizi yaliyotolewa na Wakili Kibatala).

Wakili Kibatala: Kimsingi alichoongea Wakili Kishenyi hakina jipya bali ni lugha tofauti kwani kifungu kimefanana na hukumu ya Jaji Makaramba na ufafanuzi umetolewa kwenye kifungu cha 19 katika Sheria aliyoileta mwenyewe (Electronic Transactions Act 2015).

Kesi imeahirishwa mpaka Jumatano tarehe 21/12/2017 saa sita mchana.
 
Mimi ningekuwa yule mtoa thread ,simu ningeitupilia mbali na account siitumii tena


Kwa uwezo wa Mungu JF itashinda
Mkuu unapotoa thread, hakikisha unaandika mambo ya ukweli. Usiandike uzushi, ili ikitokea kutafutana, unakomaa na vielelezo vyako hadi mwisho.
Yanini kukimbiakimbia ama kutupa cm?
 
Mimi ningekuwa yule mtoa thread ,simu ningeitupilia mbali na account siitumii tena


Kwa uwezo wa Mungu JF itashinda
namba ya smu ulotumia na email vinaweza kusaidia kujua wewe ni nan!
labda u delete email na namba ya cm ufanye manuva wa badilishe apewe mbibi kolomije huko!
halafu records zote zifutwe!
 
Kumbe mimi nikitoa thread ya uongo INASHTAKIWA JF? Kuna watu wameituhumu OilCom tena siku chache zilizopita
 
Back
Top Bottom