Kesho ni mkutano mkuu wa Simba ajenda kuu ni Katiba

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
15,204
20,185
Kesho Kuna mkutano mkuu wa timu ya Simba ,mojawapo ya ajenda ni mabadiliko ya katiba ili kukamilisha mchakato wa uwekezaji.

Tayari kamati iliyokusanya maoni kupitia mwenyekiti wake Husein Kitta umesema umemaliza kazi take na kukabidhiaoni tayari kwa ajili ya kupitishwa na mkutano mkuu lakini baadhi ya wanachama wametoa maoni tofauti, mwenyekiti wa tawi la wekundu terminal ameunga mkono maoni hayo wakati mweka hazina wa tawi la roho mbaya ameyapinga kwa kusema kamati imeleta maoni yanayompendelea zaidi mwekezaji hivyo hatakuwa tayari kuyapitisha.

Waliowahi kuwa viongozi wa Simba kwa nyakati tofauti wametoa maoni yao, Godfrey Nyange Kabutu amesema anaenda kuyapinga maoni hayo kwani yamemweka mwenyekiti wa Simba Kama mjumbe hivyo Hana mamlaka yoyote wakati ismai Aden Rage ameshauri swala la mabadiliko ya katiba lilitakiwa liandaliwe mkutano wake maalumu badala ya ya kuchanganua na mkutano mkuu.

Ukipitia harakaharaka hizi hoja utaona kuwa kamati ya mabadiko ya katiba iliteuliwa na Bodi hivyo lazima walinde maslahi ya mwekezaji kwani Rita walikataa kuipitisha katiba ya Simba baada ya kuona mwekezaji mwenye asilimia pungufu ana nguvu kuliko wanachama wenye asilimia nyingi.

Kitendo cha kuweka ajenda ya mabadiliko ya katiba kwenye mkutano mkuu ni kutaka wanachama wajikite kwenye katiba badala ya kuhoji kipigo kikubwa kwa siku za karibuni toka kwa mtani wao wa Hadi, dirisha la usajili limeshafungwa hivyo hawawezi kuwaleta kina manzoki kuwadanganya wanachama njia pekee ni kuleta mada itakayoleta ubishi na mkutano kuvunjika.

Simba ndio walianzisha mfumo wa mageuzi, wenzao yanga wakiangalia mapungufu yao na kuja na mfumo Bora zaidi hivyo Simba hawajachelewa bado wanayo nafasi ya kuboresha mfumo wao kwani wao ndio waasisi.
CEO anatoa taarifa, mtunza fedha anatoa taarifa.
Ni mapumziko baada ya mapumzikow Mwenyekiti wa kamati ya maboresho ya katiba ndio anatoa taarifa.
 
Kesho Kuna mkutano mkuu wa timu ya Simba ,mojawapo ya ajenda ni mabadiliko ya katiba ili kukamilisha mchakato wa uwekezaji.
Tayari kamati iliyokusanya maoni kupitia mwenyekiti wake Husein Kitta umesema umemaliza kazi take na kukabidhiaoni tayari kmageuzi, wenzao yanga wakiangalia mapungufu yao na kuja na mfumo Bora zaidi hivyo Simba hawajachelewa bado wanayo nafasi ya kuboresha mfumo wao kwani wao ndio waasiso.
Wale ni mbumbumbu (Rage), wameshindwa kutengeneza katiba inayoeleweka. Wapo wanazunguka zunguka tu.
 
Kesho Kuna mkutano mkuu wa timu ya Simba ,mojawapo ya ajenda ni mabadiliko ya katiba ili kukamilisha mchakato wa uwekezaji.
Tayari kamati iliyokusanya maoni kupitia mwenyekiti wake Husein Kitta umesema umemaliza kazi take na kukabidhiaoni tayari kwa ajili ya kayo nafasi ya kuboresha mfumo wao kwani wao ndio waasiso.
Mbumbumbu FC
 
Kama mambo ya katiba ya vilabu yanatupa changamoto hatuelewani vipi kuhusu katiba ya nchi?

Je, ni sahihi kwa aliyeseme wananchi wapewe elimu zaidi.

Hivi vilabu tuache wenye pesa waweke na kuviendesha. Kitu pekee ni kufanya viwe na hisa ili kila mtu anayetaka aimiliki.

Najua kutakuwa na minority uzuri sheria na taratibu zimewekwa kuwalinda.

Tuache hizi blah blah za chumia tumbo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom