Mangungu amjibu Mo Dewji: Simba SC haiuzwi na haitauzwa kamwe

babu onyango

JF-Expert Member
Jan 12, 2023
334
813
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Ally Mangungu amekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni hivi karibuni kuwa klabu hiyo imenunuliwa na mwekezaji Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’.

Mangungu amesema hayo baada ya kipande cha video kusambaa mitandaoni kikimwonesha Mo Dewji akihojiwa na kueleza kuwa ameinunua Simba kwa dola milioni 20 (zaidi ya Tsh bilioni 51), jambo ambalo liliibua taharuki na maswali yasiyo na majibu miongponi mwa mashabiki wa klabu hiyo na wadau wa soka nchini.

Akihojiwa na EFM, Jumatano ya Machi 6, 2024, Mangungu amesema kuwa yeye si sehemu ya Mo Dewji hivyo hawezi kufafanua jambo ambalo hajazungumza yeye hivyo atasimama upande wa wanachama ambao yeye anauwakilisha ndani ya Simba.

“Hayo yanayosemwa na mimi nimeyasikia, nadhani kuna mapugufu kidogo kweye tafsiri ya maelezo ambayo yametolewa na wahusika. Mimi siwezi kumjibia Mo Dewji kwenye yale aliyoyasema kwa sababu mimi sio sehemu yake.

“Ninyi waandishi mnapenda kukimbilia kuwauliza watu mambo yaliyosemwa na watu wengine. Kama yeye ndiye aliyetoa hiyo kauli, sikutegema kama mimi ndiye nije studio kufafanua maelezo aliyoyatoa yeye, ilitakiwa ninyi mumuulize yeye. Simba haijawahi kuuzwa, haitokuja kuuzwa, Simba SC ipo

“Baada ya Mo Dewj kujitoa sana, akatoa wazo kwamba tutengeneze mfumo ambao utasaidia watu kuwekeza ili klabu iwe ya ushindani zaidi. Ndipo tukaunda Simba Sports Club Company ambayo imegawanywa katika muundo wa share ya 51% kwa 49% ambayo iliwekwa na Serikali ili kuhakikisha kuwa wanachama wanakuwa majority shareholders.

“Simba imetoa mali zake na nguvu zake kuwekeza na mwekezaji ametoa pesa zake zikaunganishwa pamoja kutengeneza mtaji ili kuendesha klabu, huo ndiyo ukweli uliopo. Mchakato huo sasa upo hatua za mwisho,” amesema Mangungu.
 
Simba imeuzwa we Mangungu acha kutuona Sisi mazuzu Simba ishanunuliwa Mo kainunua billion 51 wewe Mangungu unazo?
 
Simba Sc haijauzwa kwa yeyote, uto hangaikeni kuyalisha majini yenu yasije wakausha damu, mambo ya Simba SC tuachieni wenye chama letu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Ndugu mbumbumbu wanao bishania Simba kuuzwa au kuto ku uzwa ni viongozi wa Simba wenyewe.
Yanga haingii apo, Kwasasa Yanga wapo katika mchakato wa kutwaa Mataji ayo mengine Yana wahusu Simba.
 
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Ally Mangungu amekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni hivi karibuni kuwa klabu hiyo imenunuliwa na mwekezaji Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’.

Mangungu amesema hayo baada ya kipande cha video kusambaa mitandaoni kikimwonesha Mo Dewji akihojiwa na kueleza kuwa ameinunua Simba kwa dola milioni 20 (zaidi ya Tsh bilioni 51), jambo ambalo liliibua taharuki na maswali yasiyo na majibu miongponi mwa mashabiki wa klabu hiyo na wadau wa soka nchini.

Akihojiwa na EFM, Jumatano ya Machi 6, 2024, Mangungu amesema kuwa yeye si sehemu ya Mo Dewji hivyo hawezi kufafanua jambo ambalo hajazungumza yeye hivyo atasimama upande wa wanachama ambao yeye anauwakilisha ndani ya Simba.

“Hayo yanayosemwa na mimi nimeyasikia, nadhani kuna mapugufu kidogo kweye tafsiri ya maelezo ambayo yametolewa na wahusika. Mimi siwezi kumjibia Mo Dewji kwenye yale aliyoyasema kwa sababu mimi sio sehemu yake.

“Ninyi waandishi mnapenda kukimbilia kuwauliza watu mambo yaliyosemwa na watu wengine. Kama yeye ndiye aliyetoa hiyo kauli, sikutegema kama mimi ndiye nije studio kufafanua maelezo aliyoyatoa yeye, ilitakiwa ninyi mumuulize yeye. Simba haijawahi kuuzwa, haitokuja kuuzwa, Simba SC ipo

“Baada ya Mo Dewj kujitoa sana, akatoa wazo kwamba tutengeneze mfumo ambao utasaidia watu kuwekeza ili klabu iwe ya ushindani zaidi. Ndipo tukaunda Simba Sports Club Company ambayo imegawanywa katika muundo wa share ya 51% kwa 49% ambayo iliwekwa na Serikali ili kuhakikisha kuwa wanachama wanakuwa majority shareholders.

“Simba imetoa mali zake na nguvu zake kuwekeza na mwekezaji ametoa pesa zake zikaunganishwa pamoja kutengeneza mtaji ili kuendesha klabu, huo ndiyo ukweli uliopo. Mchakato huo sasa upo hatua za mwisho,” amesema Mangungu.
ha ha somba imeuzwa
 
Mangungu mchekeshaji tu..!!

Tangu ile video anaambiwa ajuhudhuru yeye anajimu , kwanini usianze wewe kujiudhuru.
Wakati tunafungwa 5 wewe ulikua wapi.
Nikajua huyu jamaa ni msanii wa vichekesho tu.
 
Wasipokuwa makini na tajiri Mo atakuja kuiuza timu yao kimyakimya.
 
Back
Top Bottom