Kero: TBC hamtutendei haki wananchi

Kero: TBC hamtutendei haki wananchi

Hivi nyie Wachaga mnataka kila TV iwatangaze nyie tu.... Hiyo itv haiwatoshi? na mmeongeza na channel ten sasa shida hipo wapi...wabinafsi sana nyie Wachaga kama mnafikiri media zitawapa nchi subirini muone.
 
kaka acha hasira. Apart from tbc, every private media is free to affiliate itself with a party of choice. Hata huko kwa wenzetu iko hivo. Just because hawa ipi ipaumbele CHADEMA yako usijaribu kulazimisha mambo. Hii ni free world, Kama hupendi unachokitazama, vidole vyako viko huru kubadilisha channel.

Inaonekana katika vyama vya upinzani chadema inakutetemesha mkuu, sijaona sehemu alipitaja chama yeye katumia wapinzani.
 
Kama mimi nisivyoangalia ITV EATV CH TEN na Capital.

Hizo station ulizotaja ni lazima uangalie bila kupenda penye Ukweli tuseme jamani, ITV, channel ten wanatangaza habar za ccm na wapinzani.
 
Mkuu hapo kwenye Red siyo sahihi, kuna sheria inawalazimisha broadcasters wote regardless ni private au public kuwa balanced kwenye habari za uchaguzi. Nimeweka hiyo sheria kwenye post zang huko juu.
Poa ndugu, nimeisoma, I didnt know about that. Hivyo basi jamaa wanavunja sheria wazi wazi kabisa then.
 
Sasa ulitaka vituo vya television vyote nchini vionyeshe mkutano wa chadema wkt upande wa pili kuna tukio lingine?Chadema walitaka kuwateka wananchi wote tufatilie mkutano wao wa kuwatangaza wagombea waliowaazima vyama vingine walivyosikia ratiba ya Nec kwamba tarehe 4 mgombea wa ccm anaenda kuchukua form ya urais nao wameweka mkutano wao tarehe hiyo hiyo ndio maana tv zingine zimejigawa zimeonyesha upande wa ccm.Kila mtu anahaki ya kupata habari najua chadema waliwai kulipia matangazo Azam tv,Chanel ten na Itv

Wanamaanisha taarifa ya habari mkuu sio kuonyesha live.
 
Tatizo liko TCRA ambao ndiyo wasimamizi wa hivi vyombo vya habari, kuna sheria kabisa mahususi kwa ajili ya kusimamia fairness ya vyombo vya habari kwenye uchaguzi. Nadhani TRCA hawafanyi kazi yao vizuri bado wamelala hawajajua kama tayari tuko kwenye uchaguzi. Naamini wakiona haya malalamiko watalifanyia kazi na hata vyombo vya habari wanajua penalt yake ni kubwa

kama kuna mtu anaweza kulifikisha hili TCRA walitolee maelezo anaweza kufanya hivyo naamini watalishughulikia.
Jana ITV wamefanya balance nzuri sana kwenye habari za uchaguzi na ndivyo sheria inataka wafanye.

Ni kweli mkuu wali balance upinzani na ccm.
 
Naomba kusema kuwa mtoa Uzi anapenda kuangalia na kusikia vyombo vya habari vinavyoisifia na kuiongelea vzr Chadema na ukawa,na sasa kumsifia Lowasa kwake ndio weledi.Nayasema haya coz Mara nyingi huwa naona vijana na viongozi wa Chadema wakialikwa ktk mijadala star TV,na wanapewa nafac kubwa kuchangia sasa tatizo lako ni LA kawaida,kumbuka star ni kituo cha biashara,wateja wao wakubwa ni Ccm,na hata live zote za Ccm huruka star TV,so ni wateja wao na lazima wawape nafasi,the same kwa ITV kuwa chadema ni wateja wao na ni lazima wawape nafasi kubwa wateja wao wakubwa.
 
Hivi nyie Wachaga mnataka kila TV iwatangaze nyie tu.... Hiyo itv haiwatoshi? na mmeongeza na channel ten sasa shida hipo wapi...wabinafsi sana nyie Wachaga kama mnafikiri media zitawapa nchi subirini muone.

Akili yako kama jina lako tu! Unawezaje kuongelea 'ukabilala'????!!!!
 
Comments zako zinaakisi sura ya avatar yako, ambayo nayo inaakisi udogo wa ubongo wako..
Kwa bahati mbaya huyo kwa ujinga wake na akili zake mbovu anafikiri anaijenga CCM kumbe ndiyo anazidi kuiumbua. Ngoja tu watembeze hilo kufuli, funguo ziko UKAWA.
 
TBC ovyoooo!Naangalia taarifa za mikoani ss hivi yani ni upuuzi wa hali ya juu.Wametangaza kuwa wanaohama CCM eti wametumia hela nyingi hivyo zinawauma na wamepeleka habari mtwara kwa Magufuli dk 2 nzima ila hakuna habari yoyote ya wizi wa kura za maoni CCM huko mikoani,kuhama kwa viongozi CCM Mbeya,Arusha n.k..Afu eti kuna habari ya semina kwa waandishi na vyombo vya habari kuwa fair na kutumia kalamu zao vizuri.
Hili shirika ni la ovyo sijui wanadanganya umma UPI??
 
hicho si chombo cha Umma tena bali kimekuwa ni sehemu ya CCM kupelekea matangazo yake ninacho washangaa hawa jamaa hawasomi upepo unanenda wapi mkurugenzi wake sasa atakuwa na kibarua kigumu sana endapo Wana mapinduzi tutakapochukua nchi inabidi wabadilike mana hawako pale kwa hela za CCM bali ni kodi za wananchi ambao ndio tunahitaji kupata taarifa.
 
TBC ilikuwepo enzi za TIDO MHANDO.sasa ni ya ovyo ovyo sana.nikikumbuka tbc ya Tido na vipindi murua vya uchaguzi majimboni it was excellent.sasa hivi sijui ni viandishi na vikurugenzi uchwara !?nashindwa kuelewa.
 
TBC ovyoooo!Naangalia taarifa za mikoani ss hivi yani ni upuuzi wa hali ya juu.Wametangaza kuwa wanaohama CCM eti wametumia hela nyingi hivyo zinawauma na wamepeleka habari mtwara kwa Magufuli dk 2 nzima ila hakuna habari yoyote ya wizi wa kura za maoni CCM huko mikoani,kuhama kwa viongozi CCM Mbeya,Arusha n.k..Afu eti kuna habari ya semina kwa waandishi na vyombo vya habari kuwa fair na kutumia kalamu zao vizuri.
Hili shirika ni la ovyo sijui wanadanganya umma UPI??

mkuu bado unaangalia TBC.hii inakuwaga TV ya chooni
 
Nyamafu Kati ya tbc na itv .nani anaeye pendelea zaidi ?uchimbi wa itv hamuoni mnaona wa tbc? Ndorobooo


tbc ni vyombo vya habar vya umma ambavyo vinatakiwa kuripot na kuhabarisha habar zote za nchi hii pasipo upendeleo wa aina yoyote, <sababu wafanyakazi wanalipwa mishahara na pesa za kuendeshea vipindi ambazo ni kodi za wananchi>

ITV ni chombo cha habar cha mtu binafsi ambaye kwa gharama zake ndiye anayelipa mishahara na gharama za kuendeshea vipind, hivyo hafungwi {does not tied to} na jamii nzima ya watanzania,yuko huru ktk habar zake (i.e kuegemea kwa mtu\kund flan au vyovyote vile)
 
Napata wakati mgumu sana kuamini kuwa hili shirika ni la umma. Kuelekea uchaguzi mwaka huu kituo hiki cha televisheni kimekuwa kikiripoti habari kwa upendeleo wa hali ya juu yaani hata kufika mahali na kupotosha jamii ya waTz.Hivi najiuliza TBC wanadhani tuko miaka ya 70? Au wana mawazo mgando na finyu kiasi hiki?? Yaani hata kuripoti habari mfano za upinzani au Lowassa ni kwa uzandiki na urapurapu(ikitokea zimeripotiwa).

Mikutano ya CCm inarushwa live na makolombwezo meeengi..Hivi mnamdanganya nani? Mtz wa leo anajua na ndo maana anajiandikisha afanye maamuzi. Onyesheni kwa uwiano, Tz ya leo inahitaji ukweli na usawa ktk habari.

Mkuu pole sana umeandika kwa hisia juu ya chombo ambacho kinaendeshwa na kodi za watanzania,lkn hali halisi ni kuwa tbc imetia pamba kwenye masikio yake kwani imelalia kwenye chama tawala.
 
Back
Top Bottom