January Makamba: Bila Magufuli CCM ilikuwa imekataliwa na wananchi Uchaguzi 2015

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866

Akiongea na kituo cha Taifa cha Utangazaji(TBC),Mbunge wa Bumbuli na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano,Ndugu January Makamba,amesema katika uchaguzi wa mwaka 2015 CCM ilikuwa inaondoka madarakani kwa nguvu ya wananchi,lkn kwa uchaguzi wao wa kumchagua ndugu JPM kidogo imani ya wananchi ikarudi kwa Chama Cha Mapinduzi.
Makamba Jnr anasema CCM ilipoteza imani na kutoaminiwa na wananchi kwa kiasi kikubwa sana kiasi cha wao kuona dalili la wazi la kuanguka kwa CCM.Anasema uchaguzi wa 2015 ulikuwa ni moja ya chaguzi ngumu kuwahi kutokea na wana imani kwa utendaji huu wa JPM wananchi watarudisha imani kwa CCM na Serikali yake na kuepuka kuwaadhibu ktk sanduku la kura mwaka 2020.
 
Wangeondoka vipi madarakani wakati kama wangenusa kushindwa kwa chama chao wangefuta matokeo kama walivyofanya Zanzibar?
Wamepoteza heshima kubwa mbele ya umma na Kimataifa kwa yale waliyoyafanya Zanzibar

Exactly!

Kama wangenusa harufu ya kushindwa wangefanya mizengwe tu.

Hivi kwani unadhani hawajui faida za kuwa na tume ya uchaguzi waliyoiunda wao?

Unadhani hawajui faida za katiba ya sasa licha ya mapungufu yake?

Wanajua sana na ndo maana wala hawana mshawasha wa kubadili hali iliyopo.

Wenyewe wanakwambia tume ya uchaguzi ni huru [huku inateuliwa na mwenyekiti wa chama chao].

Hao jamaa hawana akili nzuri kabisa. Hata simile hawana.
 
Aisey! Kwa hiyo angechaguliwa yeye alikuwa anakwenda kushindwa! Kwa nini alichukua fomu kama alilijua hili? Haya ni maajabu yaani kutoka uwezekano wa kushindwa mpaka kupata karibu 3/4 ya wabunge na ushindi wa karibu asilimia 60 za kura za uraisi, kisa ni kuvhagua mtu mwafaka tu! Sina hakika kama maelezo yake ni sahihi sana.
 
Ni kweli ccm imechokwa na watanzania wengi lakini ni wale wenye uelewa tu wa mambo. Walio wengi ambao ni maskini wa kutupwa na wenye uelewa mdogo wa mambo bado wataendelea kuichagua ccm na hao ndio wengi. Ukichanganya na tume kuwa chini ya ccm, jeshi la polisi kujiona ni kama zilivyo taasisi za ccm kama uvccm nk ni ngumu upinzani kutwaa dola. Kwahiyo kujifanya eti bila Magufuli ni kama anajaribu kutuaminisha kwamba ushindi wa ccm uliletwa na Magufuli pekee. Huko vijijini bado ccm inashinda hasa kwa vitisho, rushwa nk. Na ukiangalia wapiga kura wengi wako vijijini na hao ndio mtaji wa ccm.
 
Makamba, Tungekuelewa kama ungetuambia bila tume ya uchaguzi kuwa ya ccm, nchi ilishaenda upinzani.
Lazima mkubali kuwa kumchukua lowassa na sisiemu kumsimamisha magufuli ni chanzo cha chadema na ukawa kwa ujumla kudondokea pua, huo ndo ukweli, vinginevyo ni UPUMBAVU NA UJINGA wa kushindwa tu ndo unawasumbua.
 
Ni kweli ccm imechokwa na watanzania wengi lakini ni wale wenye uelewa tu wa mambo. Walio wengi ambao ni maskini wa kutupwa na wenye uelewa mdogo wa mambo bado wataendelea kuichagua ccm na hao ndio wengi. Ukichanganya na tume kuwa chini ya ccm, jeshi la polisi kujiona ni kama zilivyo taasisi za ccm kama uvccm nk ni ngumu upinzani kutwaa dola. Kwahiyo kujifanya eti bila Magufuli ni kama anajaribu kutuaminisha kwamba ushindi wa ccm uliletwa na Magufuli pekee. Huko vijijini bado ccm inashinda hasa kwa vitisho, rushwa nk. Na ukiangalia wapiga kura wengi wako vijijini na hao ndio mtaji wa ccm.
Sisiemu itaendelea kuchaguliwa na kuongoza as long as upinzani ni wapumbavu wasio na msimamo, hivi hamjui kabisa sababu ya kushindwa urais au mnatafuta mchawi? Msiwe wapumbavu, lowasa kawagharimu, mbowe na maamuzi yake kawagharim. Na magufuli kawagharim.
Mbowe and Co. Anajua hilo!
 
Mwaka 2010 pia aligombea Lowassa? Mbona bado ccm ilishinda chini ya dhaifu?
 
Mwaka 2010 pia aligombea Lowassa? Mbona bado ccm ilishinda chini ya dhaifu?
Mwaka 2010 sisiemu haikuwa ktk hali mbaya kama mwaka huu, mwaka huu ni kweli watu walikuwa wameichoka sisiemu nikiwapo MIMI, ila walipomchagua Magufuli awe mgombea wao ndo mtu pekee wa sisiemu ambaye ningempa kura yangu, hivyo baada ya Magufuli kichaguliwa nikawa nasubiri chadema wanatuletea nani, eti wakamleta lowassa! Hii ni kwangu na wengine wengi. Hivyo 2010 sisoemu ilikuwa imechoka ila upinzani walikuwa hawajakaa sana, na mwaka 2015 sisiemu walipojikanyaka badala ya chadema kuitumia fursa wakaleta mtu AMBAYE WAO WENYEWE CHADEMA WALIMPONDA NA WALISABABISHA WATU WASIIPENDE SISIEMU.
 
Back
Top Bottom