Kero: TBC hamtutendei haki wananchi

Kero: TBC hamtutendei haki wananchi

Habali,
ladhi
Hata habari yenyewe imetoka utamu!
 
Tatizo hawa jamaa wa TBC wanasahau kuwa posho na mishahara yao inatokana na kodi za watanzania wote ambao wengine si hata wanachama wa upinzani wala ccm....cha msingi wawe fair na si kuwa upande mmoja..wana nidhamu ya uoga ndo maana wanakuwa biased...uoga si maadili ni upumbavu wa hali ya juu...lazima wajitambue kuwa TBC ni television ya TAIFA na si ya CCM wala vyama vya UKAWA....
 
Hv mwataka kila kituo kiwe kinaonesha ukawa? Angalia ITV ili ufurahie maana ni ya mrengo wako mfano swali la kipima joto huwa wanawahoji watu wenye mitazamo tofauti ila wanaonesha wenye mrengo wao na wasio na mrengo wao hawaoneshwi!
 
Kuna Mtu Mwenye Akili Timamu Anatizama TBC? MI TANGU AONDOKE TIDO MHANDO SIJAWAHI TAZAMA NA SIIJUI KAMA BADO IPO HEWANI.
 
Tunaiomba serikali isianze kufanya upendeleo Wa kutangaza habari Na matukio mbalimbali ya vyama kwa kukipendelea chama cha mapinduzi CCM .Imetubidi tuseme hivyo kutokana Na kituo hicho kushindwa kutangaza habari za Chadema Leo katika tukio la kumtambulisha mgombea wake huko Mwanza lakini tukio la Mgombea uraisi Wa ccm la kuagana Na wajumbe Wa halmashauri Kuu ya ccm lilitangazwa.TBC ni chombo cha SERIKALI sio cha CCM kwa hiyo kitende haki.
 
Mkuu usipoteze muda kuangalia tbc mi hapa natafuta jinsi ya kuiondoa tbc kwenye kisimbusi changu.
 
Mie TBC hua naangalia ile muvi ya vita vya kagera OVER....
Habari usiajgalie uko....sio TBC tu ata star tv channel ten na Tv1 nao wametishiwa....
mfano leo star tv ndo TV iliopo mwanza lakin ktk habari yake wameonesha jinsi police walivyopiga mabomu na kuonesha jinsi LOWASSA alivyoshuka uwanja wa ndege basi lakini jins leo mji wa mwanza ulivyokua umejaa watu na ata Furahisha kwenye mkutano watu walivyokua wengi HAWAKUONESHA....Nawapongeza channel 10 waneonesha habari vizuri japo ulikua mwishon
 
Kwa vipindi kadhaa kumekuwa na matukio mengi ambayo wananchi tulipaswa kuyaona na kuya sikia live toka ktk kituo cha taifa cha utangazaji lkn unaobekana kituo hiki ambacho ni TBC kina elemea upande mmoja wa taarifa hususan chama cha mapinduzi yaani CCM.

Sasa sisi wananchi wenye hakivya kuhabalishwa kupitia local chammels kwa kushindwa gharama za Azam tv ambayo umekuwa wazi kuonyesha kila kitu bila ubaguzi sasa .

Nawaachia swali Vp kama ukawa ukachukua nchi je ? Mkurugenzi na wafanyakazi kwa hizi chuki za wazi kwa matukio ya wapinzani mtabaki hapo kazini? Na kwann muendelee kuwa kipeperushi cha chama fulani?

Kwanini msiwe fair kwa wote?

Hamtutendei haki kam chombo cha taifa..jana mlirusha kipindi cha miziki ya ajabuajabu wakati wa tukio la chadema kitu amvacho mngeweza kurusha live, lkn hamkuthamini.

Hebu tuangalie tuhuma hizi kwa wananchi na mtusaidie katika hilo
.
Asante.

Kungekuwa na option ya kudelete ningeidelete kwa list kabisa
 
Sasa ww ulitegemea warushe habari za ukawa au chadema tambua kuwa TBC ni kituo kinachomilikiwa na serikali iliyopo madarakani na serikali iliyopo madarakan ni ya ukawa au ya chadema nauliza kwako mleta uzi? Lazima iwe ya chama kilichopo madarakani kwhyo usiumie subiri kama na ww utapata mamlaka ya chama chako kuwepo mjengoni pale mtayatekeleza yakwenu kwa xx achen tu ccm ifanye inavyotaka hupend usifungulie tbc

Umajua mimi siwezi walaumu sana hao watu wa tbc maana huwenda na wao wanapewa maelekezo na wakubwa zao ili walinde ugali wao,lkn naomba nitoe ushauri wa bure kwao kwa uelewa wa mtaanzania wa leo nawashauri si kila wanaloambiwa walifanye watumie na akili zao pia siyo za kuambiwa maana siku ukawa wakishika dollar itakula kwenu pia so as longer as pesa inayowalipa nyie tbc inatokana na kodi za hao hao wananchi tendeni haki. na kama mnataka kuficha hayo madudu yenu yasionyeshwe tunyanganyeni simu zetu na ikibidi fungeni na mitandao ya cm yote.
 
Naomba nisema ukweli kipindi Tido kaja kufanya restructuring ya TBC nilikua msikilizaji namba moja lakini cha kusikitisha Tido kakomaa kulifufua shirika Serikali haikumuongeza mkataba maksudi.

Matokeo yake shirika limekosa mvuto linaongozwa na chama tawala kinavotaka chenyewe habari zitolewazo ni unbalance wanaegemea upande mmja wakijua kua watazamaji wengi ni wa mijini ambao wanajua siasa, hivyo imepelekea kuichukia hii runinga.

Nitoe rai yangu TBC nyinyi ni kituo cha Taifa toeni tarifa balanced muone kama kuna watu watawachukia vinginevyo mtapiga maktme mpaka mwisho.
 
Mbona tbc ilishajiua makusudi kama gazeti la uhuru,mzalendo,habari leo,jambo leo na tazama,mkakati.
 
Mimi nina miezi sita wala sijatia TBC machoni pangu. Siku moja mtoto alifungua TBC kwa bahati mbaya nikakuta ile sherehe ya Wizara ya ujenzi wa kumuaga mhe Rais ikiendelea mara moja nikamuagiza aweke ITV inayopendwa na wengi. Sitaki hata kuitazama kabisa.
 
hapa watu wamebaki kuangalia kipindi cha vichekesho tu vya Joti na Masanja, wakitoka hawa, watabaki wa ccm na wazee wa zamani wanaokumbushwa vita vya Idd amni dada kuwakumbusha machungu wale waliopoteza watoto wao na hawakulipwa chochote, sisi tuliobaki yatima hatutaki habari hizi bali ukombazi makini, kutoka kwa magagula Maccm
 
Back
Top Bottom