Kenya: Umeme wakatika nchi nzima na kuacha abiria kwenye uwanja wa ndege wa JKIA wamekwama

Nyasi-Man

Member
Sep 3, 2023
61
86
Wakati Tanzania ikishuhudia mgao wa umeme maeneo mengi ya nchi, huko Kenya hali ya upatikanaji wa umeme pia imekuwa kizingimkuti. Jana tarehe 10/12/2023 umeme ulikatika nchi nzima na kuathiri shughuri za uwanja wa Ndege wa JKIA, huku backup jenereta pia zikishindwa kuwaka hali iliopelekea giza zito kutanda nchi nzima na kukwamisha Abiria.

JKIA ni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa lakini hukumbwa na kukatika kwa umeme mara kwa mara na kuhatarisha usalama wake na ule wa nchi bila kusahau ni kutoka hapa ambapo KQ inasafiri moja kwa moja hadi Marekani na Uingereza.

Je, ni lini utawala wa Ruto utapata muarobaini wa aibu hii? Uzembe kama huo unaendelea kuifanya Kenya kuwa kicheko kikanda na kote ulimwenguni.

WhatsApp Image 2023-12-11 at 1.33.58 PM.jpeg
 
Back
Top Bottom