Wakenya wapata ladha kidogo ya mgao wa umeme jana 10/12/2023

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Jana Jumapili jioni 10/12/2023 Kenya ilikumbwa na mgao ulioathiri nchi nzima na kusababisha huduma kusimama katika sehemu zote za nchi.

Tatizo hilo lilianza majira ya saa mbili usiku na ilikuwa ni mara ya tatu kutokea likiathiri nchi nzima katika miezi mitatu iliyopita

Miongoni mwa taasisi muhimu ambazo huduma zake zilisimama ni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi, ambapo mitambo ya umeme ilishindwa kuanza tena.

Kampuni ya Kenya Power iliihusisha kukatika kwa umeme na kile walichokiita "usumbufu wa mfumo," ambao walisema unashughulikiwa na mafundi.

Wakati wa hitilafu kama hiyo mnamo Novemba 11, ilichukua zaidi ya saa 12 kurejesha nguvu katika maeneo mengi ya nchi.

Mwanahabari mashuhuri wa kimataifa wa Kenya Larry Madowo amelalamikia hitilafu za umeme za mara kwa mara ambazo zinaathiri uwanja mkuu wa ndege wa kimataifa nchini Kenya, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta almaarufu JKIA

“Kumekuwa na hitilafu tatu za umeme JKIA tangu nilipofika hapa saa moja iliyopita. Ninapitia takriban viwanja 50 vya ndege vya kimataifa kwa mwaka. Huu ndio pekee ambao nimeona ukipoteza umeme, na mara kwa mara," alisema

===

A nationwide power blackout hit Kenya on Sunday evening, paralysing services all across the country.

Sunday’s outage began around 8 PM and was the third national power supply failure within the last three months.

Among the key establishments whose services were paralysed is the Jomo Kenyatta International Airport (JKIA) in Nairobi, where the power generators failed to pick up yet again.

Kenya Power attributed the blackout to so-called system disturbance which they claimed was being addressed by technicians.

During a similar outage on November 11, it took over 12 hours to restore power in most parts of the country.

Citizen Kenya
 
Back
Top Bottom