Paa la uwanja wa ndege Nairobi linavuja kama nje

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,488
20,445

Lawama kuhusu paa zinazovuja katika uwanja mkuu wa ndege wa Kenya​

Waziri wa uchukuzi wa Kenya na mamlaka ya viwanja vya ndege wamekabiliwa na shutuma mtandaoni kufuatia malalamiko ya kuvuja kwa paa kwenye vituo vya uwanja mkuu wa ndege wa Jomo Kenyatta.
"Mmoja wa wanachama wa timu yetu alikumbana na hali hizi zisizo za kawaida JKIA. Labda wasimamizi katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege vya Kenya wanaona hili kama jambo la kawaida na linalokubalika,” ilisema kampuni ya utafiti wa kifedha ya Mwango Capital katika video inayoonyesha mvua ikinyesha kwenye paa juu ya eneo la kuingia na kupita kwenye kituo.

"Tuliona ni bora kuifahamisha umma ili kuchukua hatua," kampuni hiyo iliongeza, katika ujumbe ambao imeushirikisha kwenye jukwaa la mtandao wa kijamii X (zamani Twitter) siku ya Jumatatu.
Ujumbe huo ulisababisha malalamiko zaidi kuhusu hali mbaya ya uwanja wa ndege, ambayo imekuwa mbaya zaidi kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Uwanja huo wa ndege pia ulikabiliwa na ukosoaji wikendi iliyopita baada ya usimamizi wake kutangaza kuwa ilichukua dakika 20 kurejesha umeme huko, kufuatia kukatika kwa umeme kote nchini Kenya kwa saa chache Jumamosi usiku.

Si mamlaka ya viwanja vya ndege wala waziri wa uchukuzi aliyetoa maoni yake kuhusu malalamiko hayo.
Wiki jana, Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen aliahidi kuboresha huduma katika uwanja huo wa ndege, baada ya malalamiko tofauti ya kudhulumiwa kwa abiria na maafisa wa ushuru.
1699983641160.gif

1699983641160.gif
 
Back
Top Bottom