#COVID19 Kenya na Mlipuko wa Covid-19: Nini faida na hasara za kujifunza kwa maamuzi ya haraka waliyochokua?

Dr Mathew Togolani Mndeme

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
201
808
Hali ya maambukizi ya Covid19 duniani hadi kufikia 16/03/2020
1584395567565.png

Kenya wamethibitisha uwepo wa watu 3 wenye Covid19 na tayari leo Rais Kenyatta katangaza kufungwa kwa shule na taasisi zote za elimu nchini kuanzia kesho.

Pia amefunga mipaka yake kwa raia wa nchi yoyote ambayo imeshatangaza kuwa na mlipuko wa Covid19 ndani ya siku mbili zijazo. Kama vile haitoshi, kawataka waajiri wawaruhusu wafanyakazi wao wafanye kazi wakiwa majumbani na watu wapunguze usafiri wa umma kama sio lazima.

Katika hatua nyingine, kashauri manunuzi na malipo yafanyike zaidi kwa njia za kielekroniki (simu na kadi za benki) ili kuzuia maambukizi kwa kushika fedha.

Kwa kuwa tatizo la Covid19 bado linaendelea na kwenye nchi zetu za Afrika ndio kwanza linabisha hodi, nadhani ni muhimu kujiuliza faida na hasara ya uamuzi waliochukua Kenya maana ni wazi uamuzi wao utaigwa na nchi nyingine nyinge za Afrika.

Maamuzi ya hatua za kuchukua kwenye mlipuko
Kwenye kupambana na magonjwa ya kuambukiza ya mlipuko kama Covid19, kuna mambo mengi ya kutazama katika kuchukua hatua za kukabiliana na tatizo.

Kila hatua ya mlipuko inahitaji kutazamwa vema kujua ni njia gani inafaa kwa hatua husika. Kuzuia mikusanyiko na kufunga mipaka ni hatua kali na za ngazi ya juu sana.

Zinapatikana pale tu mlipuko unapokua umesambaa sana na madhara yake yamekua makubwa. Katika kufikia maamuzi ya hatua za kuchukua kuna maswali kadhaa ya kujiuliza.
  • Hali ya mlipuko ikoje?
  • Uwezo wa mfumo wa kutoa huduma za afya kukabiliana na mlipuko ukoje?
  • Tunataka kudhibiti nini na kwa kiasi gani?
  • Je, mlipuko umefikia kiwango gani cha maambukizi?
  • Tunategemea kilele cha maambukizi kitafika baada ya muda gani?
  • Tunakadiria kutakua na wagonjwa wangapi mlipuko utakapofikia kileleni na Tunakadiria vifo vingapi?
  • Ni kundi gani kwenye jamii liko kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa na/au kuathirika na maambukizo?
  • Mfumo wa kinga kwa ugonjwa husika ukoje?
  • Hatua tunazochukua zitakua na athari gani kwenye maisha ya mtu mmoja mmoja, familia, jamii, na uchumi wa nchi kwa muda mfupi na muda mrefu?
  • Hali ya wananchi wetu ikoje kwa muktadha wa mlipuko husika (kielimu, kiuchumi, nk)?
Kenya wanasema watu 2 wenye maambukizi wanahusina au walisafiri na mgonjwa wa kwanza ambaye aliingia na Covid19 akitokea Marekani kupitia Uingereza ambako tayari tatizo ni kubwa.

Wagonjwa wote hawa wamegundulika ndani ya siku tu 4 zilizopita. Kwa ugonjwa unaoambukiza kwa haraka kama Covid19, hii ni hatua ya mwanzo kabisa ya mlipuko katika nchi.

Ndio kwanza virusi vimeanza kuweka makazi ndani ya Kenya vinatazama vikatize mitaa gani. Katika hatua hii, kwa kuanzia, serikali ilitakiwa kuchukua hatua kama nne za msingi.
  • Kujikita zaidi katika kutoa elimu kwa jamii kulielewa tatizo kwa undani, ukubwa wake, na namna ya kujikinga kwa mtu mmojammoja na kama jamii.
  • Kuanza kufanya maandalizi ya kutosha (kwa maana ya vifaa, wataalamu, fedha, nk) kuwezesha hospitali na mifumo mingine ya utoaji huduma za afya kuwa tayari kukabiliana na mlipuko unapoelekea kwenye kilele (watu wengi kuugua na/au kufariki kwa wakti mmoja).
  • Kufuatilia kwa karibu mnyororo wa maambukizi na kujaribu kudhibiti kuenea zaidi kutoka kwa wale ambao wameshaupata.
  • Kuwaandaa wataalamu wa magonjwa ya mlipuko na wanasayansi wengine ili wafuatilie kwa karibu hali ya mlipuko kila siku na kushauri nini cha kufanya kulingana na ushihidi wa kisayansi.
Tatizo la maamuzi Kenya liko wapi?
Ni kwa bahati mbaya kwamba wataalamu wa Kenya na viongozi wameona waanze na kuzuia mikusanyiko. Kikubwa kitakacholetwa na maamuzi haya ni hofu na mshtuko, kwani kwa mwananchi wa kawaida, yanaashiria kwamba hali ni mbaya kupindukia.

Hali kadhalika, kwa maamuzi haya, ni vigumu kujua hali ya mlipuko itakavyokua, utaenea wapi zaidi, utawapata kina nani zaidi, na madhara yatakua kwa kundi gani na kwa ukubwa gani.

Hii ni hatua ambayo mchango wa watafiti wa sayansi na watu wenye tafakuri tunduizi na pana ya hali ya nchi, wangetakiwa kupewa nafasi zaidi ili kila uamuzi unaochukuliwa na serikali kukabiliana na hali uwe una ushahidi wa kisayansi na matokeo yake kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutabirika.

Pia, serikali ya Kenya imechukua hatua nyingi kwa wakati mmoja jambo litakaloleta ugumu sana kujua ni hatua ipi kati ya hizo inafanya kazi namatokeo yake yanaonesha kuna tija.

Katika kukabiliana na hali ya hatari, ni vema kutumia mbinu za kijeshi zaidi (military strategies) ambapo unakua na mkakati mkuu unaotumia kukabiliana na adui halafu unatazama nini cha kufanya iwapo mkakati mkuu hautafanya kazi (worse case scenario).

Kwa sasa, iwapo maamuzi waliyochukua yatafanya kazi au vinginevyo, itakua ngumu sana kujua ni njia gani imekua na tija au ni ya ovyo.

Ushahidi wa kisayansi unasemaje. Moja, hauoneshi kwamba kukimbilia kuzuia mikusanyiko ya watu kunasaidia kupunguza tatizo kwa haraka.

Mbili, ushahidi ulioko hadi sasa kuhusu maambukizi ya Covid19, unaonesha watoto sio waathirika wakubwa unapolinganisha na watu wazima.

Haijajulikana kama wana kinga zaidi au ni mazingira gani lakini wanaoathirika hadi sasa ni wachache sana kote ugonjwa ulipogundulika.

Hivyo kufunga shule za msingi na sekondari kunaweza kuwa na matokeo finyu sana ya kupunguza maambukizi hasa katika hatua hii.

Tatu, ugonjwa ukishatangazwa kwamba ni janga la kimataifa (pandemic) na uko ndani ya nchi yako, hakuna ushahidi wa kutosha kisayansi unaonesha kwamba kufunga mipaka kunasidia kupunguza madhara.

Nne, unapoamua kuchukua hatua kama vile watu wasikusanyike, wanafunzi wasiende shule, usafiri wa umma kusimamishwa, kuzuia ndege zinazongia, na kufunga mipaka; ni lazima pia uwaze hali ya maisha ya wananchi itakuwaje na iwapo madhara yatakua makubwa kuliko yale ya kukabiliana na mlipuko. Kwa mfano:
  • Nani atakaa na watoto wadogo wasiokwenda shule kwa muda usiojulikana wakati wazazi wanatakiwa kwenda kazini?
  • Je, watu wakiacha kwenda kazini mapema hivi, waajiri bado watakua na uwezo wa kuwalipa mishahara wakati hawafanyi kazi?
  • Kenyetta amewaambia waajiri wawaruhusu watumishi wao wafanyie kazi nyumbani. Lakini je, hali ya kazi na maisha ya Kenya yanaruhusu kwa kiasi gani kufanya kazi kutokea nyumbani? Maagizo haya nayaona kama ni ya kuiga kwa wanachoshauri nchi za magharibi. Kule, internet ni moja ya mahitaji muhim nyumbani kama vile bomba la maji au umeme na siyo ya kupima kama vifurushi vya tigo; na kompyuta sio kifaa kigeni kwenye familia. Tujiulize, Kenya ina wafanyakazi wangapi wenye uwezo wa kuwa na internet ya kutosha nyumbani na wanamiliki kompyuta binafsi kuwawezesha kufanya kazi nyumbani? Aina ya kazi zilizoajiri watu wengi, zinaweza kufanyika nje ya maeneo ya kazi?
  • Gharama ya kukatisha utoaji wa elimu kwenye ngazi zote kwa muda usiojulikana, utaathiri vipi taifa?
  • Wakenya wangapi wana maji safi ya bomba nyumbani na sabuni kuwawezesha kunawa mikono kila mara kama inavyoshauriwa?
  • Je, Kenya ina mfumo unaotambua kila mwananchi na anapoishi, achilia mbali makundi hatarishi kwa ugonjwa huu kama wazee?
Changamoto ya mlipuko wenyewe
Jambo lingine la kutazama ni maambukizi munayotaka kuyakabili. Kuwaambia watu wakae nyumbani kuna uwezekano mkubwa wa kuzuia maambuzi kwa kasi lakini ukasababisha tatizo lingine.

Bado wanasayansi hawana uelewa wa kutosha kuhusu Covid19. Kwa mfano, bado haijuilikani ni kwa kiasi gani kila anayeumwa anaweza kutengeneza kinga kama ambavyo imezoeleka kwa magonja mengine ya virusi.

Bado hatujui iwapo kinga inayojengeka kwa ambaye ameshaumwa itamkinga asoiugue tena ndani muda gani. Bado hatujui vya kutosha iwapo aliyepata virusi na akapona hatarudiwa ndani ya muda mfupi.

Hivyo, watu wakianza kujifungia mapema kuna uwezekano mkubwa mukashindwa kupata uelewa wa kutosha kuhusu maambukizi yanavyoenea, athari zake, na hatua za kuchukua.

Pia, virusi vinaweza kuchukua likizo (incubation) vikapumzika tu huku mukidhani mumedhibiti mlipuko. Ila watu watakapoanza kutoka na kuchangamana tena, tatizo likaanza upya kwa kua kuna wengi wasio na kinga.

Maisha ya virusi, wanavyosambaa, na mwitikio wa mwili wanapotushambukia, ni moja ya sayansi ngumu sana kuitabiri. Virusi wengi wana tabia ya kubadilika pamoja na athari wanazosababisha.

Kwa magonjwa ambayo tumeweza kutengenza kinga kama Surua, polio, na mengine, watu wanapewa chanjo ambayo inawasaidia kutengenza kinga kwa muda mrefu.

Utoaji wa chanjo hii hutengeneza kitu kinaitwa kitaalamu kama “kinga ya kijamii” (Herd/ community immunity). Kinachotokea sio kwamba virusi, kwa mfano vya surua, wametoweka Tanzania, bali ungojwa hauonekani kwa sababu watu wengi kwenye jamii wana kinga dhidi ya virusi hivyo kupitia chanjo.

Hivyo kunapotekea mlipuko (mtu au watu wasio na kinga kupata Surua) ugonjwa unashindwa kusambaa kwa sababu watu wengi wanaokutwa na kirusi wanakua na kinga.

Hivyo nao wanawakinga hata wale ambao hawana kinga maana ugonjwa hautawafikia.

Kwa mfano, nchi kama Marekani na Uingereza kuna watu wengi hawataki watoto wao wapate chanjo kwa madai kwamba chanjo zina madhara kiafya au wana imani kwamba kuna hujuma inafanywa kupitia chanjo.

Hivyo kuna maelfu ya watoto hawajapata chanjo. Ndio maana pamoja na kwamba nchi yetu tumetokomeza kabisa Surau, mwaka jana Surua iliathiri watu wengi Marekani na mwaka juzi ilikuwepo baadhi ya maeneo Uingereza.

Kwa nini walipata pamoja na maendeleo yao? Bado virusi vya surua vipo. Ila kinachowakinga wale ambao hawajachanjwa, ni uwepo wa watu wengi wenye kinga (herd/community immunity). Lakini ikatokea kirusi kikakutana na mtoto ambaye hana chanjo, atapata ugonjwa na ataambukiza wengine wa aina yake huko shuleni.

Sasa kwa habari ya Covid19, bado haina kinga na itachukua muda mrefu kinga kupatikana. Kinga pekee ambayo tunaweza kuipata kwa sasa itakayosaidia watu wengi, ni kinga ya kijamii.

Na kinga hii itapatikana pale tu ambapo watu wengi watapata maambukizi na kupona. Hawa wakishapona, wanatengeneza kinga ambayo itasaidia kuukata mnyororo wa maambukizi na hivyo kuwakinga hata wale ambao bado hawana kinga.

Tukumbuke pia kwamba sio kila mtu ana uwezo wa kutengeneza kinga anapopata maambukizi. Hii inatokana na sababu za kiafya, umri, na hata sababu za kibayolojia za mwili zinazoweza kumfanya kuwa na uwezo mdogo wa kutengeneza kinga.

Ndio maana watu wengi waliofariki kwa Covid19 hadi sasa ni wazee ambao kinga yao ni ndogo au ambao tayari walikua na magonjwa mengine yanayodhoofisha uwezo wao wa kutengeneza kinga. Nihitimishe kwa kujaribu kujibu maswali niliyoanza nayo.

MOJA: Nini faida ya hatua walizochukua Kenya?
  • Iwapo hatua zilizochukuliwa zitafanikiwa, wanaweza kudhibiti maambukizi kutowapata watu wengi na kutosambaa sehemu kubwa ya nchi.
  • Mfumo wa utoaji huduma za afya unaweza kukabiliana na tatizo kirahisi zaidi maana hatua hizi zitachelewesha mlipuko kufikia kilele mapema au kikafika kikiwa na maambukizi kidogo.
MBILI: Nini hasara za maamuzi haya?
  • Ni mapema sana kuchukua hatua kubwa kama hizi kwa kiwango cha maambukizi waliyonayo sasa. Hii ni sawa na kuanza vita na adui mukitumia SMG na AK47 kisha siku ya pili wewe unaamua kuibuka na mabomu ya maangamizi huku ukiwa hata hujajua nguvu ya adui yako na uwezo wake.
  • Kenya watashindwa kupata ufahamu wa kutosha kuhusu tabia na mwelekeo (behaviour and pattern) wa maambukizi na madhara yake.
  • Kwa kukosa uelewa wa kutosha, hatua watakazochukua zinaweza zisiwe za wakati sahihi na tija inayotegemewa ikakosekana.
  • Kuna uwezekano mkubwa maambukizi yakachelewa kufikia kilele na na mlipuko kudumu kwa muda mrefu. Ili mlipuko udhibitiwe, ni lazima ufikie kilele cha maambukizi kwanza na kikifika kwa haraka ni nafuu zaidi kwani tatizo litakwisha ndani ya muda mfupi. Unapochelewesha, hofu itaendelea kuwepo kwa muda mrefu na mikakati ya kukabili inaweza isiwe na tija.
  • Hali ya maisha ya wakenya wengi itaathirika sana na serikali haina uwezo wa kuwasaidia waathirika.
  • Hali ya uchumi inakwenda kutikisika vibaya sana kwani hakuna miundombinu ya kutosha na mbadala kuwezesha uzalishaji kuendelea watu wakikaa nyumbani.
  • Itachukua muda mrefu jamii ya wakenya kupata kinga ya Covid19 (herd/ community immunity) na huenda kukawa na hatari ya ugonjwa kujirudia kila baada ya muda fulani kutokana na tabia za kirusi ambazo bado hatujazielewa vya kutosha.
Nimalizie kwa kusema, hatua walizochukua Kenya zinaonekana ni za kisayansi lakini zimechukuliwa kwa msukumo na wakati usio sahihi. Inaonekana hofu/kuchanganyikiwa (panic) imekua kubwa; wanasiasa na washauri wao wamekua na haraka ya kuonesha wanafanya kazi; huenda wamesukumwa zaidi na maoni ya umma (public opinions) kuliko utaalamu/sayansi; baadhi ya hatua wameiga kwa nchi nyingine bila kuangalia hali halisi ya nchi yao.

Inawezekana pia, walichokifanya Kenya kinadhihirisha hali yetu waafrika ambapo mara nyingi tunafanya maamuzi bila kutazama mbali sana maana tunakua na haraka ya kutafuta suluhisho kwa matatizo ya leo kila iitwapo leo na ndio mana hatuifikii kesho tunayoitamani.

Ushauri
Ni ushauri wangu kwamba iwapo tatizo hili litaingia nchini kwetu (Mungu aepushe) viongozi na wanasiasa wawaachie watalamu wafanye kazi kisayansi.

Kukabiliana na tatizo la Covid19 hakuhitaji ushauri wa mtu mmoja, utaalamu wa aina moja au mkakati wa wizara moja. Kunahitaji wataalamu wa afya ya jamii (public health experts); wataalamu wa tabia na kuenea kwa magonjwa (epidemiologists); watabibu (Medical doctors); wafamasia; wachumi; wataalamu wa takwimu; wataalamu wa mifumo ya kompyuta; wataalamu wa mathematical modelling; wanasaikolijia, wanasosholojia, nk.

Wote hawa wanatakiwa wakae chini wakiwa na taarifa/data sahihi na kudadavua kila hatua ya maambukizi kushauri maamuzi sahihi ya kuchukua. Kutanguliza hofu/panic, na kuchukua hatua za saa za majeruhi kwa haraka, kunaweza kusisaidie kitu na ikaongeza madhara ya tatizo.

Viongozi wetu na wanasiasa wawape wataalamu uhuru wa kutosha kuchambua hali na kuongozwa na sayansi katika kutoka ushauri. Pia, tuanze kufanya maandalizi ya rasilimali kuhakikisha tunaweza kupunguza athari ya tatizo iwapo litajitokeza.

Mwisho, tumeona dunia nzima watu wanashauriwa kunawa mikono kwa maji na sabuni kama njia kuu ya kuepuka maambukizi ya Covid19.

Kwamba vitu hivi vya kawaida kabisa ndio tiba ya tatizo linaloitingisha dunia. Hivyo basi, ni wakati muafaka serikali kuongeza bidii kuhakikisha huduma hii ya msingi (upatikanaji wa maji safi na salama) inamfikia kila mwananchi mjini na kijijini.

Kwa kuanzia, kila eneo la huduma za jamii (mashule, vyuo, hospitali, stendi za mabasi, viwanja vya ndege, maeneo ya michezo, nyumba za ibada, na kwingine kunakoweza kukusanya watu wengi) linakua na huduma ya uhakika ya maji safi na salama.

Nani ajuaye baada ya Covid19 kutakua na kirusi gani kingine ambacho labda kinachokimbizwa kwa kuna uso na miguu kwa maji tu?

Iwapo nasi tukatembelewa na Covid19, itakuaje pale ambapo wataalamu na viongozi wetu watasisitiza na kutushauri kunawa mikono huku wakijua hakuna huduma ya maji inayokidhi mahitaji hayo?

Nyongeza kutokana na maswali na mrejesho kwenye uchambuzi huu.

16/03/2020

Moja:
tatizo kubwa linalokumba mlipuko wa Covid19 ni kusambazwa kwa taarifa zisizo sahihi na watu wasio na utaalamu kuwa na nguvu kubwa ya kutoa maoni na kulazimisha au kushawishi hatua za kuchukua (misinformation). Covid19 imekua na waongeaji na wachambuzi wengi (pundits) kuliko wataalamu wa afya na magonjwa, na hii imekua tatizo juu ya tatizo. Tunapojadili mlipuko wa Covid19 na hatau za kuchukua, ni vema tujikumbushe kwamba swala la maambuziki, kusambaa, na kudhibiti magonjwa ya mlipuko ni sayansi tena ngumu. Hili sio swala la hisia, siasa wala “logic” yangu inanielekeza nini.

Mbili: Unaposoma ushauri unaogusia sayansi, ni vema kuangalia “key words” ili kupata tafsiri ndani ya muktadha wa kilichoandikwa. Kuna maneno matatu ya kuzingatia unaposoma nilichoandika: “PANDEMIC” (mlipuko uliofikia ngazi inayohesabiwa nchi zote duniani haziko salama); MUDA wa kufanya maamuzi; na TIJA ya hatua zinazochukuliwa. Katika mjadala wangu, sijasema kwamba maamuzi waliyofanya Kenya hayafai kwenye mlipuko, bali nimesema hayakustahili kwa ngazi/hatua/ ukubwa wa MLIPUKO kwa SASA na hayana SAPOTI ya kutosha ya KISAYANSI. Nimejadili umuhim wa kuchukua HATUA kulingana na MUDA wa mlipuko; UKUBWA wake; na aina ya MADHARA huku ukizingatia HALI YA MAISHA YA WATU; MIUNDOMBINU; UCHUMI; uwezo wa MFUMO WA AFYA; na madhara ya MUDA MFUPI na MUDA MREFU ya maamuzi yanayochukuliwa.

Kwa kusisitiza tu, ungonjwa ukishatangazwa kama PANDEMIC, maana yake ni kwamba hauna mipaka tena na hakuna nchi duniani inaweza kujitenga au kuchukua hatua zake binafsi kukabiliana nao. Narudia tena, kufunga mipaka na taasisi za elimu mapema kama walivyofanya Kenya, sio moja ya njia zitakazohakikisha kuna TIJA katika kuzuia maambuziki. Nchi zote mulizotaja ambazo zimefunga mipaka (kutoa USA) zimefanya hivyo baada ya maambukizi kufikia kiwango ambacho udhibiti unakua mgumu na mfumo wa afya unalemewa. USA wamefunga mipaka mapema lakini ushahidi unaonesha hakuna TIJA yoyote ya maana kwani tatizo limeendea kukua tena kwa kasi. Kwenye PANDEMIC dhana ya kukimbilia kufunga mipaka inaweza kuwa na maana tu kama itatumika na nchi ambazo bado hazina maambukizi kama njia ya kuchelewesha tatizo (delay strategy) kuruhusu nchi kujipanga kukabiliana nayo (sio kuepuka). Hiki ndicho tulitegemea USA wafanye lakini tumeona kwamba hawakua wamejipanga hata kuwa na vifaa vya kupimia na hadi leo wameweza kupima watu elfu 15 pekee.

Tatu, hoja za kusema kwamba Covid19 ni hatari sana na kwamba kuchukua hatua kali (drastic/ draconian measures) mapema kama Kenya ni sawa, nao ni upotoshaji na misinformation. Ni kusababisha panic isiyo na ulazima. Kinacholeta hofu kuu kwenye Covid19 ni kwa sababu ni tatizo jipya na hivyo hatuna kinga wala tiba. Labda nitumie data kidogo kufafanua hili kwa kulinganisha hatari ya Covid19 na binamu zake ambao tayari tunao siku nyingi.
  • Kutokana na taarifa zilizoko kwenye kanzidata mbalimbali za dunia kama vile Worldometer na Statista, tangu Covid19 igundulike mwezi Dec wagonjwa waliothibitishwa hadi ninapoandika hapa ni kama 171,000. Kati yao vifo ni 6,530 na watu waliogua na kupona ni 77,800.
  • Watu wanaokufa kwa mafua Ulaya pekee kwa mwaka (msimu wa baridi) ni takrabani 40,000 na hii ni pamoja na kutoa chanjo kwa watoto na wazee kila msimu wa baridi unapoanza.
  • Kulingana na kitengo cha kuzuia magonja USA cha CDC, tangu msimu wa baridi ulipoanza mwezi October 2019 hadi sasa, kwa USA pekee watu waliugua mafua ni zaidi ya milioni 36. Kati yao zaidi ya 370,000 walilazwa hospital na yamesababisha vifo zaidi 22,000.
  • Mlipuko wa kipindupindu tuliopata hapa Tanzania kuanzia mwezi wa 8 mwaka 2015 na ukaendelea taratibu hadi 2017, waliugua watu zaidi ya 25,000 na kusababisha vifo zaidi ya 500. Kulingana na repoti ya malaria ya WHO mwaka 2019, jumla ya watu milioni 228 waliugua malaria duniani mwaka 2018 na kati yao 405,000 walifariki.
Ukweli ni kwamba Covid19 haifikii uhatari wa magonjwa ambayo tayari tunayo. Tena yenyewe ina unafuu sana maana mtu akipata Covid19 na hana matatizo mengine ya kiafya, uwezekano wa kupona ni zaidi ya 92% (kwa data zilizoko) tena wengi ikiwa ni bila hata ya kutibiwa. Una hakika ya kupona na virusi kutoweka ndani ya siku 7 hadi 14 pekee (tazama kielelezo kwa data za hadi jioni hii kwa nchi zote).
1584401899687.png

Ukiumwa kipindupindu au malaria, kwanza unateseka sana na usipotibiwa ndani ya siku chache kifo hakiepukiki. Hivyo tupambane na Covid19 kisayansi na kwa ushauri wa wataalamu na sio kwa hisia na maoni ya kusema nchi hii au ile imefanya nini. Nchi nyingi duniani (hasa tajiri) zimepanic kwa kukosa maandalizi ya tatizo kama hili na maamuzi ya kisiasa. Hivyo hatua walizochukua wao sio standard na ndio mana hadi leo Ulaya wanaibwekea USA kwa kuwafungia mipaka. Unapoamua kufungia watu ndani kwa haraka kwenye nchi maskini kama za Kiafrika, unaweza ndio kuzua uharaka wa maambukizi lakini hauzuii ungonjwa kuwepo na unaweza kuwaua watu kwa sababu nyingine zitokanazo na umaskini; magonjwa ambayo tayari tunayo; na kukosekana miundombinu wezeshi. Hatua kali zichukuliwe pale tu hali inapoonesha ni mbaya na mfumo wetu wa afya hauna uwezo wa kukabiliana nayo tena. Huwezi kuchukua hatua kwa kigezo cha kulinda maisha dhidi ya Covid19 halafu wakafa na matatizo mengine.

Kitu kingine ambacho hakijulikani na watu wengi ni kwamba sisi tuna mfumo imara sana chini ya wizara ya Afya wa kupambana na magonjwa ya kuambukiza na kukabiliana na milipuko unaoratibiwa na miongozi ya mkakati uitwao Integrated Diseases Surveillance and Response (IDSR) strategy. Mfumo huu unafanya kazi kubwa kila siku kuratibu magonjwa ya milipuko nchi nzima na namna ya kuyadhibiti. Ukisoma taarifa za kila wiki wanazochapisha utashangaa kazi wanayofanya. Yes, mfumo huu bado una mapungufu kadhaa lakini umekua msaada mkubwa sana. Hivyo usishangae sisi tukawa na uwezo wa kudhibiti Covid19 kirahisi kuliko nchi matajiri ambao mifumo yao ya afya haijazoea kupambana na magonjwa ya maambukizi.

Imeandikwa na Mathew Mndeme ((mmtogolani@gmail.com) )
Mtafiti katika mifumo ya digitali kwenye ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza
 
Safi Mndeme kwa uchambuzi murua,hata Mimi maamuma nilitafakari Hilo kuhusu Kenya . Hata hivyo niliwaza yafuatayo;​
  • Pengine Kenya tatizo Ni kubwa zaidi kuliko wanavyotangaza...sisi wengine huwa tuna ugonjwa wa ku 'politisize ' Kila kitu ,hata tukiona mlevi anapepesuka na kuongea hivyo mitaani ,tunaweza Siasa!
  • ..au labda Kenya wapo vizuri ktk kukiandaa kukabiliana na majanga!
  • Na kwa muktadha huu Tz Ni Kama... tunachelewa kuchukua hatua madhubuti stahili. Na kwa kuwa siku hizi maamuzi yanategemea majiniazi wachache Kama SI mmoja....😘😘😘
  • All in all,huu ugonjwa Ni Balaa na Mungu aturehemu!
 
China walifunga viwanda,itali wamezuia mechi zote,hawa uliondika unatueleza mawazo yako,mawazo Hayapigwi rungu
 
Kenya wapo sahihi kabisa hii ni kutokana na aina ya ugonjwa wenyewe

Maisha ya raia hayanunuliwi nibora kulinda raia kwa ghalama yoyote ile tahadhali ni bora kuliko kinga,sisi nchi masikini tuzidi kuomba Mungu kama marekani, Italy,uingereza china corona inawatoa jasho mpaka viongozi wanapata angalia canada je sisi

Tazama mashule yetu tazama usafiri wa umma kama daladala, masokoni miskitini na makanisani

Wenzetu wanaweza kujinunulia chakula hata kwa mda mlefu supermaket wakaweka ndan sisi maskini vijijini mijini njaa atakacho pata anaenda kununua sokoni kwetu tusipo chukua hatua za kujihami mapema ni hatari zaidi na zaidi ..

Kenya ni kama wazingu ama kama ulaya ya East Africa yaan the way wanavyo ratibu mambo yao wako very smart
 
Mim naungana na kenyata kwa 100%,,,kwa jinsi ugonjwa unavosambaa ni bora sana angalau kwa muda kiasi kutaka kujua real situation na kizuia kuambukiza zaidi...Rwanda wamefanya the same...hakuna namna kiukweli maana akipatikana mmoja possibility wako wengi due to contact...nashauri hayohayo kwa nchi yetu ikithibitisha hata mmoja tu
 
Huu ndo ushauri mzuri siyo ule wa Mwanakijiji anayetaka tutangaze Martial laws bila kujiuliza hali ya kiuchumi ya wananchi wetu kuhimili hiyo martial law ikoje kwa sasa. Anataka watu wafe kwa njaa?

Kimsingi nakubaliana na mengi uliyoandika lakini napingana na wewe unaposema kuwa kirusi kikiishaingia nchini mwako then kufunga mipaka na kuzuia wageni hakuna tija. Hilo mimi naona si sahihi kwa sababu hawa wageni wanaoingia iwapo wanakuja na virusi basi wanaongeza kasi ya maambukizi. Ni bora uwazuie ili upambane na waliomo ndani. Usipowazuia maana yake ni sawa na kuziba matundu ya mtumbwi huku ukiruhusu uendelee kutobolewa pengine
 
Kenyatta yupo sahihi Sana Tena ningekuwa mm magufuli mipaka ningekuwa nishafunga hahaha eti tusubiri mlipuko ufike kileleni hivi mnadhani Corona ni mzaamzaa.....kwa gharama yoyote uhai wa raia ulindwe. Kenyatta kafanya maamuzi sahihi kwa muda muafaka itasaidia sanaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana Mkuu Mwalimu MM kwa
taarifa hii ni muhimu, itumwe kwa Waziri Ummie Mwalimu, PM Majaaliwa na kwa No. 1 mwenyewe Mzee Baba!.

P
Corona sio mzaamzaa, Kenyatta kafanya maamuzi sahihi kabisa hata magufuli sahivi ashauriwe kujiandaa kufanya strong protective decisions hii ya kusalimiana kwa miguu mara sijui nn it's not necessary kwa Sasa..mm nadhani kwa Sasa tupambane mipakani uko ili kutoruhusu kabisa ichi kirusi kuingia .it's a serious mess mwalimu MM Corona sio theory uliosoma darasani wen comes to protect the citizens

Nashukuru kwa maoni, maswali, nyongeza na kukosoa. Naomba nijaribu kujibu hoja chache zilizoibuka hapa kwa pamoja.

Moja: tatizo kubwa linalokumba mlipuko wa Covid19 ni kusambazwa kwa taarifa zisizo sahihi na watu wasio na utaalamu kuwa na nguvu kubwa ya kutoa maoni na kulazimisha au kushawishi hatua za kuchukua (misinformation). Covid19 imekua na waongeaji na wachambuzi wengi (pundits) kuliko wataalamu wa afya na magonjwa, na hii imekua tatizo juu ya tatizo. Tunapojadili mlipuko wa Covid19 na hatau za kuchukua, ni vema tujikumbushe kwamba swala la maambuziki, kusambaa, na kudhibiti magonjwa ya mlipuko ni sayansi tena ngumu. Hili sio swala la hisia, siasa wala “logic” yangu inanielekeza nini.

Mbili: Unaposoma ushauri unaogusia sayansi, ni vema kuangalia “key words” ili kupata tafsiri ndani ya muktadha wa kilichoandikwa. Kuna maneno matatu ya kuzingatia unaposoma nilichoandika: “PANDEMIC” (mlipuko uliofikia ngazi inayohesabiwa nchi zote duniani haziko salama); MUDA wa kufanya maamuzi; na TIJA ya hatua zinazochukuliwa. Katika mjadala wangu, sijasema kwamba maamuzi waliyofanya Kenya hayafai kwenye mlipuko, bali nimesema hayakustahili kwa ngazi/hatua/ ukubwa wa MLIPUKO kwa SASA na hayana SAPOTI ya kutosha ya KISAYANSI. Nimejadili umuhim wa kuchukua HATUA kulingana na MUDA wa mlipuko; UKUBWA wake; na aina ya MADHARA huku ukizingatia HALI YA MAISHA YA WATU; MIUNDOMBINU; UCHUMI; uwezo wa MFUMO WA AFYA; na madhara ya MUDA MFUPI na MUDA MREFU ya maamuzi yanayochukuliwa.

Kwa kusisitiza tu, ungonjwa ukishatangazwa kama PANDEMIC, maana yake ni kwamba hauna mipaka tena na hakuna nchi duniani inaweza kujitenga au kuchukua hatua zake binafsi kukabiliana nao. Narudia tena, kufunga mipaka na taasisi za elimu mapema kama walivyofanya Kenya, sio moja ya njia zitakazohakikisha kuna TIJA katika kuzuia maambuziki. Nchi zote mulizotaja ambazo zimefunga mipaka (kutoa USA) zimefanya hivyo baada ya maambukizi kufikia kiwango ambacho udhibiti unakua mgumu na mfumo wa afya unalemewa. USA wamefunga mipaka mapema lakini ushahidi unaonesha hakuna TIJA yoyote ya maana kwani tatizo limeendea kukua tena kwa kasi. Kwenye PANDEMIC dhana ya kukimbilia kufunga mipaka inaweza kuwa na maana tu kama itatumika na nchi ambazo bado hazina maambukizi kama njia ya kuchelewesha tatizo (delay strategy) kuruhusu nchi kujipanga kukabiliana nayo (sio kuepuka). Hiki ndicho tulitegemea USA wafanye lakini tumeona kwamba hawakua wamejipanga hata kuwa na vifaa vya kupimia na hadi leo wameweza kupima watu elfu 15 pekee.

Tatu, hoja za kusema kwamba Covid19 ni hatari sana na kwamba kuchukua hatua kali (drastic/ draconian measures) mapema kama Kenya ni sawa, nao ni upotoshaji na misinformation. Ni kusababisha panic isiyo na ulazima. Kinacholeta hofu kuu kwenye Covid19 ni kwa sababu ni tatizo jipya na hivyo hatuna kinga wala tiba. Labda nitumie data kidogo kufafanua hili kwa kulinganisha hatari ya Covid19 na binamu zake ambao tayari tunao siku nyingi.
  • Kutokana na taarifa zilizoko kwenye kanzidata mbalimbali za dunia kama vile Worldometer na Statista, tangu Covid19 igundulike mwezi Dec wagonjwa waliothibitishwa hadi ninapoandika hapa ni kama 171,000. Kati yao vifo ni 6,530 na watu waliogua na kupona ni 77,800.
  • Watu wanaokufa kwa mafua Ulaya pekee kwa mwaka (msimu wa baridi) ni takrabani 40,000 na hii ni pamoja na kutoa chanjo kwa watoto na wazee kila msimu wa baridi unapoanza.
  • Kulingana na kitengo cha kuzuia magonja USA cha CDC, tangu msimu wa baridi ulipoanza mwezi October 2019 hadi sasa, kwa USA pekee watu waliugua mafua ni zaidi ya milioni 36. Kati yao zaidi ya 370,000 walilazwa hospital na yamesababisha vifo zaidi 22,000.
  • Mlipuko wa kipindupindu tuliopata hapa Tanzania kuanzia mwezi wa 8 mwaka 2015 na ukaendelea taratibu hadi 2017, waliugua watu zaidi ya 25,000 na kusababisha vifo zaidi ya 500. Kulingana na repoti ya malaria ya WHO mwaka 2019, jumla ya watu milioni 228 waliugua malaria duniani mwaka 2018 na kati yao 405,000 walifariki.
Ukweli ni kwamba Covid19 haifikii uhatari wa magonjwa ambayo tayari tunayo. Tena yenyewe ina unafuu sana maana mtu akipata Covid19 na hana matatizo mengine ya kiafya, uwezekano wa kupona ni zaidi ya 70% (kwa data zilizoko) tena bila hata ya kutibiwa na una hakika ya kupona na virusi kutoweka ndani ya siku 7 hadi 14 pekee. Ukiumwa kipindupindu au malaria, kwanza unateseka sana na usipotibiwa ndani ya siku chache kifo hakiepukiki.

Tupambane na Covid19 kisayansi na kwa ushauri wa wataalamu na sio kwa hisia na maoni ya kusema nchi hii au ile imefanya nini. Nchi nyingi duniani (hasa tajiri) zimepanic kwa kukosa maandalizi ya tatizo kama hili na maamuzi ya kisiasa. Hivyo hatua walizochukua wao sio standard na ndio mana hadi leo Ulaya wanaibwekea USA kwa kuwafungia mipaka. Unapoamua kufungia watu ndani kwa haraka kwenye nchi maskini kama za Kiafrika, unaweza ndio kuzua uharaka wa maambukizi lakini hauzuii ungonjwa kuwepo na unaweza kuwaua watu kwa sababu nyingine zitokanazo na umaskini; magonjwa ambayo tayari tunayo; na kukosekana miundombinu wezeshi. Hatua kali zichukuliwe pale tu hali inapoonesha ni mbaya na mfumo wetu wa afya hauna uwezo wa kukabiliana nayo tena. Huwezi kuchukua hatua kwa kigezo cha kulinda maisha dhidi ya Covid19 halafu wakafa na matatizo mengine.

Kitu kingine ambacho hakijulikani na watu wengi ni kwamba sisi tuna mfumo imara sana chini ya wizara ya Afya wa kupambana na magonjwa ya kuambukiza na kukabiliana na milipuko unaoratibiwa na miongozi ya mkakati uitwao Integrated Diseases Surveillance and Response (IDSR) strategy. Mfumo huu unafanya kazi kubwa kila siku kuratibu magonjwa ya milipuko nchi nzima na namna ya kuyadhibiti. Ukisoma taarifa za kila wiki wanazochapisha utashangaa kazi wanayofanya. Yes, mfumo huu bado una mapungufu kadhaa lakini umekua msaada mkubwa sana. Hivyo usishangae sisi tukawa na uwezo wa kudhibiti Covid19 kirahisi kuliko nchi matajiri ambao mifumo yao ya afya haijazoea kupambana na magonjwa ya maambukizi.

MM Togolani
 
Kenya wamethibitisha uwepo wa watu 3 wenye Covid19 na tayari leo Rais Kenyatta katangaza kufungwa kwa shule na taasisi zote za elimu nchini kuanzia kesho.

Pia amefunga mipaka yake kwa raia wa nchi yoyote ambayo imeshatangaza kuwa na mlipuko wa Covid19 ndani ya siku mbili zijazo. Kama vile haitoshi, kawataka waajiri wawaruhusu wafanyakazi wao wafanye kazi wakiwa majumbani na watu wapunguze usafiri wa umma kama sio lazima.

Katika hatua nyingine, kashauri manunuzi na malipo yafanyike zaidi kwa njia za kielekroniki (simu na kadi za benki) ili kuzuia maambukizi kwa kushika fedha.

Kwa kuwa tatizo la Covid19 bado linaendelea na kwenye nchi zetu za Afrika ndio kwanza linabisha hodi, nadhani ni muhimu kujiuliza faida na hasara ya uamuzi waliochukua Kenya maana ni wazi uamuzi wao utaigwa na nchi nyingine nyinge za Afrika.

Maamuzi ya hatua za kuchukua kwenye mlipuko
Kwenye kupambana na magonjwa ya kuambukiza ya mlipuko kama Covid19, kuna mambo mengi ya kutazama katika kuchukua hatua za kukabiliana na tatizo.

Kila hatua ya mlipuko inahitaji kutazamwa vema kujua ni njia gani inafaa kwa hatua husika. Kuzuia mikusanyiko na kufunga mipaka ni hatua kali na za ngazi ya juu sana.

Zinapatikana pale tu mlipuko unapokua umesambaa sana na madhara yake yamekua makubwa. Katika kufikia maamuzi ya hatua za kuchukua kuna maswali kadhaa ya kujiuliza.
  • Hali ya mlipuko ikoje?
  • Uwezo wa mfumo wa kutoa huduma za afya kukabiliana na mlipuko ukoje?
  • Tunataka kudhibiti nini na kwa kiasi gani?
  • Je, mlipuko umefikia kiwango gani cha maambukizi?
  • Tunategemea kilele cha maambukizi kitafika baada ya muda gani?
  • Tunakadiria kutakua na wagonjwa wangapi mlipuko utakapofikia kileleni na Tunakadiria vifo vingapi?
  • Ni kundi gani kwenye jamii liko kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa na/au kuathirika na maambukizo?
  • Mfumo wa kinga kwa ugonjwa husika ukoje?
  • Hatua tunazochukua zitakua na athari gani kwenye maisha ya mtu mmoja mmoja, familia, jamii, na uchumi wa nchi kwa muda mfupi na muda mrefu?
  • Hali ya wananchi wetu ikoje kwa muktadha wa mlipuko husika (kielimu, kiuchumi, nk)?
Kenya wanasema watu 2 wenye maambukizi wanahusina au walisafiri na mgonjwa wa kwanza ambaye aliingia na Covid19 akitokea Marekani kupitia Uingereza ambako tayari tatizo ni kubwa.

Wagonjwa wote hawa wamegundulika ndani ya siku tu 4 zilizopita. Kwa ugonjwa unaoambukiza kwa haraka kama Covid19, hii ni hatua ya mwanzo kabisa ya mlipuko katika nchi.

Ndio kwanza virusi vimeanza kuweka makazi ndani ya Kenya vinatazama vikatize mitaa gani. Katika hatua hii, kwa kuanzia, serikali ilitakiwa kuchukua hatua kama nne za msingi.
  • Kujikita zaidi katika kutoa elimu kwa jamii kulielewa tatizo kwa undani, ukubwa wake, na namna ya kujikinga kwa mtu mmojammoja na kama jamii.
  • Kuanza kufanya maandalizi ya kutosha (kwa maana ya vifaa, wataalamu, fedha, nk) kuwezesha hospitali na mifumo mingine ya utoaji huduma za afya kuwa tayari kukabiliana na mlipuko unapoelekea kwenye kilele (watu wengi kuugua na/au kufariki kwa wakti mmoja).
  • Kufuatilia kwa karibu mnyororo wa maambukizi na kujaribu kudhibiti kuenea zaidi kutoka kwa wale ambao wameshaupata.
  • Kuwaandaa wataalamu wa magonjwa ya mlipuko na wanasayansi wengine ili wafuatilie kwa karibu hali ya mlipuko kila siku na kushauri nini cha kufanya kulingana na ushihidi wa kisayansi.
Tatizo la maamuzi Kenya liko wapi?
Ni kwa bahati mbaya kwamba wataalamu wa Kenya na viongozi wameona waanze na kuzuia mikusanyiko. Kikubwa kitakacholetwa na maamuzi haya ni hofu na mshtuko, kwani kwa mwananchi wa kawaida, yanaashiria kwamba hali ni mbaya kupindukia.

Hali kadhalika, kwa maamuzi haya, ni vigumu kujua hali ya mlipuko itakavyokua, utaenea wapi zaidi, utawapata kina nani zaidi, na madhara yatakua kwa kundi gani na kwa ukubwa gani.

Hii ni hatua ambayo mchango wa watafiti wa sayansi na watu wenye tafakuri tunduizi na pana ya hali ya nchi, wangetakiwa kupewa nafasi zaidi ili kila uamuzi unaochukuliwa na serikali kukabiliana na hali uwe una ushahidi wa kisayansi na matokeo yake kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutabirika.

Pia, serikali ya Kenya imechukua hatua nyingi kwa wakati mmoja jambo litakaloleta ugumu sana kujua ni hatua ipi kati ya hizo inafanya kazi namatokeo yake yanaonesha kuna tija.

Katika kukabiliana na hali ya hatari, ni vema kutumia mbinu za kijeshi zaidi (military strategies) ambapo unakua na mkakati mkuu unaotumia kukabiliana na adui halafu unatazama nini cha kufanya iwapo mkakati mkuu hautafanya kazi (worse case scenario).

Kwa sasa, iwapo maamuzi waliyochukua yatafanya kazi au vinginevyo, itakua ngumu sana kujua ni njia gani imekua na tija au ni ya ovyo.

Ushahidi wa kisayansi unasemaje. Moja, hauoneshi kwamba kukimbilia kuzuia mikusanyiko ya watu kunasaidia kupunguza tatizo kwa haraka.

Mbili, ushahidi ulioko hadi sasa kuhusu maambukizi ya Covid19, unaonesha watoto sio waathirika wakubwa unapolinganisha na watu wazima.

Haijajulikana kama wana kinga zaidi au ni mazingira gani lakini wanaoathirika hadi sasa ni wachache sana kote ugonjwa ulipogundulika.

Hivyo kufunga shule za msingi na sekondari kunaweza kuwa na matokeo finyu sana ya kupunguza maambukizi hasa katika hatua hii.

Tatu, ugonjwa ukishatangazwa kwamba ni janga la kimataifa (pandemic) na uko ndani ya nchi yako, hakuna ushahidi wa kutosha kisayansi unaonesha kwamba kufunga mipaka kunasidia kupunguza madhara.

Nne, unapoamua kuchukua hatua kama vile watu wasikusanyike, wanafunzi wasiende shule, usafiri wa umma kusimamishwa, kuzuia ndege zinazongia, na kufunga mipaka; ni lazima pia uwaze hali ya maisha ya wananchi itakuwaje na iwapo madhara yatakua makubwa kuliko yale ya kukabiliana na mlipuko. Kwa mfano:
  • Nani atakaa na watoto wadogo wasiokwenda shule kwa muda usiojulikana wakati wazazi wanatakiwa kwenda kazini?
  • Je, watu wakiacha kwenda kazini mapema hivi, waajiri bado watakua na uwezo wa kuwalipa mishahara wakati hawafanyi kazi?
  • Kenyetta amewaambia waajiri wawaruhusu watumishi wao wafanyie kazi nyumbani. Lakini je, hali ya kazi na maisha ya Kenya yanaruhusu kwa kiasi gani kufanya kazi kutokea nyumbani? Maagizo haya nayaona kama ni ya kuiga kwa wanachoshauri nchi za magharibi. Kule, internet ni moja ya mahitaji muhim nyumbani kama vile bomba la maji au umeme na siyo ya kupima kama vifurushi vya tigo; na kompyuta sio kifaa kigeni kwenye familia. Tujiulize, Kenya ina wafanyakazi wangapi wenye uwezo wa kuwa na internet ya kutosha nyumbani na wanamiliki kompyuta binafsi kuwawezesha kufanya kazi nyumbani? Aina ya kazi zilizoajiri watu wengi, zinaweza kufanyika nje ya maeneo ya kazi?
  • Gharama ya kukatisha utoaji wa elimu kwenye ngazi zote kwa muda usiojulikana, utaathiri vipi taifa?
  • Wakenya wangapi wana maji safi ya bomba nyumbani na sabuni kuwawezesha kunawa mikono kila mara kama inavyoshauriwa?
  • Je, Kenya ina mfumo unaotambua kila mwananchi na anapoishi, achilia mbali makundi hatarishi kwa ugonjwa huu kama wazee?
Changamoto ya mlipuko wenyewe
Jambo lingine la kutazama ni maambukizi munayotaka kuyakabili. Kuwaambia watu wakae nyumbani kuna uwezekano mkubwa wa kuzuia maambuzi kwa kasi lakini ukasababisha tatizo lingine.

Bado wanasayansi hawana uelewa wa kutosha kuhusu Covid19. Kwa mfano, bado haijuilikani ni kwa kiasi gani kila anayeumwa anaweza kutengeneza kinga kama ambavyo imezoeleka kwa magonja mengine ya virusi.

Bado hatujui iwapo kinga inayojengeka kwa ambaye ameshaumwa itamkinga asoiugue tena ndani muda gani. Bado hatujui vya kutosha iwapo aliyepata virusi na akapona hatarudiwa ndani ya muda mfupi.

Hivyo, watu wakianza kujifungia mapema kuna uwezekano mkubwa mukashindwa kupata uelewa wa kutosha kuhusu maambukizi yanavyoenea, athari zake, na hatua za kuchukua.

Pia, virusi vinaweza kuchukua likizo (incubation) vikapumzika tu huku mukidhani mumedhibiti mlipuko. Ila watu watakapoanza kutoka na kuchangamana tena, tatizo likaanza upya kwa kua kuna wengi wasio na kinga.

Maisha ya virusi, wanavyosambaa, na mwitikio wa mwili wanapotushambukia, ni moja ya sayansi ngumu sana kuitabiri. Virusi wengi wana tabia ya kubadilika pamoja na athari wanazosababisha.

Kwa magonjwa ambayo tumeweza kutengenza kinga kama Surua, polio, na mengine, watu wanapewa chanjo ambayo inawasaidia kutengenza kinga kwa muda mrefu.

Utoaji wa chanjo hii hutengeneza kitu kinaitwa kitaalamu kama “kinga ya kijamii” (Herd/ community immunity). Kinachotokea sio kwamba virusi, kwa mfano vya surua, wametoweka Tanzania, bali ungojwa hauonekani kwa sababu watu wengi kwenye jamii wana kinga dhidi ya virusi hivyo kupitia chanjo.

Hivyo kunapotekea mlipuko (mtu au watu wasio na kinga kupata Surua) ugonjwa unashindwa kusambaa kwa sababu watu wengi wanaokutwa na kirusi wanakua na kinga.

Hivyo nao wanawakinga hata wale ambao hawana kinga maana ugonjwa hautawafikia.

Kwa mfano, nchi kama Marekani na Uingereza kuna watu wengi hawataki watoto wao wapate chanjo kwa madai kwamba chanjo zina madhara kiafya au wana imani kwamba kuna hujuma inafanywa kupitia chanjo.

Hivyo kuna maelfu ya watoto hawajapata chanjo. Ndio maana pamoja na kwamba nchi yetu tumetokomeza kabisa Surau, mwaka jana Surua iliathiri watu wengi Marekani na mwaka juzi ilikuwepo baadhi ya maeneo Uingereza.

Kwa nini walipata pamoja na maendeleo yao? Bado virusi vya surua vipo. Ila kinachowakinga wale ambao hawajachanjwa, ni uwepo wa watu wengi wenye kinga (herd/community immunity). Lakini ikatokea kirusi kikakutana na mtoto ambaye hana chanjo, atapata ugonjwa na ataambukiza wengine wa aina yake huko shuleni.

Sasa kwa habari ya Covid19, bado haina kinga na itachukua muda mrefu kinga kupatikana. Kinga pekee ambayo tunaweza kuipata kwa sasa itakayosaidia watu wengi, ni kinga ya kijamii.

Na kinga hii itapatikana pale tu ambapo watu wengi watapata maambukizi na kupona. Hawa wakishapona, wanatengeneza kinga ambayo itasaidia kuukata mnyororo wa maambukizi na hivyo kuwakinga hata wale ambao bado hawana kinga.

Tukumbuke pia kwamba sio kila mtu ana uwezo wa kutengeneza kinga anapopata maambukizi. Hii inatokana na sababu za kiafya, umri, na hata sababu za kibayolojia za mwili zinazoweza kumfanya kuwa na uwezo mdogo wa kutengeneza kinga.

Ndio maana watu wengi waliofariki kwa Covid19 hadi sasa ni wazee ambao kinga yao ni ndogo au ambao tayari walikua na magonjwa mengine yanayodhoofisha uwezo wao wa kutengeneza kinga. Nihitimishe kwa kujaribu kujibu maswali niliyoanza nayo.

MOJA: Nini faida ya hatua walizochukua Kenya?
  • Iwapo hatua zilizochukuliwa zitafanikiwa, wanaweza kudhibiti maambukizi kutowapata watu wengi na kutosambaa sehemu kubwa ya nchi.
  • Mfumo wa utoaji huduma za afya unaweza kukabiliana na tatizo kirahisi zaidi maana hatua hizi zitachelewesha mlipuko kufikia kilele mapema au kikafika kikiwa na maambukizi kidogo.
MBILI: Nini hasara za maamuzi haya?
  • Ni mapema sana kuchukua hatua kubwa kama hizi kwa kiwango cha maambukizi waliyonayo sasa. Hii ni sawa na kuanza vita na adui mukitumia SMG na AK47 kisha siku ya pili wewe unaamua kuibuka na mabomu ya maangamizi huku ukiwa hata hujajua nguvu ya adui yako na uwezo wake.
  • Kenya watashindwa kupata ufahamu wa kutosha kuhusu tabia na mwelekeo (behaviour and pattern) wa maambukizi na madhara yake.
  • Kwa kukosa uelewa wa kutosha, hatua watakazochukua zinaweza zisiwe za wakati sahihi na tija inayotegemewa ikakosekana.
  • Kuna uwezekano mkubwa maambukizi yakachelewa kufikia kilele na na mlipuko kudumu kwa muda mrefu. Ili mlipuko udhibitiwe, ni lazima ufikie kilele cha maambukizi kwanza na kikifika kwa haraka ni nafuu zaidi kwani tatizo litakwisha ndani ya muda mfupi. Unapochelewesha, hofu itaendelea kuwepo kwa muda mrefu na mikakati ya kukabili inaweza isiwe na tija.
  • Hali ya maisha ya wakenya wengi itaathirika sana na serikali haina uwezo wa kuwasaidia waathirika.
  • Hali ya uchumi inakwenda kutikisika vibaya sana kwani hakuna miundombinu ya kutosha na mbadala kuwezesha uzalishaji kuendelea watu wakikaa nyumbani.
  • Itachukua muda mrefu jamii ya wakenya kupata kinga ya Covid19 (herd/ community immunity) na huenda kukawa na hatari ya ugonjwa kujirudia kila baada ya muda fulani kutokana na tabia za kirusi ambazo bado hatujazielewa vya kutosha.
Nimalizie kwa kusema, hatua walizochukua Kenya zinaonekana ni za kisayansi lakini zimechukuliwa kwa msukumo na wakati usio sahihi. Inaonekana hofu/kuchanganyikiwa (panic) imekua kubwa; wanasiasa na washauri wao wamekua na haraka ya kuonesha wanafanya kazi; huenda wamesukumwa zaidi na maoni ya umma (public opinions) kuliko utaalamu/sayansi; baadhi ya hatua wameiga kwa nchi nyingine bila kuangalia hali halisi ya nchi yao.

Inawezekana pia, walichokifanya Kenya kinadhihirisha hali yetu waafrika ambapo mara nyingi tunafanya maamuzi bila kutazama mbali sana maana tunakua na haraka ya kutafuta suluhisho kwa matatizo ya leo kila iitwapo leo na ndio mana hatuifikii kesho tunayoitamani.

Ushauri
Ni ushauri wangu kwamba iwapo tatizo hili litaingia nchini kwetu (Mungu aepushe) viongozi na wanasiasa wawaachie watalamu wafanye kazi kisayansi.

Kukabiliana na tatizo la Covid19 hakuhitaji ushauri wa mtu mmoja, utaalamu wa aina moja au mkakati wa wizara moja. Kunahitaji wataalamu wa afya ya jamii (public health experts); wataalamu wa tabia na kuenea kwa magonjwa (epidemiologists); watabibu (Medical doctors); wafamasia; wachumi; wataalamu wa takwimu; wataalamu wa mifumo ya kompyuta; wataalamu wa mathematical modelling; wanasaikolijia, wanasosholojia, nk.

Wote hawa wanatakiwa wakae chini wakiwa na taarifa/data sahihi na kudadavua kila hatua ya maambukizi kushauri maamuzi sahihi ya kuchukua. Kutanguliza hofu/panic, na kuchukua hatua za saa za majeruhi kwa haraka, kunaweza kusisaidie kitu na ikaongeza madhara ya tatizo.

Viongozi wetu na wanasiasa wawape wataalamu uhuru wa kutosha kuchambua hali na kuongozwa na sayansi katika kutoka ushauri. Pia, tuanze kufanya maandalizi ya rasilimali kuhakikisha tunaweza kupunguza athari ya tatizo iwapo litajitokeza.

Mwisho, tumeona dunia nzima watu wanashauriwa kunawa mikono kwa maji na sabuni kama njia kuu ya kuepuka maambukizi ya Covid19.

Kwamba vitu hivi vya kawaida kabisa ndio tiba ya tatizo linaloitingisha dunia. Hivyo basi, ni wakati muafaka serikali kuongeza bidii kuhakikisha huduma hii ya msingi (upatikanaji wa maji safi na salama) inamfikia kila mwananchi mjini na kijijini.

Kwa kuanzia, kila eneo la huduma za jamii (mashule, vyuo, hospitali, stendi za mabasi, viwanja vya ndege, maeneo ya michezo, nyumba za ibada, na kwingine kunakoweza kukusanya watu wengi) linakua na huduma ya uhakika ya maji safi na salama.

Nani ajuaye baada ya Covid19 kutakua na kirusi gani kingine ambacho labda kinachokimbizwa kwa kuna uso na miguu kwa maji tu?

Iwapo nasi tukatembelewa na Covid19, itakuaje pale ambapo wataalamu na viongozi wetu watasisitiza na kutushauri kunawa mikono huku wakijua hakuna huduma ya maji inayokidhi mahitaji hayo?

Imeandikwa na Mathew Mndeme ((mmtogolani@gmail.com) )

Mtafiti katika mifumo ya digitali kwenye ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza
Aa so seessazx

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nimekuelewa sana katika kipindi cha awali kabisa cha maambukizi cha hususani watu wa 3 kwa measures walizoziweka kenya itakuwa ni ngumu mno kujua wanadhibiti kitu gani endapo maambukizi yatazidi kuenea sababu kila kitu wamekuzuia ile regulatory mechanism itakuwa ngumu mno.
 
Asante sana.

Baadae baada ya hili au kwa mkabala na hili la Corona, ndugu yangu Mndeme naomba kwa utaalamu wako ujaribu kutupitisha kidogo kwa baadhi ya pandemic zilizowahi kuvunja record ya dunia kwa kutufafanulia kitaalamu kama ufanyavyo hivi ili tupate ka mwangaza.

Mwisho
Makala kama hizi zinaamsha hisia za utafiti na pia zinatusaidia sisi viyoo vya jamii kupunguza mihemko isiyorasmi kwa wale wanaotutazama.
 
Back
Top Bottom