Ni kwa namna gani Maji husababisha Mlipuko wa Kipindupindu?

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Kwa Mujibu wa Mwongozo wa Kitaifa wa Kudhibiti Mlipuko wa Kipindupindu, Maeneo ambayo huonekana kushamiri maambukizi zaidi Nchini ni yale yasiyokuwa na maji ya kutosha ambayo ni safi na salama kwa ajili ya kunywa na matumizi mengine ya nyumbani

Upungufu wa Maji haya husababishwa na Mabomba yaliyotoboka kwa sababu ya uchakavu na hivyo kuwa rahisi kuingiza uchafu unaoweza kuwa na vimelea vya kipindupindu

Dalili Za Kipindupindu

Pia, imebainika kuwa watu wengi katika Maeneo yenye Kipindupindu hawana utamaduni wa kuchemsha au kuweka dawa ya kuua wadudu katika maji ya kunywa na ya matumizi mengine

Aidha, Maji machafu yatiririkayo kutoka Vyooni na Bafuni husababisha uchafuzi wa Mazingira hivyo kueneza vimelea vya Kipindupindu

Wataalamu wa Afya wamebainisha kuwa inachukua kati ya saa 12 hadi siku 5 kwa mtu kuonyesha dalili za Kipindupindu baada ya kula chakula au kunywa maji yenye vimelea vya Ugonjwa huo

Bakteria wanaosababisha Kipindupindu wanaweza kukaa mwilini hadi siku kadhaa baada ya kuambukizwa na hata wale ambao hawaoneshi dalili wanaweza kuambukiza ikiwa hawatachukua hatua za kulinda wengine ikiwemo kwenda Hospitali

Ifahamike kuwa inakadiriwa 10% ya Wagonjwa wa Kipindupindu ndio huonesha Dalili za Ugonjwa, hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari wakati wote kwani Watu wote (watoto kwa watu wazima) wanaweza kuambukizwa Kipindupindu

Njia zaKujikinga na Kipindupindu

Kufuatia Mlipuko wa Kipindupindu katika Mikoa ya Shinyanga, Ruvuma, Tabora, Simiyu, Mwanza na Kagera ni muhimu kukumbuka kuwa kwasababu Ugonjwa huu unahusishwa moja kwa moja na uchafu, uzingatiaji wa Usafi wa Mazingira wakati wote ni hatua ya kwanza ya kujikinga

Pia ni vyema mtu mmoja mmoja kuzingatia usafi binafsi kama Unywaji wa maji safi na salama, kunawa mikono mara kwa mara na kuepuka Vyakula vya Mtaani hasa wakati wa Mvua na wa Mlipuko

Muhimu; Japokuwa Kipindupindu huathiri watu wengi kwa wakati mmoja, kinaepukika kwa kuwahi Hospitali mara unapohisi dalili za kuharisha maji maji, kutapika na kusikia mlegevu

Chanzo: Mwongozo wa Kitaifa wa Kudhibiti Kipindupindu 1998
 
Kwa Mujibu wa Mwongozo wa Kitaifa wa Kudhibiti Mlipuko wa Kipindupindu, Maeneo ambayo huonekana kushamiri maambukizi zaidi Nchini ni yale yasiyokuwa na maji ya kutosha ambayo ni safi na salama kwa ajili ya kunywa na matumizi mengine ya nyumbani

Upungufu wa Maji haya husababishwa na Mabomba yaliyotoboka kwa sababu ya uchakavu na hivyo kuwa rahisi kuingiza uchafu unaoweza kuwa na vimelea vya kipindupindu

Pia, imebainika kuwa watu wengi katika Maeneo yenye Kipindupindu hawana utamaduni wa kuchemsha au kuweka dawa ya kuua wadudu katika maji ya kunywa na ya matumizi mengine

Aidha, Maji machafu yatiririkayo kutoka Vyooni na Bafuni husababisha uchafuzi wa Mazingira hivyo kueneza vimelea vya Kipindupindu

Chanzo: Mwongozo wa Kitaifa wa Kudhibiti Kipindupindu 1998
Harakati hizi jmn
 
Back
Top Bottom