Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,502
- 9,282
Mahakama ya rufani nchini Kenya jana imekataa jaribio la serikali la kufanya mabadiliko makubwa ya katiba katika uamuzi ambao ni pigo kwa rais Uhuru Kenyatta aliyeasisi mchakato huo wenye utata.
Jopo la Majaji saba limeunga mkono uamuzi wa awali uliotolewa na mahakama kuu ya nchi hiyo uliosema mapendekezo ya kubadili katiba ni kinyume na sheria na kwamba rais wa nchi hiyo hana mamlaka ya kuratibu mabadiliko ya katiba.
Rais Kenyatta ambaye amekuwa akishirikiana na kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga kupigia upatu mageuzi hayo alijenga hoja kuwa mabadiliko ya katiba chini ya mchakato wa maridhiano ya kisiasa maarufu BBI yatamaliza uhasama kwenye siasa za Kenya.
Uamuzi huo wa mahakama ya rufani unatarajiwa kubadili hali ya siasa za Kenya mwaka mmoja kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu.