Kenya: Mahakama ya Rufani yaweka zuio la Serikali kufanya mabadiliko ya Katiba

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,479
9,234
Mahakama ya rufani nchini Kenya jana imekataa jaribio la serikali la kufanya mabadiliko makubwa ya katiba katika uamuzi ambao ni pigo kwa rais Uhuru Kenyatta aliyeasisi mchakato huo wenye utata.

Jopo la Majaji saba limeunga mkono uamuzi wa awali uliotolewa na mahakama kuu ya nchi hiyo uliosema mapendekezo ya kubadili katiba ni kinyume na sheria na kwamba rais wa nchi hiyo hana mamlaka ya kuratibu mabadiliko ya katiba.

Rais Kenyatta ambaye amekuwa akishirikiana na kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga kupigia upatu mageuzi hayo alijenga hoja kuwa mabadiliko ya katiba chini ya mchakato wa maridhiano ya kisiasa maarufu BBI yatamaliza uhasama kwenye siasa za Kenya.

Uamuzi huo wa mahakama ya rufani unatarajiwa kubadili hali ya siasa za Kenya mwaka mmoja kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu.
 
Majaji wa Kenya wanapatikana baada ya kufanyiwa vetting kali, sio hakimu anaagizwa awafunge jela wapinzani eti ndio apewe ujaji na rais, never.

Pia katiba yao imeundwa kwa kuangalia maslahi mapana ya nchi na sio kulenga kubeba chama fulani kiendelee kutawala kwa ghiliba.

Ukitaka kuthibitisha utofauti wa judiciary ya Kenya na hii ya hapa kwetu, jaribu kusoma judgment ya mahakama za Kenya kisha usome za hapa halafu draw your conclusion.

Tanzania mahakama ni sehemu ya serikali na serikali inaingilia mahakama wakati wowote ikiona kuna haja kwao kufanya hivyo kitu ambacho Kenya hakipo kabisa kwani Kenya mbele ya sheria serikali na raia wa kawaida ngoma ni droo. Kwa hali hii tuliyonayo tuko nyuma ya Kenya kwa miaka 50.
 
Ruto kafurahi sababu alikuwa anapinga Ayo makubaliano Ruto anajiona kama raisi ajaye wa Kenya na saivi yeye na Kenyatta hawaivi ndyo maana
Lakini hawa si chama kimoja?
Na kabila pia si moja na itikadi si moja
Wakitofautiana wao wafuasi watakuweje?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom