Kelele Hoteli ya Bahari Beach

Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,205
1,459
Habari za jioni GT's

Naandika waraka huu nikiwa mkazi wa eneo la Bahari Beach kulalamikia kelele za kila weekend au za masherehe ktk Hotel hii.

Yaani kila week end kuna Ma disco toto nk. Ma DJ wanapiga wanapayuka na kupiga ma taarabu nk yaani ni vurugu tu. Kama ujuavyo upepo nao unabeba hizo sauti yaani utafikiria wote tuko kwenye hizo sherehe. Kila wanachoongea na miziki inayoimbwa inaimbia kwenye nyumba zetu.

Huyu MMILIKI wa hii hotel tumemwomba mara nyingi atuondolee kelele hizi hataki. Serikali tusaidieni jamani. Uhuru gani huu Kama sio kukomoana kwa raha za watu wengine??? Kama uko maeneo ya Bahari Beach hadi Kunduchi naona utakuwa umenielewa. Tuungane KUKATAA haya makelele. Mtu huwezi kupumzika jamani!!!!!

Wahusika tusaidieni.

Queen Esther
 
Last edited:
Makelele yaendelee hapa kazi tu!Si kuna sheria zinazokataza umeipigania hapa kazi tu!Haya endelea na makelele mbele kwa mbele mpaka ufe.
 
Kelele zinapeperushwa na upepo, sasa hao Ma DG wana uwezo wa kuzuia nguvu za upepo?
 
Mwasu sio nguvu ya upepo tu!!!

Kelele hizi zimezidi. Hakuna faragha huku yaani uswahilini ni afadhali!!! Ni mwendo wa Ma disco na ma taarabuu tuu!! Hii haikubaliki hata kidogo.

Watoto wetu wanasoma saa hizi na kumalizia home work. Kwa kelele hivi kwa kweli ni shida na haya ni makwazo ya MAKUSUDI.

Serikali tusaidieni. Hii ni Hotel ya kitalii Kama inavyojiita au ukumbi wa disco???? Basi waweke sound proof!!

Queen Esther

Kelele zinapeperushwa na upepo, sasa hao Ma DG wana uwezo wa kuzuia nguvu za upepo?
 
We Mdumah wewe!!!

Hii si ni Hotel ya ki MATAIFA?? Hayo Ma Disco na Ma Taarabuu jamani yanahusu kweli??? Kama kila Hotel ya ufukweni itafanya hivi basi amani uhuru utakuwa umeingiliwa kwa kiasi kikubwa.

Hivi hamuwaonei huruma watoto wetu huku?? Mchana hata kulaza mtoto huwezi achilia mbali wanaojisomea na kufanya home work. Wapendwa kwenye mambo ya msingi tushikamane kukataa. Hivi hii haiwahusu NEMC??

Queen Esther

Apo tatizo upepo unaobeba io sauti
 
Habari za jioni GT's

Naandika waraka huu nikiwa mkazi wa eneo la Bahari Beach kulalamikia kelele za kila weekend au za masherehe ktk Hotel hii.

Yaani kila week end kuna Ma disco toto nk. Ma DJ wanapiga wanapayuka na kupiga ma taarabu nk yaani ni vurugu tu. Kama ujuavyo upepo nao unabeba hizo sauti yaani utafikiria wote tuko kwenye hizo sherehe. Kila wanachoongea na miziki inayoimbwa inaimbia kwenye nyumba zetu.

Huyu MMILIKI wa hii hotel tumemwomba mara nyingi atuondolee kelele hizi hataki. Serikali tusaidieni jamani. Uhuru gani huu Kama sio kukomoana kwa raha za watu wengine??? Kama uko maeneo ya Bahari Beach hadi Kunduchi naona utakuwa umenielewa. Tuungane KUKATAA haya makelele. Mtu huwezi kupumzika jamani!!!!!

Wahusika tusaidieni.

Queen Esther

Akhsante Kwa Kutufahamisha Kuwa Unakaa au Unaishi Ushuani BAHARI BEACH.
 
Back
Top Bottom