Kelele Hoteli ya Bahari Beach

Kelele Hoteli ya Bahari Beach

Makelele yaendelee hapa kazi tu!Si kuna sheria zinazokataza umeipigania hapa kazi tu!Haya endelea na makelele mbele kwa mbele mpaka ufe.
Mkuu hapa ndio umefika mwisho wa kufikiri?naona comment kama za watu wa "hapa na pale"
 
Habari za jioni GT's

Naandika waraka huu nikiwa mkazi wa eneo la Bahari Beach kulalamikia kelele za kila weekend au za masherehe ktk Hotel hii.

Yaani kila week end kuna Ma disco toto nk. Ma DJ wanapiga wanapayuka na kupiga ma taarabu nk yaani ni vurugu tu. Kama ujuavyo upepo nao unabeba hizo sauti yaani utafikiria wote tuko kwenye hizo sherehe. Kila wanachoongea na miziki inayoimbwa inaimbia kwenye nyumba zetu.

Huyu MMILIKI wa hii hotel tumemwomba mara nyingi atuondolee kelele hizi hataki. Serikali tusaidieni jamani. Uhuru gani huu Kama sio kukomoana kwa raha za watu wengine??? Kama uko maeneo ya Bahari Beach hadi Kunduchi naona utakuwa umenielewa. Tuungane KUKATAA haya makelele. Mtu huwezi kupumzika jamani!!!!!

Wahusika tusaidieni.

Queen Esther
Waambieni NEMC na nakiri kwenye magazeti ili tuone watakavyofanya kazi tuwapime. Tumeona kwenye kubomoa nyumba wako safi, sasa tunataka tuone na kelele za makusudi na udhia kama watazizuia. Kumbuka wameshatoa taadhari kuhusu hili suala.
 
Last edited:
Wewe na Bahari beach nani amemfata mwenzie?

Bahari Beach au Bahari Beach Hotel?

Je hilo lina uhusiano gani na malalamiko ya makelele ya hao owners kwenye haya makazi ya watu??? Tena kuna kiingilio na Serikali imesema fukwe zote ni bure????

Queen Esther
 
Mtoto utamlaza na earphone??? Watoto wanaosoma na kufanya home work watavaa earphone??? Kama mna mazungumzo ya familia wote mvae earphone nk

NEMC ituoneshe kibali cha hii Hotel Kama kuna sehemu walisema watachezesha Ma disco na Ma taarabuu mchana kutwa na usiku kucha ni masherehe!!!! Ma spika ni makali yaani sijui nisemeje?? Pia mambo yanayojadiliwa huko hayatuhusu lakini wote tunasikia!!! Je hii ni sawa??

NEMC tunawaangalia kwa macho matatu kwenye jipu hili la Bahari Beach!!

Queen Esther

Mkuu vaa earphones tulia zako acha watu wale raha zao
 
Habari za jioni GT's

Naandika waraka huu nikiwa mkazi wa eneo la Bahari Beach kulalamikia kelele za kila weekend au za masherehe ktk Hotel hii.

Yaani kila week end kuna Ma disco toto nk. Ma DJ wanapiga wanapayuka na kupiga ma taarabu nk yaani ni vurugu tu. Kama ujuavyo upepo nao unabeba hizo sauti yaani utafikiria wote tuko kwenye hizo sherehe. Kila wanachoongea na miziki inayoimbwa inaimbia kwenye nyumba zetu.

Huyu MMILIKI wa hii hotel tumemwomba mara nyingi atuondolee kelele hizi hataki. Serikali tusaidieni jamani. Uhuru gani huu Kama sio kukomoana kwa raha za watu wengine??? Kama uko maeneo ya Bahari Beach hadi Kunduchi naona utakuwa umenielewa. Tuungane KUKATAA haya makelele. Mtu huwezi kupumzika jamani!!!!!

Wahusika tusaidieni.

Queen Esther

Akhsante Kwa Kutufahamisha Kuwa Unakaa au Unaishi Ushuani BAHARI BEACH.
GENTAMYCINE huishi vituko!!! Kweni ume-mind?? Si unajua tena extended family??

Queen Esther

Hujanizoea Tu Queen Esther? Nilikuwa Nakutania Tu Kwani Hata Mimi Nina Watu Wangu Wa Karibu Wanaishi Huko Hasa Hasa Hapo Njia Panda Ya Kuelekea Bahari Beach Mkabala Na Hiyo Hotel Kubwa Mkono Wa Kushoto.
 
Kazi tu, tukisema kazi tunamaanisha hivo. Kama mziki na kukodisha ukumbi ndo kunaingiza kipato halali cha mmiliki wa bahari beach then wapige kazi 24/7
 
Mwasu sio nguvu ya upepo tu!!!

Kelele hizi zimezidi. Hakuna faragha huku yaani uswahilini ni afadhali!!! Ni mwendo wa Ma disco na ma taarabuu tuu!! Hii haikubaliki hata kidogo.

Watoto wetu wanasoma saa hizi na kumalizia home work. Kwa kelele hivi kwa kweli ni shida na haya ni makwazo ya MAKUSUDI.

Serikali tusaidieni. Hii ni Hotel ya kitalii Kama inavyojiita au ukumbi wa disco???? Basi waweke sound proof!!

Queen Esther
Mkuu nilikuwa nataka kuhamia huko BB.. ila sasa najishauri nisije wapoteea wadogo zangu Mood ya kusoma!!
 
Umeenda wizara ya mazingira kutoa malalamiko ukashindwa kusaidiwa??
nakushauri nenda kwanza huko kuliko kulalamika tu bila dira.
ni kama mimi niseme" queen esther mchoyo kweli "wakati hata sijajaribu kukuomba ukaninyima
 
Hoteli ya Bahari Beach ilikuwa Nje ya Mji ... Mmeifuata na Kumpangia cha kufanya mwenyeji wenu ...Nendeni Mkaongee nae, akiwazidi fungeni sound Proof nyumba zenu ...kama Mliweza Kujenga au Kupanga apartment ...Mtashindwa SoundProof.... its peanuts
 
Ushirikiano ni pale you got something in common. Sasa kweli mtu wa Tandale atashirikiana na wa bahari beach? wapi na wapi ndugu yangu? Wewe jipange na wanene wenzako huko uzunguni kwenu...

Cruel world...enheee?
 
Back
Top Bottom