View attachment 956046
Baada ya Katibu Mkuu wa CCM, bashiru Ally Kakurwa kumtaka Membe aende ofisni kwake kujibu tuhuma za njama zake za kuunda Makundi ndani ya Chama hicho tawala, Viongozi wa vyama vya upinzani vya CHADEMA na ACT-Wazalendo na Vijana wa Vyama hivyo Mitandaoni walianza kusambaza Ujumbe usemao "Twende na Membe 2020" na kauli mbiu ya #KaziNaBata ambapo mwanzoni wengi waliamini ujumbe huo ulilenga kutaka kuuaminisha Umma kuwa Membe anaweza kupeperusha bendera ya CCM 2020.
Kumbe ukweli ni kwamba baada ya Membe kupoteza matumaini ya kugombea urais kupitia CCM kutokana na mambo makubwa ya Maendeleo na huduma za Jamii anayoyafanya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Shushushu wa zamani ametumia taaluma yake hiyo vizuri na kufanikiwa kuwashawishi watu wenye ushawishi ndani ya upinzani majukwaani na Mitandaoni wamuandalie mazingira ya kuhamia upinzani na kugombea urais 2020.
Imekwa kama ni bahati kwa issue ya Membe kuibuka kipindi ambacho Tundu Lissu bado yuko Hospitalini, Mbowe yuko Rumande. Godbless Lema, Yeriko Nyerere na vijana wengine ambao ni watiifu kwa Mbowe na Lissu kungana na Zitto Kabwe kusambaza ujumbe wa "Twende na Membe 2020" kwa uhuru zaidi.
Hali hii imemuacha njia panda Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na mgombea urais 2015 aliyewakilisha vyama vilivyounda Umoja wa UKAWA na kuviwezesha kupata viti vingi vya Madiwani na Wabunge.
Haijafahamika kama Mbowe naye anaujua mkakati huu wa Membe (amebadili gia angali) na kumtosa Lowassa. Tundu antipas Lissu ambaye licha ya kuwa hospitali amekuwa mahiri sana wa kufuatilia siasa za Tanzania ya kutoa maoni yake hajasema chochote kuhusiana na akina Lema na kauli yao ya Twende na Membe 2020. ZIpo taarifa kuwa huenda ukaribu wa Lowassa na Rais Dkt. John Magufuli ndiyo unaomponza na kupelekea Chadema nao kuamua kumwaga Mboga.