Kazi na bata vs hapa kazi tu

Kazi na bata vs hapa kazi tu

Hayo ni maneno tu mnaletewaga kila awamu, mimi siku zote napiga kazi na kula bata pia ndo maana hiyo kazi na bata hainihusu sisubiri kudanganywa na wanasiasa na slogan zao za uongo.Mkuu bora anayekwambia kazi tu anajua bata lipo pale pale kuliko anayekuongopea kazi na bata as if atawagawia watu pesa wakale bata.
We nae cjui unaandika vinini au ulipo dish lishayumbishwa na Serengeti lite nini?
 
Siasa za Zitto zenyewe za kishamba tu, tangu akiwa Chadema amekuwa na siasa za kujikombakomba, kujionesha onesha, kusalitisaliti tu, hizi ni siasa za kishamba sana.
Katika kujifanya mzalendo, Zitto amekuwa mshambamshamba tu, amekuwa mtu wa kuzitishiatishia Taasisi za Umma ili zimhonge asianike maovu, amediriki hata kutetea ukiukwaji wa maadili ya nchi yetu na kuwa kibaraka wa Wazungu wanaotaka kutupa misaada kwa masharti ya kukubali Ushoga. Huu ni ushamba wa Hali ya juu.

Bata huliwa na wastaabu. Zitto hata mahusiano yake yamekuwa ya kishamba tu, ndiye mwenye historia ya kuoa wake wawili ndani ya Wiki moja.

Ulimbukeni ni kitu kibaya sana. Limbukeni anaweza kufanya mambo ya ajabu bila ya kuona aibu ila wanaomzunguka wakaona aibu kwa niaba yake. Kitu kibaya sana.
Zitto washawishi Watanzania kwa kitu kingine wakuelewe washawishike kukuona unafaa kuwa Rais, hili la kula bata, sifa hiyo huna kwa sababu mpaka hapo ulipo na zaidi ya miaka 40 huna historia ya kila Bata, Unataka kula Bata ukiwa Rais? Uzeeni? Kwanza nani alikwambia Watanzania wanamtaka Rais mla Bata? Unakumbuka 2015 kuna Mgombea alipata tabu sana kwa sababu tu ya kawaida yake ya kunyoa Unga? Itakuwaje Wewe unaetaka kula Bata ambayo huna hitoria nayo bali kwa sababu tu wewe ni Rais .

Urais ni ngazi ya juu kabisa katika nchi yetu, msiwe mnaropoka ropoka tu kama mtu anayeutaka urais wa Wasaf au Team Kiba. Au unautaka urais wa Leka Dutigite ile Taasisi ulioianzisha kwa Fedha za Walipa kodi ulizohongwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jami wakati ulipokuwa Mwenyekiti wa PAC?

Acha wivu!hayo ni mashambulizi binafsi,kwahiyo unataka kutuaminisha kua ile taarifa ya watu kuhongwa kuhujumu mradi wa mchuchuma jamaa anataka rushwa!?

Kwa akili hizi ni bora kabisa hata hiyo 25% ya mafuo ipunguzwe tu iwe 15%!
 
Umepotosha, Kama kawaida ni propaganda za kiBAVICHA zaidi.

Hapa kazi tu ni slogan iliyobeba philosophy ya kuthamini kazi, kukubali kwamba matatizo yetu tutayatatua wenyewe, tutangulize kuwajibika kuliko kitu chochote, tusipende kutafuta visingizio kwa changamoto tunavyokumbana nazo.

Hapa kazi tu inaongeza ajira, inakuza uchumi hasa kupitia viwanda, idadi ya wanaopewa mikopo ya elimu ya juu imeongezeka(mtoa mada anasema hamna mikopo!!), kuboresha tija kwa wakulima(mifumo na gharama za pembejeo zimebireshwa sana ,tofauti na mtoa mada), huduma kwa wananchi kama afya na elimu zimeimarishwa, miundo mbinu imeimarishwa na inazidi kujengwa. Matokeo chanya na makubwa ni mengi na yako wazi, lakini uzi huu haujalenga zaidi kuelezea hayo ila kumjibu mtoa mada.

Kiuhalisia aliye kuja na slogan hii kaleta mapinduzi makubwa ya fikra na kuendesha siasa. Ikumbukwe kabla yake kulikuwa na kauli mbiu laini na ya kuvutia "kisiasa" " maisha Bora kwa kila mtanzania". Lakini yeye Ali risk na kuja na kauli mbiu iliyobeba ukweli zaidi badala ya cosmetic statements. Hili kiuhalisia si jambo dogo hata kidogo.

Sasa "kazi na bata" kwanza lugha tu ya "bata" inaashiria lack of ; seriousness, maturity, focus, na commitment. Ata baadhi ya wanaoamini hili ni mateenegers tu, na wengi tume pitia huko, baada ya maturity tuligundua ni ujinga tu. Kwa ngazi ya mtu binafsi tu, ili usonge mbele kimaisha kipaumbele ni kazi. Bata haiwezi ikawa kipaumbele labda inaweza ikawa ni matokeo. Angalia tu vijana ambao wanaamini "kazi na bata" tunao wengi mitaani, wote wanaishia kuchemsha.

Kiufupi anayeelewa dhana ya umuhimu wa kufanya kazi, hawezi akaamini kwenye umuhimu wa kula bata. Sembuse kwa kiongozi wa ngazi nchi!
 
Nilisoma na Zitto sehemu fulani sio mshamba kama unavyojidanganya
 
Siasa za Zitto zenyewe za kishamba tu, tangu akiwa Chadema amekuwa na siasa za kujikombakomba, kujionesha onesha, kusalitisaliti tu, hizi ni siasa za kishamba sana.
Katika kujifanya mzalendo, Zitto amekuwa mshambamshamba tu, amekuwa mtu wa kuzitishiatishia Taasisi za Umma ili zimhonge asianike maovu, amediriki hata kutetea ukiukwaji wa maadili ya nchi yetu na kuwa kibaraka wa Wazungu wanaotaka kutupa misaada kwa masharti ya kukubali Ushoga. Huu ni ushamba wa Hali ya juu.

Bata huliwa na wastaabu. Zitto hata mahusiano yake yamekuwa ya kishamba tu, ndiye mwenye historia ya kuoa wake wawili (Binti Jaji na Mhe. Mbunge) ndani ya Wiki moja.
Ulimbukeni ni kitu kibaya sana. Limbukeni anaweza kufanya mambo ya ajabu bila ya kuona aibu ila wanaomzunguka wakaona aibu kwa niaba yake. Kitu kibaya sana.
Zitto washawishi Watanzania kwa kitu kingine wakuelewe washawishike kukuona unafaa kuwa Rais, hili la kula bata, sifa hiyo huna kwa sababu mpaka hapo ulipo na zaidi ya miaka 40 huna historia ya kila Bata, Unataka kula Bata ukiwa Rais? Uzeeni? Kwanza nani alikwambia Watanzania wanamtaka Rais mla Bata? Unakumbuka 2015 kuna Mgombea alipata tabu sana kwa sababu tu ya kawaida yake ya kunyoa Unga? Itakuwaje Wewe unaetaka kula Bata ambayo huna hitoria nayo bali kwa sababu tu wewe ni Rais .

Urais ni ngazi ya juu kabisa katika nchi yetu, msiwe mnaropoka ropoka tu kama mtu anayeutaka urais wa Wasaf au Team Kiba. Au unautaka urais wa Leka Dutigite ile Taasisi ulioianzisha kwa Fedha za Walipa kodi ulizohongwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jami wakati ulipokuwa Mwenyekiti wa PAC?
Zitto ni bonge la mshamba fulani na limbukeni mkubwa.
Anajidai kuongelea kazi na bata ili kuwanufaisha watu wa Dar es Salaam wale gambe na kuiacha Kigoma ikiendelea kuvuta mkia katika maendeleo.

Mkoa wake una umasikini mkubwa wa hadi asilimia 40% lakini yeye anawaza mitungi, plant (bangi) na mikasi? Anajidai mtoto wa mjini mla gambe kumbe zwazwa fulani tena lishamba tu.
Serikali inapigania kuinua Mkoa wako masikini wewe unapigania watu wa Dar. Hana aibu Kigoma wanatumia MV Liemba ya Mjerumani yenye miaka zaidi ya 100 yeye anaona poa tu. Kuna vijiji vingi mwambao wa Ziwa Tanganyika havina usafiri na hulazimika kupitia mpaka Burundi, yeye anaona poa tu.

This is Tanzania.
 
Siasa za Zitto zenyewe za kishamba tu, tangu akiwa Chadema amekuwa na siasa za kujikombakomba, kujionesha onesha, kusalitisaliti tu, hizi ni siasa za kishamba sana.
Katika kujifanya mzalendo, Zitto amekuwa mshambamshamba tu, amekuwa mtu wa kuzitishiatishia Taasisi za Umma ili zimhonge asianike maovu, amediriki hata kutetea ukiukwaji wa maadili ya nchi yetu na kuwa kibaraka wa Wazungu wanaotaka kutupa misaada kwa masharti ya kukubali Ushoga. Huu ni ushamba wa Hali ya juu.

Bata huliwa na wastaabu. Zitto hata mahusiano yake yamekuwa ya kishamba tu, ndiye mwenye historia ya kuoa wake wawili (Binti Jaji na Mhe. Mbunge) ndani ya Wiki moja.
Ulimbukeni ni kitu kibaya sana. Limbukeni anaweza kufanya mambo ya ajabu bila ya kuona aibu ila wanaomzunguka wakaona aibu kwa niaba yake. Kitu kibaya sana.
Zitto washawishi Watanzania kwa kitu kingine wakuelewe washawishike kukuona unafaa kuwa Rais, hili la kula bata, sifa hiyo huna kwa sababu mpaka hapo ulipo na zaidi ya miaka 40 huna historia ya kila Bata, Unataka kula Bata ukiwa Rais? Uzeeni? Kwanza nani alikwambia Watanzania wanamtaka Rais mla Bata? Unakumbuka 2015 kuna Mgombea alipata tabu sana kwa sababu tu ya kawaida yake ya kunyoa Unga? Itakuwaje Wewe unaetaka kula Bata ambayo huna hitoria nayo bali kwa sababu tu wewe ni Rais .

Urais ni ngazi ya juu kabisa katika nchi yetu, msiwe mnaropoka ropoka tu kama mtu anayeutaka urais wa Wasaf au Team Kiba. Au unautaka urais wa Leka Dutigite ile Taasisi ulioianzisha kwa Fedha za Walipa kodi ulizohongwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jami wakati ulipokuwa Mwenyekiti wa PAC?
CCM nzima mnahangaishwa na slogan tu mnajiaibisha.

Achaneni na slogan ya kufanyishwa kazi kitumwa twende na #KaziNaBata.
 
Mshamba ni babu yenu aneyetembea na msafara wa helkopta na washawasha
 
Mimi ni mwana CCM mwenzako mkuu!
Usishangazwe na hilo kwani ni agizo huko Lumumba...kwamba wana CCM wote ambao hawalitaki jiwe na sasa wanataka bata wavuliwe uanachama na waitwe Bavicha. Nimesoma thread zote, naona waliokinai jiwe wakitaka bata wote ni wana CCM na hili limewatisha kweli huko Lumumba.
 
Hata wewe si unakomaa usiku na mchana humu ili ulipwe buku 7 ukale bata[emoji1]
 
Back
Top Bottom