Kazi na bata vs hapa kazi tu

Kazi na bata vs hapa kazi tu

Random

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2017
Posts
791
Reaction score
743
Hii ni misemo miwili kutoka pande mbili znazopinzana, hapa kazi tuh! ni motto ya CCM kutoka kwa Rais JPM since 2015,

Kazi na bata ni kutoka kwa wapinzani wa CCM na imeanzishwa na Zitto Kabwe kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiwa na hashtag, imeshika kasi tarehe za mwanzo za Dec 2018

Baaadhi ya wanachama wa CHADEMA wameipokea kwa mikono miwili na wao kuhashtag kwenye kurasa zao, pia wako wasiokuwa wanachama wa CHADEMA au chama chochote pia wameonekana kuibali

Maana ya motto '' Kazi na bata"
Hii inapooza makali ya hapa kazi tuu, baada ya kazi mtu astarehe si unajua labour always prefer leissure? Stress za kazini, vibaruan zckufanye ufikirie kaz mda wote, jipe mda wa bata/starehe kidogo, hii inaeza kuwa ni modified version ya hapa kazi tuu
 
Muungwana wewe upo upande gani?

"Kazi Na Bata"

Kuna wale wa "Kazi Na Bata" wameibuka hivi karibuni hawakubaliani na sera ya "Hapa Kazi Tu". Sera ambayo serikali inasema inanyoosha nchi wakati mtaani hali ni ngumu. Ajira hakuna, mishahara haipandi,zaidi ya nusu ya wanafunzi wa elimu ya juu hawana mikopo, mazao yanaozea mashambani, hakuna pembejeo, wastaafu wanalia mafao yao, pesa imepotea lakini wanaambiwa hapa kazi tu serikali inanyoosha nchi. Wamechoka na hali ngumu iliyopo ya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa kujieleza, hakuna katiba mpya eti ni wakati wa kazi tu.
Kwa upande wao wanataka kazi na bata. Serikali ifanye kazi huku pesa zikiwepo mtaani. Serikali ifanye kazi huku haki za binadamu zikiheshimiwa, uhuru wa kujieleza na demokrasia kwa ujumla.
Serikali ifanye kazi huku watu wakipata ajira, mishahara ikipanda na wastaafu wakipata mafao yao. Serikali ifanye kazi mazao yakipata wateja.
Wadau wa " Kazi Na Bata"wanaona kujenga mabarabara, reli SGR, madaraja, kununua ndege, kuzungushia ukuta Tanzanite, kutunga sheria za madini nk kuende sambamba na maisha mazuri kwa wananchi siyo wananchi waishi kama mashetani huku serikali ikisema yenyewe ni kazi tu.

"Hapa Kazi Tu"

Hawa wanaamini kwamba huu ni wakati wa kazi tu, nchi inyooshwe kwanza maana ilikuwa imeharibika. Wao wanaamini mambo ya demokrasia, uhuru wa maoni na haki za binadamu visubiri kwanza maana ni vikwazo vya maendeleo.

Wadau wa "Hapa Kazi Tu" wanaamini wananchi wanatakiwa kuvumilia wakati nchi ikinyooshwa kwanza kuelekea nchi ya viwanda na uchumi wa kati.
Wananchi wanaolalamika ajira, pesa kutokuwepo mtaani, wakulima kukosa masoko ya mazao, hospitali kukosa dawa wawe wavumilivu mambo yatakaa sawa tu. Kwa mujibu wa wadau wa "Hapa Kazi Tu" tunatakiwa tujifunge mkanda wakati burudoza akirudisha nchi kwenye misingi iliyokuwa imepotea, wakati akipeleka nchi uchumi wa viwanda na wa kati. Waumini wa "Hapa Kazi Tu" wamefikia hatua ya kuomba Burudoza aongezewe muda hata askip uchaguzi ili ajenyooshe nchi kwanza.

Mwanajamvi nahitaji maoni yako wewe upo upande gani?
 
#KaziNaBata Zitto 2020

Kwanza "BATA" inaongeza mzunguko wa hela, mapato ya kodi, utulivu wa kichwa ili kazi ifanyike kwa umakini, amani & upendo utawale, ajira kwa wafanyabiashara & wakulima (wa ngano/tumbaku/zabibu kwaajili ya gambe), watalii (Kuja kula bata), WASANII hata wasiojiweza watapiga shoo hata BAA ZA VICHOCHORONI.[emoji18]

***Hushangai hata YESU aliwaambia wana wa Israel siku ya SABA wasifanye kazi (Wasivue samaki hio siku)???

***Anaesema KAZI TU ina maana anajua zaidi ya Bwana Mkubwa Yesu Mnazareti???[emoji53]
 
Hatuoni dalili ya kunyoosha nchi maana haikupinda,kila kukicha ni afadhali ya Jana,wakulima wamekataa tamaa,ukivuna huna pa kuuzia,watumishi hawana motisha hata mishahara haipandi wakati maisha yanazidi kuwa magumu,bora kazi na bata,kuliko hii ngonjera
 
Hivi Ndege zioizobaki zinatua lini!?

Lissu mbona amekuwa kimya sana now!!???
 
Back
Top Bottom