Uchaguzi 2020 Kawe, Dar: Yaliyojiri mkutano wa Dkt. Magufuli katika viwanja vya Tanganyika Packers

Serikali itatoa Ajira ngapi wewe ?? Hata akiajiri bado watu wengi watabaki mtaani. Tatizo la ajira halijaanza leo! Mbona zimetolewa ajira za madaktari na walimu , hamulioni Hilo!. Miuondombinu inayojengwa si kuna ajira zinazalishwa mule?? Acheni kujitia upofu!.
Nani kasema serikali iajiri? Serikali inaweka mazingira ya kutengeneza ajira. Mfano kurasimisha idara ya sanaa, kurahisisha cost za kufungua biashara (TRA inasumbua), intellectual property rights kusimamiwa n.k sasa ikifeli huko hakuna solution.

Mie binafsi nnafahamu mtu ana app ila kupewa tu copyright imekua shida. Mwingine kaja na idea ya bidhaa anaambiwa haina standardization huko TFDA so alipe zaidi ya 1m ili tu apatiwe standards.

Ssa kwa mifano hyo miwili hao watamlaumu nani kukosa ajira? Mind you wametaka kujiajiri ila serikali ina urasimu wa kipuuzi. Haya kuna zile 10% za halmashauri, to be honest wanufaika hawafikia 0.5 ya walio apply wote nchi nzima.

Sasa ukizingatia halmashauri 80% mpaka mabaraza kuvunjwa zilikua chini ya CCM je unadhani wakina mama na vijana wajasirialamali wakikosa mitaji watamlaumu nani kma sio CCM na Rais wao?

NB: Naomba ujibu kwa hoja specific nilizohoji hapo.
 
Kama miradi yote hii iliyojengwa hukupata ajira ujue wewe ni wale wale ambao wanawza zile ajira za kukaa ofisini kama walivyoambiwa na mababu zao> Mimi nipo kwenye ajira miaka 16 ila kipato cha nje ya ajira ni kikubwa hadi huwa najiuliza huu utumwa wa vyeti ulinipotezea muda sana, njoo kanda ya ziwa kwenye migodi ya wachimbaji wadogo wadogo uone wenzako graduates wa vyuo vyenye heshima kama MUHAS wanavyokamua pesa wewe!
Huu ndio upuuzi wa JF yeye kahoji makundi ww unajibu specifically kwangu mimi? Kwani kura yangu si moja tu. Hapa ongelea 15M plus vijana wasio na ajira sababu ya mitaji ama mazingira kutowekwa vizuri na serikali.

Nmeongelea kuanzia Intellectual property rights, urasimishaji wa sanaa (Hadi kozi ziwepo chuoni), 10% za halmashauri kufikia walengwa, urasimu kwenye kutafuta standards hasa kwa wajasiriliamali wadogo n.k hivo vyote serikali ina uwezo nao na sio hao wachimbaji wa huko maporini kwenu.

Jibu hoja hapo kijana akikosa 10% ya halamshauri amlaumu nani hapo? Serikali inaamua muelekeo wa sekta binafsi. Serikali ikiweka sera mbovu usitegemee sekta binafsi itazalisha ajira. Ssa kma haya hufahamu basi sishangai unashabikia graduates wa MUHAS kuchimba mifereji ilihali kuna gap kwenye medical sector ndani na nje ya nchi.
 
Askofu Gwajima vitu vidogo tu mpk asome kaandika kwenye simu na note book. Huyu angebaki tu kwenye kanisa lake huku ule mvuto aliokuwa nao wakati wa masakata yake na Pengo na Makonda nk kiasi watu kuwa radhi kumsikiliza kwenye clip na kwenda kanisani huku hana kbs kwenye siasa anazungusha kiuno tu
mwache asome,amezoea uongo..anaogopa kupiga bomu la uongo
 
Jua linachomoza, madimbwi yamekauka kwa Upendo wa Mungu na watu kwa maelfu wanaelekea viwanja vya Kawe Tanganyika packers kumsindikiza kipenzi cha watanzania Dr Magufuli...
Sialisema hapeleki maendeleo kwa wapinzani, asituone ss ni wajinga!! tar 28 tuna jambo letu!!
 
Anayaorodhesha matatizo yote ya Kawe lkn anadai hayajatatuliwa kwasababu:-

Mbunge hakuwa na mahusiano mazuri na mawaziri. Kwani miradi inatekelezwa ktk majimbo kwa kutongozana?

Mbunge aliyekuwepo hakuwa jasiri kama Gwajima. Kwani bungeni ili kuoitisha bajeti mpk vita ipiganwe?

Mbunge aliyekuwepo hakuwatetea wanaKawe. Hoja mfu kabisa hii. Kuna clip nyingi Sana zinaonesha Halima akiwasemea wanaKawe.

Huu ulaghai wa kisiasa wanaKawe tuukatae.
 
Jua linachomoza, madimbwi yamekauka kwa Upendo wa Mungu na watu kwa maelfu wanaelekea viwanja vya Kawe Tanganyika packers kumsindikiza kipenzi cha watanzania Dr Magufuli...
Mbona Kama magufuri anatumia Nguvu kubwa Sana kumnadi Gwajima kuliko mgombea ubunge CCM.kunanini?Apo kawe
 
Tumekusikia mheshimiwa Magufuli , umempigia tafu mbunge mtarajiwa Gwajima. Kwa kweli kwa ahadi za miundombinu uliyoitaja, hapo umefunga kazi. Asante kwa kusikia kilio chetu, na umetaja karibu sehemu zote ambazo ni kero huku Kawe.

Kura zote kwa Gwajima!
 
Anasema alikuwa hajui matatizo ya Kawe ila mbona huwa tunaambiwa wakuu wa wilaya ndiyo wawakilishi wa Rais wilayani, sasa huwa wanawasiliana naye kuhusu nini kama siyo matatizo yaliyoko katika wilaya zao?
 
Kawe hiyo: Shughuli imeisha
My humble and honest observation kwa Jiji la DSM;

Kwa hali niliyoiona ktk mikutano ya CCM na ile ya vyama via Upinzani jijini DSM, sidhani tena kama kuna chama chochote cha Upinzani kitapata hata kiti kimoja cha Ubunge, kuna uwezekano mdogo wa Upinzani kupata madiwani ktk kata hapa na pale.

Kura za Urais JPM atapata asilimia kubwa sana kumzidi mpinzani wake wa karibu.

My 5 cents.
 
Back
Top Bottom