Kauli ya Pinda sasa kwa January Makamba

Kauli ya Pinda sasa kwa January Makamba

To Hon. Makamba Why do you think that Watu kutoka Bumbuli are more "Tanzanians" than watu kutoka Arusha. Kwamba watu wa Bumbuli wana Haki ya Kumkataa Mwekezaji kwa njia ya amani lakini watu wa Arusha hawana haki ya kumkataa kiongozi wasiyemtaka kwa njia ya Sanduki la kura. Au ndio Ugimbi wa Madaraka
 
Lakini ikumbukwe hicho kichapo kilitembea kabla ya kauli ya Pinder
 
Kweli, Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu ni mchungu. ngawa nahisi kilichofanyika ni mbinu ya kutaka ieleweke kuwa jamaa wako fair na wanagawa dose sawa bila kujali itikadi ya mkosaji, hHivi Makamba Jnr anataka aseme hakujua kuwa Policcm ni ma-robots ambao wakipigwa ufunguo wanafanya kwa uelekeo na matakwa ya mtengenezaji!
 
Komredi January,

Uendelee kutujuza kila litakalojiri wakati mkiwa kwenye mapambano na jeshi lenye maelekezo kutoka kwa waserikali wenzako huko mkoani...! Ningekuwa wewe nisingeenda badala yake ningeongea na Waziri Mkuu kwanza maana kumbuka Komredi wewe una maslahi ya 100 kwenye serikali ukivaa ile kofia nyingine...na pia kwa wananchi wako ukivaa hii ya kwetu sote...sasa hapo ku-balance ungepaswa kupatanisha tu sababu uko nao hao wakubwa, usihangaike kama sisi makapuku wengine, wenzako hawatokuelewa!
 
Serekali ya CCM inatapatapa. Januari makamba hana haja ya kulalamika kwa sababu yuko serekalini na ni waziri na kiongozi wake, Pinda alisema watu wapigwe tu, tena wapigwe sana. Kwa hiyo ni mwanzo tu, wataendelewa kuigwa watu mpaka pale CCM itakapoondoka madarakani
 
Hii hapa chini ni post ya January Makamba toka kwenye facebook wall yake: Masaa 2 yaliyopita.

Yaliyojiri leo Mponde, Bumbuli:

Tarehe 26 Mei 2013, wakulima wa Chai Bumbuli waliazimia kumkataa mwekezaji/mbia kwenye kiwanda chao cha Chai Mponde ambaye wanaamini alikuwa anawadhulumu. Pia waliazimia kwamba viongozi wao wa wakulima wa Chai ambao wameshindwa kusimamia maslahi yao na kujali matumbo yao tu, waondoke. Vilevile, waliamua kuuza chai yao kwenye viwanda vya jirani na hivyo kiwanda chaMponde kufungwa. Na katika kipindi chote hiki kumekuwa na utulivu wananchi wakisubiri suluhu ya matatizo yao.

Jana, Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto waliamuru kiwanda kifunguliwe hata kwa mtutu wa bunduki na leo wakapelekwa askari polisi wakiwa na silaha. Katika kulazimisha kiwanda kifunguliwe wananchi wamepigwa na watu watano wamejeruhiwa. Kabla ya polisi kwenda hakukuwa na ghasia yoyote, watu walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida. Kitendo cha kupigwa wananchi kimewaudhi sana wananchi na kimeniudhi sana na mimi, wanauliza kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki pahala ambapo hapakuwa na fujo na kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki kumlinda mwekezaji ambaye wananchi kwa kauli moja walimkataa - tena walimkataa kwa amani bila fujo. Bahati mbaya au nzuri, ni mwekezaji huyu huyu ndiye aliyekuwa na matatizo na wakulima wa chai kule Lupembe, Iringa ambao walilazimika kuvamia kiwanda na kukichoma moto. Sisi hatukuamua kufanya hivyo kwa kuwa sio sahihi.

Nimeongea na IGP kwamba kuwe na restraint. Watu wetu huwa sio watu wa fujo. Hata hivyo, watu wakiwa na hisia kwamba wanaonewa wanaweza kufanya chochote. Naelekea huku kuungana na wananchi wangu, kama ni kupigwa tupigwe sote.

My Take: Kila siku watanzani wengi tumekua tukilalamika kuhusu vyombo vya ulinzi na usalama kutumia nguvu,mabavu,unyanyasaji na hata mauaji ya watu wasio kua na hatia na mbaya zaidi vitendo hivyo hutokea wakati wanachi wakidai haki zao za msingi kabisa na badala yake Polisi na baadhi ya viongozi huwageuzia kibao hao wanachi na kusema kwamba walikua wakifanya fujo au vitendo vya kuvunja amani...Wanachi tunapigwa mabomu ya machozi,risasi za moto, virungu,tunamwagiwa maji ya sumu bila sababu zozote za msingi, polisi wanatumiwa na viongozi kisiasa na hata kwa maslahi yao binafsi ,wabunge wa upinzani wakiyasema haya bungeni Ccm mnawazomea na kuwaita waongo.Hope kwa hili la Bumbuli litakua fundisho kwako wewe January na wana ccm wenzako wanaotetea wawekezaji wanyonyaji na wenye sura ya kuwekwa kifisadi na watawala wetu.FEEL THE TASTE OF YOUR OWN MEDICINE.nakutakia kila la kheri ndugu January Makamba unapokwenda kuwapigania wakulima wa chai wanaonyanyaswa na mwekezaji pamoja na serikali yao walio ichagua.
 
Komredi January,

Uendelee kutujuza kila litakalojiri wakati mkiwa kwenye mapambano na jeshi lenye maelekezo kutoka kwa waserikali wenzako huko mkoani...! Ningekuwa wewe nisingeenda badala yake ningeongea na Waziri Mkuu kwanza maana kumbuka Komredi wewe una maslahi ya 100 kwenye serikali ukivaa ile kofia nyingine...na pia kwa wananchi wako ukivaa hii ya kwetu sote...sasa hapo ku-balance ungepaswa kupatanisha tu sababu uko nao hao wakubwa, usihangaike kama sisi makapuku wengine, wenzako hawatokuelewa!

Unafiki mwinginehuu...wewe unajifanya si mmoja wao ilhali bungeni mlimpigia sana makofi Pinda alipokuwa anamwaga upuuzi wake!? Mtalaaniwa kwa unafiki wenu!!
 
Naombeni mwongozo, inapotokea Naibu Waziri anapingana na bosi wake yaani Waziri Mkuu, mimi mwananchi nifanye nini?
kwa nchi hii shika jembe ukalime. Wasanii tu hao
 
Wadau, kwenye ukurasa facebook wa Januaary Makamba analalamikia nguvu kubwa waliyotumia polisi kuwapiga wananchi wake...amesahau Pinda alisema wapigwe tu.....soma hapa chini kutoka ukurasa wake wa facebook

"Yaliyojiri leo Mponde, Bumbuli:

Tarehe 26 Mei 2013, wakulima wa Chai Bumbuli waliazimia kumkataa mwekezaji/mbia kwenye kiwanda chao cha Chai Mponde ambaye wanaamini alikuwa anawadhulumu. Pia waliazimia kwamba viongozi wao wa wakulima wa Chai ambao wameshindwa kusimamia maslahi yao na kujali matumbo yao tu, waondoke. Vilevile, waliamua kuuza chai yao kwenye viwanda vya jirani na hivyo kiwanda cha Mponde kufungwa. Na katika kipindi chote hiki kumekuwa na utulivu wananchi wakisubiri suluhu ya matatizo yao.

Jana, Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto waliamuru kiwanda kifunguliwe hata kwa mtutu wa bunduki na leo wakapelekwa askari polisi wakiwa na silaha. Katika kulazimisha kiwanda kifunguliwe wananchi wamepigwa na watu watano wamejeruhiwa. Kabla ya polisi kwenda hakukuwa na ghasia yoyote, watu walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida. Kitendo cha kupigwa wananchi kimewaudhi sana wananchi na kimeniudhi sana na mimi, wanauliza kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki pahala ambapo hapakuwa na fujo na kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki kumlinda mwekezaji ambaye wananchi kwa kauli moja walimkataa - tena walimkataa kwa amani bila fujo. Bahati mbaya au nzuri, ni mwekezaji huyu huyu ndiye aliyekuwa na matatizo na wakulima wa chai kule Lupembe, Iringa ambao walilazimika kuvamia kiwanda na kukichoma moto. Sisi hatukuamua kufanya hivyo kwa kuwa sio sahihi.

Nimeongea na IGP kwamba kuwe na restraint. Watu wetu huwa sio watu wa fujo. Hata hivyo, watu wakiwa na hisia kwamba wanaonewa wanaweza kufanya chochote. Naelekea huku kuungana na wananchi wangu, kama ni kupigwa tupigwe sote."

Nafikiri yeye as mbunge wao akiwa umeajiriwa kama naibu waziri katika serikali hiyo hiyo hakutakiwa kutoa malalamiko haya kwenye social media. Anatakiwa kuongoza kwa kuonyesha mifano. Kama kweli ameudhika wananchi wake kutandikwa bila kuwa na kosa lolote, kwa nini bado anaendelea kuwa sehemu ya serikali hiyo?????
Kwa kuwa amepata unaibu waziri kupitia kura za hao waliopigwa na serikali yake, sasa ni wakati wa kuonyesha uongozi kwa vitendo kuwa amechukizwa na kitendo hicho huku akitanguliza barua ya
RESIGNATION kwa Kikwete.
Kama akishindwa kufanya hivyo (kuongoza kwa mifano), then he needs to shut the "hole" period.
 
Kunya anye kuku, akinya bata ameharisha.

Huu ni mfano wa police brutality inayolalamikiwa na CHADEMA kila siku ila tunaonekana kuwa ni watu wa fujo na polisi ndo huonekana kuwa sahihi kila mara.

Mizengo Peter alisema tupigwe tu.

Sasa ni dhahiri serikali ya CCM vipande-vipande.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
This is silly! haki haiwi haki kwa sababu wewe umeathirika; haki ni haki hata adui yako anapoathirika. Viongozi wa CCM wanapokuwa kimya wakati wapinzani wananyanyaswa na hawatoi kauli yoyote ya kuonesha kujali badala ya kauli za jumla jumla wao wanapogeukwa watu wengine tunaangalia na hatuelewi. Kama kupiga raia wasio na hatia ni makosa; basi ni makosa haijalishi nani anapigwa. Hata adui yako akipigwa inabidi umtetee. Tulipolaani kauli ya Pinda si kwa sababu inawalenga CDM; bali kwa sababu inahalalisha impunity ya polisi kwa raia. It is that simple. Haijalishi raia ni wa chama, dini, kabila au eneo gani la jiografia.
 
Komredi January,

Uendelee kutujuza kila litakalojiri wakati mkiwa kwenye mapambano na jeshi lenye maelekezo kutoka kwa waserikali wenzako huko mkoani...! Ningekuwa wewe nisingeenda badala yake ningeongea na Waziri Mkuu kwanza maana kumbuka Komredi wewe una maslahi ya 100 kwenye serikali ukivaa ile kofia nyingine...na pia kwa wananchi wako ukivaa hii ya kwetu sote...sasa hapo ku-balance ungepaswa kupatanisha tu sababu uko nao hao wakubwa, usihangaike kama sisi makapuku wengine, wenzako hawatokuelewa!
Wenzake hawatamuelewa kwasababu serikali ya ccm haipo kwa maslahi ya wananchi.

Je kwa snerio hii hamuoni kuwa hii ni sababu nyingine muhimu ya kutumia katiba mpya kutenganisha uwaziri na ubunge??!

Then, wewe dr vitumbua kama wewe unajiita kapuku huoni sababu ya serikali ya ccm kuondoshwa madarakani kwa hili kosa la kukumbatia muwekazaji na kuwatelekeza wananchi waliowapa nyie ridhaa ya kuwatumikia?????

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Nini cha ajabu wao kupigwa? Mbona Arusha na Mtwara wamepigwa? Na wao WAPIGWE TU...
 
Nilisema siku moja hapa hii sio kauli ya kuifurahia hata kidogo,itamkumba kila mtu katika nafasi yake iwe kweli kuwa wananchi hawajatii amri halali au basi tu polisi watumie mwanya huo kufanya uhalifu na maovu mengine kwa raia.....tuendelee kusubiri.
 
Januari,

Sasa umeiamini ile methali maridhawa ya lugha yetu adhimu Kiswahili, isemayo "Ukiona mwenzako ananyolewa, tia maji kichwani."

Ulidhani kauli ya Pinda iliwahusu Watanzania waliopo kambi ya upinzani tu? Tutapigwa sana, tena sana!

Wao wameshika "mpini", sisi tumeshika "makali". Wakivuta.... Oh... samahani, kumbe wameshavuta mpini, ona damu yetu inavyomwagika!

Kazi ni kwako! (Samahanini Vodacom!)
 
piga hao... piga kabisa .. au uwa kabisa piga wote piga mpaka mbunge piga piga tu tumechoka afande endelea kupiga hao piga pia makamba snr. piga uwa nasema piga tumechoka... piga mbeya piga arusha piga msoga piga tu.... mlichagua ccm wenyewe piga wote....
Hahaha! Teh teh! Pigaa nasisitiza tena wapigwee hawasikii hao uaa. Tena walijipendekeza kutuchagua uaa kabisa!
 
Back
Top Bottom