Kauli ya Pinda sasa kwa January Makamba

Kauli ya Pinda sasa kwa January Makamba

kyumbo

Member
Joined
Jan 21, 2013
Posts
79
Reaction score
33
Wadau, kwenye ukurasa facebook wa Januaary Makamba analalamikia nguvu kubwa waliyotumia polisi kuwapiga wananchi wake...amesahau Pinda alisema wapigwe tu.....soma hapa chini kutoka ukurasa wake wa facebook

"Yaliyojiri leo Mponde, Bumbuli:

Tarehe 26 Mei 2013, wakulima wa Chai Bumbuli waliazimia kumkataa mwekezaji/mbia kwenye kiwanda chao cha Chai Mponde ambaye wanaamini alikuwa anawadhulumu. Pia waliazimia kwamba viongozi wao wa wakulima wa Chai ambao wameshindwa kusimamia maslahi yao na kujali matumbo yao tu, waondoke. Vilevile, waliamua kuuza chai yao kwenye viwanda vya jirani na hivyo kiwanda cha Mponde kufungwa. Na katika kipindi chote hiki kumekuwa na utulivu wananchi wakisubiri suluhu ya matatizo yao.

Jana, Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto waliamuru kiwanda kifunguliwe hata kwa mtutu wa bunduki na leo wakapelekwa askari polisi wakiwa na silaha. Katika kulazimisha kiwanda kifunguliwe wananchi wamepigwa na watu watano wamejeruhiwa.

Kabla ya polisi kwenda hakukuwa na ghasia yoyote, watu walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida. Kitendo cha kupigwa wananchi kimewaudhi sana wananchi na kimeniudhi sana na mimi, wanauliza kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki pahala ambapo hapakuwa na fujo na kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki kumlinda mwekezaji ambaye wananchi kwa kauli moja walimkataa - tena walimkataa kwa amani bila fujo. Bahati mbaya au nzuri, ni mwekezaji huyu huyu ndiye aliyekuwa na matatizo na wakulima wa chai kule Lupembe, Iringa ambao walilazimika kuvamia kiwanda na kukichoma moto. Sisi hatukuamua kufanya hivyo kwa kuwa sio sahihi.


Nimeongea na IGP kwamba kuwe na restraint. Watu wetu huwa sio watu wa fujo. Hata hivyo, watu wakiwa na hisia kwamba wanaonewa wanaweza kufanya chochote. Naelekea huku kuungana na wananchi wangu, kama ni kupigwa tupigwe sote."
 
[h=5]Tarehe 26 Mei 2013, wakulima wa Chai Bumbuli waliazimia kumkataa mwekezaji/mbia kwenye kiwanda chao cha Chai Mponde ambaye wanaamini alikuwa anawadhulumu. Pia waliazimia kwamba viongozi wao wa wakulima wa Chai ambao wameshindwa kusimamia maslahi yao na kujali matumbo yao tu, waondoke. Vilevile, waliamua kuuza chai yao kwenye viwanda vya jirani na hivyo kiwanda cha Mponde kufungwa. Na katika kipindi chote hiki kumekuwa na utulivu wananchi wakisubiri suluhu ya matatizo yao.

Jana, Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto waliamuru kiwanda kifunguliwe hata kwa mtutu wa bunduki na leo wakapelekwa askari polisi wakiwa na silaha. Katika kulazimisha kiwanda kifunguliwe wananchi wamepigwa na watu watano wamejeruhiwa. Kabla ya polisi kwenda hakukuwa na ghasia yoyote, watu walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida. Kitendo cha kupigwa wananchi kimewaudhi sana wananchi na kimeniudhi sana na mimi, wanauliza kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki pahala ambapo hapakuwa na fujo na kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki kumlinda mwekezaji ambaye wananchi kwa kauli moja walimkataa - tena walimkataa kwa amani bila fujo. Bahati mbaya au nzuri, ni mwekezaji huyu huyu ndiye aliyekuwa na matatizo na wakulima wa chai kule Lupembe, Iringa ambao walilazimika kuvamia kiwanda na kukichoma moto. Sisi hatukuamua kufanya hivyo kwa kuwa sio sahihi.

Nimeongea na IGP kwamba kuwe na restraint. Watu wetu huwa sio watu wa fujo. Hata hivyo, watu wakiwa na hisia kwamba wanaonewa wanaweza kufanya chochote. Naelekea huku kuungana na wananchi wangu, kama ni kupigwa tupigwe sote.
[/h]
 
Umemuaga pinda?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Heeee, yakitokea kwenye majimbo yenu ndio mnayaona??? Hayo maneno ungeyasema ukiwa bungeni wakati waziri wako anayatamka na watu wa arusha na mtwara wanapigwa, poleni sana wananchi wa bumbuli mungu atawasaidia.
 
Makamba anashangaa nini wakati polisi wanatekeleza maagizo ya mkuu wake"Wapigwe"
 
Mh. January naomba uwasihi wapiga kura wako watii sheria bila shuruti, nchi haiendeshwi kwa jazba na kweli usipoelewa mtapigwa wote kama ulivyoomba!
 
Tujiulize, HIVI NDIVYO AMBAVYO TUNATAKA NCHI YETU IENDE? JE KUNA MAHUSIANO YOYOTE NA KAULI ZA VIONGOZI WETU WA SERIKALI?
 
Kwa kuwa Wana Bumbuli ni wapole na wakarimu sana, watavumulia tu. Na hata yule waliyemchagua kwa mbwembwe nyingi kama kiongozi wao mkuu alishawasahau toka alivyoapishwa.
 
Inasikitisha mno.

piga hao... piga kabisa .. au uwa kabisa piga wote piga mpaka mbunge piga piga tu tumechoka afande endelea kupiga hao piga pia makamba snr. piga uwa nasema piga tumechoka... piga mbeya piga arusha piga msoga piga tu.... mlichagua ccm wenyewe piga wote....
 
Sasa kama kweli anaenda ili apigwe na akaitishe maandamano wakafunge tena kiwanda!!!!

Wajomba wanasema zilongwa mbalii...

He was there wakati kauli inatoka bungeni.,..wapigeni!!!!!
 
Back
Top Bottom