Kauli ya Pinda sasa kwa January Makamba

Kauli ya Pinda sasa kwa January Makamba

pga tu,nasema piiiga afande chacha, we naniliu,hebu angalia na yale kule yatakimbia hebu taaandika virunu mana tuna ruksa ya pm
 
Mlaumu Waziri mkuu wako. Alipokuwa anawaamuru polisi kupiga raia wabunge wa ccm walipiga makofi wakafikiri hili ni suala linalowahusu CDM tu, Bado tutapigwa sana kama PINDA hatafuta kauli yake.
Usiseme Wabunge wa Ccm walipiga makofi,sema Wabunge wa Ccm mlipiga makofi.
 
Serikali ni moja na waziri mkuu ni mmoja. Kauli ya waziri mkuu inahusu watanzania wote bila kujali eneo, dini, rangi wala jinsia.

Kama watanzania wa Arusha, mtwara, mbeya, morogoro, iringa na mwanza wanapigwa kwa kudai haki zao za msingi kwanini watanzania wa Bumbuli wasipigwe wanapodai haki zao za msingi?. Hii ni double standard na haikubaliki hata kidogo.
Ningemuelewa na kukubaliana na kauli ya Mh January Makamba iwapo angepingana na kauli ya Mh Pinda palepale bungeni Dodoma ama angetoa tamko la kuipinga ile kauli mara moja.
Hii inanionesha wazi kwamba wabunge wengi wa CCM ni wanafiki wakubwa. Ningependa sana Polisi watembeze kichapo cha mbwa mwizi huko jimboni Bumbuli na kama watafanikiwa kumshika Mh January Makamba wampe kichapo kitakatifu na kumsweka ndani.
 
Watanzania dawa yao ndo hiyo. Vipigo vitakatifu,ukiwapiga vipigo makini kesho yake hautamuona hata mmoja akidai eti ameonewa. Nadhani kauli ya pinda imewaingia vilivyo wadanganyika. Tutaendelea kugawiwa vibano vya uhakika mpaka vilema loh
 
Yaliyojiri leo Mponde, Bumbuli:

Tarehe 26 Mei 2013, wakulima wa Chai Bumbuli waliazimia kumkataa mwekezaji/mbia kwenye kiwanda chao cha Chai Mponde ambaye wanaamini alikuwa anawadhulumu. Pia waliazimia kwamba viongozi wao wa wakulima wa Chai ambao wameshindwa kusimamia maslahi yao na kujali matumbo yao tu, waondoke. Vilevile, waliamua kuuza chai yao kwenye viwanda vya jirani na hivyo kiwanda cha Mponde kufungwa. Na katika kipindi chote hiki kumekuwa na utulivu wananchi wakisubiri suluhu ya matatizo yao.

Jana, Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto waliamuru kiwanda kifunguliwe hata kwa mtutu wa bunduki na leo wakapelekwa askari polisi wakiwa na silaha. Katika kulazimisha kiwanda kifunguliwe wananchi wamepigwa na watu watano wamejeruhiwa. Kabla ya polisi kwenda hakukuwa na ghasia yoyote, watu walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida. Kitendo cha kupigwa wananchi kimewaudhi sana wananchi na kimeniudhi sana na mimi, wanauliza kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki pahala ambapo hapakuwa na fujo na kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki kumlinda mwekezaji ambaye wananchi kwa kauli moja walimkataa - tena walimkataa kwa amani bila fujo. Bahati mbaya au nzuri, ni mwekezaji huyu huyu ndiye aliyekuwa na matatizo na wakulima wa chai kule Lupembe, Iringa ambao walilazimika kuvamia kiwanda na kukichoma moto. Sisi hatukuamua kufanya hivyo kwa kuwa sio sahihi.

Nimeongea na IGP kwamba kuwe na restraint. Watu wetu huwa sio watu wa fujo. Hata hivyo, watu wakiwa na hisia kwamba wanaonewa wanaweza kufanya chochote. Naelekea huku kuungana na wananchi wangu, kama ni kupigwa tupigwe sote.
 
Januari Makamba, Tambua kuwa wewe ni miongoni mwa viongozi wa juu nchini. Unaposema nguvu nyingi inatumika hali ya kuwa ninyi ndio mliotoa baraka na kumruhusu Waziri Mkuu kutoa kauli ya wananchi kuupigwa kabla hawajafikishwa kule wanakopelekwaka tena mkamshangilia kwa kuona ni kauli nzuri na inayofaa kutekelezwa. Wale wa Mtwara waliokuwa wanaandamana na kufanya mikutano yao bila bughudha yeyote mliona wanatenda kosa kwa kuongelea gesi kutotoka kwa kuwa ni ya mwekezaji, Arusha kwa kuwa ni wapinzani mkasema wapigwe tu. Leo tena hapo taifa linatetea wawekezaji wake ili waendelee kunufaisha Taifa kama kauli yenu kama chama na serikali inavyosema kila kukicha, Leo unakuja juu kwa kusema imetumika nguvu nyingi.

Hii inadhihirisha kuwa, Ninyi kama viongozi, Mmegeuka na kuwa viongozi wa jamii ndogo sana hasa wale wanaowapa kura na kujisahau kuwa wewe ni Naibu waziri sio tu wa wanabumbuli bali ni watanzania wote.

Ulipaswa kutoa kauli hiyo na kuungana na wananchi popote pale wanapoonewa kwa kuwa wewe sasa ni kiongozi wa watanzania wote, Kuwa mzalendo kama wabunge wa chama fulani tuliona wakishirikiana bila kujali majimbo yao au laa. Walienda kusaidia na kutetea wananchi pale wanakoonewa.
 
Siamini kama haya yameandikwa na January. Kama kweli ni yeye ndo ameandika haya basi ni dhahiri kwamba hajitambui kama yey ni nani katika serikali ya JK. Na kama kweli huu msimamo ni wa kweli basi ajiuzulu uwaziri ili aende akaungane na wananchi kuwatetea. Otherwise, huu ni unafiki na upuuzi kujifanya unapinga maamuzi yanayofanywa na serikali ambayo unaiongoza tena kwa level ya uwaziri. January aache kutufunga kamba.
 
hua mnawacheka chadema sasa makamba na wewe sunilia kipigo na watawapiga kweli maana wamechoka sasa
 
si ndio yeye na wale vibua wenzake kule Bungeni walishangilia saaana Pinda aliposema polisi watupige sisi walalahoi.
CCM WANA AKILI ZA MAITI
 
Na wao yamewakuta!!!Siamini,yakiwa, Bungeni huwa yanashangilia kama yamekatika vichwa!!
 
nyerere alisema ukishakula nyama ya mtu huwezi kuacha... sasa wanakulana wao kwa wao
 
Ndiyoooo ulisema mwenyewe sasa hivi unakuja kuleta huruma ili 2015 urudi mjemgoni haiwezkaniki tena
 
Mheshimiwa Mbunge, nahisi kuwa kwa tafsiri iliyopo, WEWE NI MCHOCHEZI! Unawachochea raia kugoma. Tena huna nidhamu kwa kuwa bosi wako alishasema wazi kuwa sasa ni kichapo tu! Tena nahisi unaleta sera za Chadema wewe! Acha!
 
[TABLE="width: 1013"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]Source: Tanzania Daima 6th June 2013: ​Shelukindo, Makamba vitani
Shelukindo, Makamba vitani



na Hellen Ngoromera


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #FFFFFF"]

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR="bgcolor: #ffffff"]
[TD]UHASAMA wa kisiasa kati ya aliyekuwa Mbunge wa Bumbuli, William Shelukindo na mbunge wa sasa, January Makamba umechukua sura mpya ya kufikishana mahakamani.
Shelukindo aliyeangushwa kwenye kura za maoni mwaka 2010 na Makamba kuwania ubunge kwenye jimbo hilo, ametangaza kumburuza mahakamani mbunge wake.
Mbunge huyo wa zamani ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Chai wa Usambara (UTEGA) alisema atamfungulia kesi ya madai Makamba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi jioni jijini Dar es Salaam, Shelukindo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda cha Kusindika Chai Mponde kupitia Utega, alisema amekashifiwa na Makamba.
Shelukindo alidai kuwa Makamba alisema kuwa yeye anawanyonya wakulima wa chai madai aliyatoa wakati wa mkutano wake na wakulima wa chai aliouitisha Mei 26 mwaka huu.
Katika mkutano huo Shelukindo aliyeambatana na Mwenyekiti Kampuni ya Chai Lushoto iliyoingia ubia na Utega, Nawab Mullah, alisema kitendo cha kuitwa mnyonyaji kimemvunjia heshima.
“Kutangaza kwenye majukwaa kwamba mimi ni mtu wa kunyonya wenzangu ni kunivunjia heshima yangu…, nafikiria kumfungulia kesi ya madai Makamba,” alisema.
Hata hivyo, Shelukindo hakuwa tayari kueleza ni lini na wapi atamfungulia kesi hiyo.
Shelukindo aliongeza kuwa katika mkutano huo, Makamba aliamuru kiwanda hicho kifungwe jambo linalokifanya kipate hasara ya sh milioni 13 kila siku.
Alisema Makamba alitumia mkutano huo kugawa fomu kwa wanaushirika hao wazijaze ili kuunga mkono kuvunjwa na kuundwa upya kwa umoja wa wakulima wa chai Utega.
Kuhusu kuvunjwa kwa Utega, Shelukindo alisema umoja huo unatambulika kisheria na kama kuna haja ya yeye kuondolewa, kuna taratibu za kuzifuata.
“Inatia uchungu kufunga kiwanda na kukosesha mapato huku watu wakikosa ajira, jambo hili limeleta athari kwani kilo 700 za chai zimemwagwa halafu leo hii uniite mimi mnyonyaji, hili si sawa,” alisema'
Tanzania Daima lilimtafuta Makamba kujibu tuhuma hizo ambapo alikiri Shelukindo ni mnyonyaji kwani amewanyonya wakulima kwa muda mrefu na hivi sasa wamechoka.
Kuhusu kuburuzwa mahakamani, Makamba alimtaka Shelukindo aendelee na utaratibu huo na atakutana naye huko.
“Shelukindo ni sehemu ya tatizo la chai Usambara, anawanyonya wakulima, wakulima wanalalamika bei haiwalipi vizuri na hivi sasa wamechoka, na wao ndio walioazimia Utega ivunjwe. Kwahiyo mimi nasimama kwa niaba yao, siwezi kusimama na mafisadi,” alisema Makamba.
Alipoulizwa aliwezaje kuamuru kiwanda kifungwe wakati kisheria hana mamlaka hayo, alisema hizo ni propaganda za kisiasa zenye lengo la kumchafulia jina lake

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Sasa kama kweli anaenda ili apigwe na akaitishe maandamano wakafunge tena kiwanda!!!!

Wajomba wanasema zilongwa mbalii...

He was there wakati kauli inatoka bungeni.,..wapigeni!!!!!

Du jamaa mnafiki huyo nilimuona TBC akishangilia tamko la Pinda ndani ya bunge? au hakumuelewa .
 
wananchi wamepigwa na watu watano wamejeruhiwa.

Kabla ya polisi kwenda hakukuwa na ghasia yoyote, watu walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
Kitendo cha kupigwa wananchi kimewaudhi sana wananchi na kimeniudhi sana na mimi, wanauliza kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki pahala ambapo hapakuwa na fujo na kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki kumlinda mwekezaji ambaye wananchi kwa kauli moja walimkataa - tena walimkataa kwa amani bila fujo. Bahati mbaya au nzuri, ni mwekezaji huyu huyu ndiye aliyekuwa na matatizo na wakulima wa chai kule Lupembe, Iringa ambao walilazimika kuvamia kiwanda na kukichoma moto. Sisi hatukuamua kufanya hivyo kwa kuwa sio sahihi.

Januari, wala usilalamike!... Tulipolalamika kuwa piga piga za polisi zitaleta madhara nyie mlisema "WAKOMESHWE!!"... Wenzako wengi waliona kila anayedai haki katumwa na CHADEMA... PIGENI tu!.. VUNJENI MIGUU!.. Hao siyo CCM wala ndugu zenu PIGA.
 
Back
Top Bottom