Wadau, kwenye ukurasa facebook wa Januaary Makamba analalamikia nguvu kubwa waliyotumia polisi kuwapiga wananchi wake...amesahau Pinda alisema wapigwe tu.....soma hapa chini kutoka ukurasa wake wa facebook
"Yaliyojiri leo Mponde, Bumbuli:
Tarehe 26 Mei 2013, wakulima wa Chai Bumbuli waliazimia kumkataa mwekezaji/mbia kwenye kiwanda chao cha Chai Mponde ambaye wanaamini alikuwa anawadhulumu. Pia waliazimia kwamba viongozi wao wa wakulima wa Chai ambao wameshindwa kusimamia maslahi yao na kujali matumbo yao tu, waondoke. Vilevile, waliamua kuuza chai yao kwenye viwanda vya jirani na hivyo kiwanda cha Mponde kufungwa. Na katika kipindi chote hiki kumekuwa na utulivu wananchi wakisubiri suluhu ya matatizo yao.
Jana, Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto waliamuru kiwanda kifunguliwe hata kwa mtutu wa bunduki na leo wakapelekwa askari polisi wakiwa na silaha. Katika kulazimisha kiwanda kifunguliwe wananchi wamepigwa na watu watano wamejeruhiwa.
Kabla ya polisi kwenda hakukuwa na ghasia yoyote, watu walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida. Kitendo cha kupigwa wananchi kimewaudhi sana wananchi na kimeniudhi sana na mimi, wanauliza kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki pahala ambapo hapakuwa na fujo na kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki kumlinda mwekezaji ambaye wananchi kwa kauli moja walimkataa - tena walimkataa kwa amani bila fujo. Bahati mbaya au nzuri, ni mwekezaji huyu huyu ndiye aliyekuwa na matatizo na wakulima wa chai kule Lupembe, Iringa ambao walilazimika kuvamia kiwanda na kukichoma moto. Sisi hatukuamua kufanya hivyo kwa kuwa sio sahihi.
Nimeongea na IGP kwamba kuwe na restraint. Watu wetu huwa sio watu wa fujo. Hata hivyo, watu wakiwa na hisia kwamba wanaonewa wanaweza kufanya chochote. Naelekea huku kuungana na wananchi wangu, kama ni kupigwa tupigwe sote."
Mkuki kwa chadema kwa binaccm mchunguuuuuuu!Mkuki kwa chadema ccm ha ha ha
Nini cha ajabu wao kupigwa? Mbona Arusha na Mtwara wamepigwa? Na wao WAPIGWE TU...
Unashangaa nini? hujui Bumbuli ni wanaccm, Arusha ni CHADEMA na Mtwara ni CUF? na ujue kuwa Mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya ccm mkoa, na DC nae ni mmwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya ccm wilaya. Naomba urejee kauli ya Baba wa taifa kuhusu ubaguzi "WAO WATANGANYIKA SISI WAZANZIBARI" sasa inakuwa "WAO CHADEMA/CUF SISI CCM" hiki ndicho kinachomshangaza makamba kwa wanaccm kupingwa na viongozi wa ccm. anasahau kuwa wote ni WATANZANIA.
Pinda alisema watapigwe tu wale ambao wamekaidi amri na sheria halali. Tazama mkanda, hakusema polisi wapige watu bila sababu za msingi.
Wakulima katika kiwanda cha Mponde wamepigwa bila kukaidi amri yoyote ya polisi.