Kauli hii inanikera, nifanyeje?

Kauli hii inanikera, nifanyeje?

Pole sina cha kukushauri ila nitakuombea ili hiyo hali iishe ukae kwa amani kwani umeshapewa ushauri mzuri humu.Nilivyosoma majibu yako unaelekea you are very good man.Ongea na mkeo mweleze kinachokukera waziwazi mweleweshe na umwonjeshe mmekua sasa na siyo wakati wakutupiana maneno kama hayo.
Unamjua Mkeo better than anyone in this world ukitoa labda wazazi wake.
 
Mume ni kichwa cha nyumba. Mume asipoimiliki nafasi yake sawasawa kunakuwa na udhaifu wa mahusiano. Chukueni nafasi zenu kama viongozi wa nyumba. Pia msisahau kuwa Mungu amewataka wanawake wawatii waume zao na wanaume wawapende wake zao. Je mnawapenda wake zenu?? Jichunguzeni kwanza ili owte mvumiliane na kuishi kwa upendo.

Kwenye kuwapenda sijui wamaanisha nini?

Nilim-aproach;
Nikatoa mahali;
Nikafunga naye ndoa;
Nikaanza kuishi naye tukiwa tunapanga;
Tumekaa na kushauliaana hadi tukajenga nyumba (sio mojatu);
Usafiri upo; na si kwamba nautumia mimi mara kwa mara;
Kwa ujumla mambo ya nyumbani (matumizi) sio mgogoro hata kidogo;
Ndugu zake wakiwa na matatizo nawasaidia kama kawaida;
Yeye akiwa na shida inakuwa shida yetu wote;
NIMPENDEJE?
 
kukua sio umri kakangu ni uzoefu na busara jinsi ya kuishi na watu!
kwanza pole na yote!ndo ukubwa huo!
nimekuuliza maswali yangu kama sita hizi kwenye post imepita
1.wewe na mkeo mna mawasiliano ya aina gani?
2.unamsikiliza kihisia,yani unaweza kumuelewa hata kabla hajaongea kitu?
3.mkeo anajivunia wewe kuwa mume wake?
4.wewa unafahamu thamani ya ndoa,mke na familia?
5.unatimiza wajibu wako kama mume(hii ni zaidi ya kuwa baba yani kuwa na uwezo wa kuleta watoto duniani)
6.mna nafasi ya kusali na mkeo pamoja?
7.mkeo ana fahamu hili linakukera kiasi gani?ulishawahi kumwambia na kumuonyesha kuwa hupendi?
8.mkeo anajua nafasi yake yeye kama mwanamke kwenye akili yako?
9.wewe unajua mapungufu yako kama mume na kama mwanaume?(hivi ni vitu viwili tofauti)
10.value ndoa yako katika makundi yafutayo
A)NI NZURI NAITHAMINI NA NI MIMI KATIKA UKAMILIFU WANGU
B)YA KAWAIDA NAKUBALI CHANGAMOTO
C)SI MUHIMU NAWEZA KUISHI MWENYEWE
snowhite mhhh haya maswali akiweza kuyajibu atajua umuhimu wa ndoa yake na nini kina kasoro katika ndoa yake
Nimesoma comment nyingi za wachangiaji kwa kweli kuna mu9da sisi wanaume ni chanzo cha ndoa zetu kuenda mrama kwa sababu ambazo ziko ndani ya uwezo wetu au ambazo tunaweza kuzizuia
Ni nadra kwetu kukubali kuwa tuna makosa au kukubali kujishusha
Mwanamke hawezi kunyanyuka from nowhere na kuanza kusema kuwa anarudi kwao bila sababu ambayo ina mshiko kuna mahali mwanaume ameenda mrama na akashindwa kuadmit kosa lake au kwa sababu ya ubabe au kwa sababu tuu ni mwanaume na hawezi kujishusha na kujionyesha kuwa ana makosa
 
Last edited by a moderator:
Kero za ndoa sio kuwa na mahawara tu, inawezekana huna mahawara ila labda
-una kauli mbaya
-una ghubu, kosa la miaka kumi iliyopita utalikumbusha weee
-mchoyo
-mbinafsi
-humjali
-mkorofi
-mbabe
-hushauriki
-una dharau na nyodo
na mengineyo, hivyo jichunguze
nimekubali hoja nimeshuhudia ndoa mbili zikivunjika sababu ya mambo uliyoyataja hapo juu mkuu
 
Mume ni kichwa cha nyumba. Mume asipoimiliki nafasi yake sawasawa kunakuwa na udhaifu wa mahusiano. Chukueni nafasi zenu kama viongozi wa nyumba. Pia msisahau kuwa Mungu amewataka wanawake wawatii waume zao na wanaume wawapende wake zao. Je mnawapenda wake zenu?? Jichunguzeni kwanza ili owte mvumiliane na kuishi kwa upendo.

Mie nadhani kila mmoja ana nafasi sawa kwenye ndoa...kwa maana nyingine kila mmoja ana wajibu wa kutimiza katika ndoa yake. Baba/Mume awajibike kwa familia yake, na mama/mke naye awajibike katika familia yake. Ni kweli, kuwajibika huko kutatofautiana kulingana na uwezo na mazingira na mahitaji ya familia kwa wakati huo.

Mkiendelea na mambo yenu ya eti oooh mume ni kichwa, na nyie ni miguu, mtaishia kufungasha virago kila wakati mnapotishiwa nyau...na mwishowe mnachapa lapa.
 
Ciello hakupenda pesa alimipenda mimi ndio maana akanieleza anachohitaji, ila ndo ivyo watu wachawi wametimia unafiki hata mke kaniacha, nam chukua Baba V, Mtambuzi na ErickB52 hawa ndio chanzo.... Cha kunitenganisha na wife

pole mwaya huwezijua twaweza kutana after life tukaliendeleza ucfe moyo....
 
Pole sina cha kukushauri ila nitakuombea ili hiyo hali iishe ukae kwa amani kwani umeshapewa ushauri mzuri humu.Nilivyosoma majibu yako unaelekea you are very good man.Ongea na mkeo mweleze kinachokukera waziwazi mweleweshe na umwonjeshe mmekua sasa na siyo wakati wakutupiana maneno kama hayo.
Unamjua Mkeo better than anyone in this world ukitoa labda wazazi wake.

Kwa umri wa utambuzi, mimi ndo nimeishi naye miaka mingi zaidi ya m2 yeyote hapa duniani, ninaposema over 10 years yaweza kuwa hata 18/20; nieleweni; mnaonibeza kuwa mi ni mvulana nawashangaa sana tena sana. Just immagine mtoto wetu kwa kwanza yuko Secondary! Nashukuru kwa ushauri wako.
 
Kwenye kuwapenda sijui wamaanisha nini?

Nilim-aproach;
Nikatoa mahali;
Nikafunga naye ndoa;
Nikaanza kuishi naye tukiwa tunapanga;
Tumekaa na kushauliaana hadi tukajenga nyumba (sio mojatu);
Usafiri upo; na si kwamba nautumia mimi mara kwa mara;
Kwa ujumla mambo ya nyumbani (matumizi) sio mgogoro hata kidogo;
Ndugu zake wakiwa na matatizo nawasaidia kama kawaida;
Yeye akiwa na shida inakuwa shida yetu wote;
NIMPENDEJE?
Tutor B hapo ndipo unapofanya kosa kudhani kuwa mwanamke anahitaji hayo tuu usafiri, chakula, mahitaji yake ya kawaida ambayo wanakuambia hata kwao yapo na angeweza kuyapata hata akiwa kwao
Suala kubwa ni ile nyama ya ulimi wenyewe wanasema unaongea nae vipi unamtreat vipi, unamhandle vipi mkeo katika suala zima la upendo na mahitaji yake kama mwanamke, unamlinda, unamjali, sio kimwili zaidi kwenye nguo na mavitu kama hayo ila kiupendo kama mke, unamsikiliza hata kama sometime anaongea mambo yanakukera humkatizi maongezi yake, uko tayari kuwa nae hata mbele ya marafiki zao uko proud kuwa nae yaani ni vitu vidogo vidogo sana ila most important kwake
 
hebu hama hapo!
hiki kiburi chako hiki na jeuri ya pesa rafiki yangu havikufikishi popote!hakuna mwanamke kwanza sio mwanamke tu hakuna mtu yeyote anaweza kuvumilia hili!
we kama unaona hela zako na unayomfanyia mkeo kwa kutumia pesa no ya maana basi
chukua noti zako zooote benki kisha zikunje kunje upate kishimo hivi halafu ulale nazo!
 
Tutor B hebu jichunguze labda una makero yanayopita mipaka
Maana kauli zingine ni ngumu kutoka mdomoni...nashindwa kuelewa kwanini kila mnapogombana akwambie hivo
Inawezekana umejaza vinyumba ndogo na wife anajua
Inawezekana kila siku ukirudi home umelewa tilalila usiku wa manane ..
 
Last edited by a moderator:
Kwa umri wa utambuzi, mimi ndo nimeishi naye miaka mingi zaidi ya m2 yeyote hapa duniani, ninaposema over 10 years yaweza kuwa hata 18/20; nieleweni; mnaonibeza kuwa mi ni mvulana nawashangaa sana tena sana. Just immagine mtoto wetu kwa kwanza yuko Secondary! Nashukuru kwa ushauri wako.
mwanaume wa ukweli ni zaidi ya kuwa na mtoto wa kwanza sekondari
 
Kila tukiwa na mtafaruku na mama watoto wangu ananambia kauli hii "Nitawapisha wengine waje wajaribu, nina kwetu" Hivi mwanamke aliyeolewa, yuko ndani ya ndoa zaidi ya miaka 10 anaweza kuendeleaje kufikiria kurudi kwao badala ya kufikiria kujenga mji wake ambao unaweza kuwa kimbilio kwa jamaa zake wanaoweza kuwa na matatizo?
Akili au matope??????

KAULI HII INANIKERA SANA!

Ni vizuri kumweleza ukweli kuwa lengo lako la kuoana nae ni kuishi pamoja mpaka pale kifo kitakapowatenganisha (au kutenganishwa na uzinzi). Sasa kama objectives zake zimekuwa achieved ni vizuri kumwambia ajisikie huru ashuke kwenye gari safari iendelee.......! Tatizo kubwa ni kuwa wengi huwa wanasema hivyo akijua kuwa kiuhalisia hatua hiyo haitafikia. Kwa hivyo ndugu usichoke kama vile ng'ombe asivyoelemewa na nundu yake.
 
Tutor B hapo ndipo unapofanya kosa kudhani kuwa mwanamke anahitaji hayo tuu usafiri, chakula, mahitaji yake ya kawaida ambayo wanakuambia hata kwao yapo na angeweza kuyapata hata akiwa kwao
Suala kubwa ni ile nyama ya ulimi wenyewe wanasema unaongea nae vipi unamtreat vipi, unamhandle vipi mkeo katika suala zima la upendo na mahitaji yake kama mwanamke, unamlinda, unamjali, sio kimwili zaidi kwenye nguo na mavitu kama hayo ila kiupendo kama mke, unamsikiliza hata kama sometime anaongea mambo yanakukera humkatizi maongezi yake, uko tayari kuwa nae hata mbele ya marafiki zao uko proud kuwa nae yaani ni vitu vidogo vidogo sana ila most important kwake
Ulikuwa wapi m2 wangu? nashukuru sana kwa ushauri wako; ila naamini mengi kati ya uloyataja najituma mkuu.
 
Kwenye kuwapenda sijui wamaanisha nini?

Nilim-aproach;
Nikatoa mahali;
Nikafunga naye ndoa;
Nikaanza kuishi naye tukiwa tunapanga;
Tumekaa na kushauliaana hadi tukajenga nyumba (sio mojatu);
Usafiri upo; na si kwamba nautumia mimi mara kwa mara;
Kwa ujumla mambo ya nyumbani (matumizi) sio mgogoro hata kidogo;
Ndugu zake wakiwa na matatizo nawasaidia kama kawaida;
Yeye akiwa na shida inakuwa shida yetu wote;
NIMPENDEJE?

kauli kaka kauli......

Hata mkijenga maghorofa kama kauli mbaya na ndoa pia huwa mbaya....

Hata ukisaidia ukoo wake wote, kama lugha mbaya na nk niliyoyaorodhesha hapo juu bado ndo itakua na migongano
 
Tutor B hebu jichunguze labda una makero yanayopita mipaka
Maana kauli zingine ni ngumu kutoka mdomoni...nashindwa kuelewa kwanini kila mnapogombana akwambie hivo
Inawezekana umejaza vinyumba ndogo na wife anajua
Inawezekana kila siku ukirudi home umelewa tilalila usiku wa manane ..
FirstLady1 huyu hana hawara wala sijui pombe labda!tatizo lake KIBRI!MWANAUME ANARINGA NA KUJISIKIA KA HAENDI CHOO HUYU!KHA!
 
Last edited by a moderator:
Ni vizuri kumweleza ukweli kuwa lengo lako la kuoana nae ni kuishi pamoja mpaka pale kifo kitakapowatenganisha (au kutenganishwa na uzinzi). Sasa kama objectives zake zimekuwa achieved ni vizuri kumwambia ajisikie huru ashuke kwenye gari safari iendelee.......! Tatizo kubwa ni kuwa wengi huwa wanasema hivyo akijua kuwa kiuhalisia hatua hiyo haitafikia. Kwa hivyo ndugu usichoke kama vile ng'ombe asivyoelemewa na nundu yake.

Jina kama maneno yanayonikera (Kwetu ni kwetu) jokes m2 wangu;
nashukuru kwa ushauri wako.
 
Back
Top Bottom