Kauli hii inanikera, nifanyeje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli hii inanikera, nifanyeje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tutor B, Oct 30, 2012.

 1. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Kila tukiwa na mtafaruku na mama watoto wangu ananambia kauli hii "Nitawapisha wengine waje wajaribu, nina kwetu" Hivi mwanamke aliyeolewa, yuko ndani ya ndoa zaidi ya miaka 10 anaweza kuendeleaje kufikiria kurudi kwao badala ya kufikiria kujenga mji wake ambao unaweza kuwa kimbilio kwa jamaa zake wanaoweza kuwa na matatizo?
  Akili au matope??????

  KAULI HII INANIKERA SANA!
   
 2. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Inategemea mnagombana kwa ajili ya kitu gani,kama kuna tishio la wanawake wengine kwake unataka aseme nini ili akuzime ili maisha yenu yaendelee?

  Mwanamke siku zote fimbo yake ni mdomo hivyo kama unakereka na kauli kama hizo basi mtendee yaliyo mema na yasiyomtishia ndoa yake.
   
 3. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,319
  Likes Received: 2,605
  Trophy Points: 280
  Jaribu kuweka na kiini cha ugomvi, pengine wewe ukawa ndio chanzo cha kila kasheshe kiasi mwanamke kaona yanaelekea kumshinda.
   
 4. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Kama yapi Jose?
  Ameolewa kwa ndoa ya kanisani;
  Tumejaliwa watoto tena kwa kuchanganya jinsia;
  Anaishi kwake;
  Sina hawala;
  Nifanyeje ndugu yangu!
   
 5. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Kwa wanandoa chokochoko za hapa na pale huwa hazikosi; huwa ni kuheshimiana tu ndo amani inakuwemo ndani.
   
 6. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mambo ya ndoa hayanaga ushauri! Maanza hazifanani, chukua mdomo wake, changanya na actions zako, utapata majibu!
   
 7. Raimundo

  Raimundo JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 13,552
  Likes Received: 10,940
  Trophy Points: 280
  Kama hizi ndio lugha zako za kumwongela mkeo unategemea nini? Hivi kweli mke unayempenda kwa dhati hata akikosea unaweza kuwaambia watu kwamba akili zake ni matope! Kweli? Huna heshima kwa mke wako, labda una unao waheshimu ndio maana anataka kuwapisha wenye akili nzuri.

  Jifanyie assessment ya jinsi gani ambavyo huwa unahandle huo mtafaruku, kamwombe samahani kwamba umemtukana kwenye mhadhara wa watu wa JF na kwingine kote utakakokuwa umewahi kuyatamka haya.

  Kifupi: Jichunguze, umenikera kweli kweli! Hivi wanaume wa siku hizi tukoje? Inaonekana hata siri zake zingine unatangazaga wewe, ndio maana anaona unamdharau wazi wazi!

  Akikosea mwabie, haya ulitakiwa umwambia yeye, sasa unatuambia sisi tukamwambie au?
   
 8. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kuna mengi katika maisha ya ndoa zaidi ya watoto, haijalishi ni ndoa ya kanisani au msikitini,kama huna hawala ila mazingira yote yanayokuzunguka yanaonesha hivyo unategemea nini toka kwa mwenza wako?

  Maisha ya ndoa ni magumu sana hasa kwa vile nyie mmekutana huku mkiwa mmelelewa katika mazingira tofauti hivyo kuoneshana tabia tofauti ni jambo la kawaida na yafaa ukawa mvumilivu kwa mwenzio,na kama unaona hukosei basi kaa nae chini na zungumza nae jambi hili na mtafikia muafaka maana kwangu mimi si rahisi mwanamke kukwambia ana kwao na kusiwe na sababu inayomfanya aseme maneno hayo.
   
 9. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Action kama zipi ndg yangu?
   
 10. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  Joseph na Kanigini hamjui tu vile mmenipa amani na ushauri wenu!yani full mwanaume aliye na busara!
  mi hata siongezi!nahisi ntaharibu mapwenti
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Unajua kimya kingi mshindo wake mkari;
  Si kwamba kauli hizo namwambia yeye wala m2 mwingine. Mimi binafsi huwa napenda mambo yanayohusu ndoa tuyamalize sisi wenyewe; ila yeye hupendelea kuwahusisha wa2 wa kwao na kutishia kuondoka kurudi nyumbani kwao. Sasa kwa kuwa muda umeenda na umri ndo hivyo umeenda; nimeona niwauliwe wanaJF ili nipate ushauri.

  Kama nimekuudhi nisamehe ndg yangu!
   
 12. smallvile

  smallvile JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 12, 2012
  Messages: 497
  Likes Received: 171
  Trophy Points: 60
  inakera kweli, sasa huyu mwananke ana matatizo, kwanza yawezekana anasema hivo kukutisha unajua tena wanawake akili zao ndogo saana, pili yawezekana ni mambo ambayo aliyazoea kuyasema bila kumaanisha, au background ya familia yake wazazi walikua wanatishana mbele ya watoto mambo kama hayo, ila kama hana makosa makubwa ya kumwacha, mpende mtimizie ilyo haki yake, nadhani mtaelewana kwani kupishana kimawazao katika familia ya wawili mbona kawaida, mwanaume pia unakosea, ila maana na msingi kusaeheana wongo jombaaaaaa
   
 13. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Zaidi ya miaka 10 unafikiri sijawahi kuzungumza naye tukiwa wawili? Ila washwahili wanasema tabia haina dawa! Kumvumilia ni kumfanya atoe mapembe na kuendekeza dharau ya kunitishia mara kwa mara akijua wazi kuwa sina mpango wa kuwa na mwanamke mwingine hata kama ikitokea tukatengana kwa sababu yoyote ile.

  Tatizo kubwa ni namna anavyodekezwa na ndugu zake + wazazi wake!
   
 14. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,319
  Likes Received: 2,605
  Trophy Points: 280
  Basi jaribu kukaa na huyo mwenzi wako akueleze nini haswa huwa kinamkera toka kwako....pengine huwa hamna wasaa wa kurekebishana pale mnapokoseana zaidi ya kutumia maneno ya hasira na kejeli...
   
 15. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Ahsante kwa ushauri mkuu, ila kauli hiyo inakera sana!
   
 16. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,507
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ndugu yangu akili za wanawake wengi kama sio 98% walioolewa huwa ni kurudi nyumbani tu.....ukikuta wachache wanaojiweza huwa wanakaa na familia zao na wako confident hata wakiachika watakaa wenyewe bila kurudi nyumbani.....
   
 17. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Fikiria kesi ndogo kama hii;
  Amechelewa kurudi nyumbani; anakukuta uko nje; unamuuliza mbona umechelewa hivi ulikuwa wapi?
  Jibu; Eh! Baba fulani nisiongee ma marafiki zangu eti kisa nitaulizwa? kama ni hivyo ni bora nikupishe waje wengine wajaribu!

  Utajisikiaje kwa jibu la namna hiyo??? Inakera!
   
 18. M

  Mundu JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Wakwangu huwa anasema..."hapa siondoki ng'o..."

  Huwa ananiambia "kama kuondoka niondoke mie"

  Huyo wa kwako Tutor B yupo poa kabisa hahaha

  Anyway, wanawake/wake zetu mara nyingi wanajifikiria kuwa wapo insecure...sijui kwa nini?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. smallvile

  smallvile JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 12, 2012
  Messages: 497
  Likes Received: 171
  Trophy Points: 60
  ni kweli wala hakuna anayepinga mwanawane
   
 20. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Mkuu;
  Hawajui kuwa huko nyumbani kuna Mwanamke aliyeheshimu mumewe ndo maana hiyo nyumba inadumu hadi sasa?

  Na kwa nini sisi wanaume huwa hatuwazi kurudi majumbani kwetu wakati wa migogoro?

  Je! Hawajui kuwa familia inaundwa na baba, mama na watoto? Iweje mwanamke awe na mawazo ya kurudi kwao kuiterekeza familia yake? Hapo ndo najiuliza hadi wengine wananishangaa kwa kutumia maneno makali JF!
   
Loading...