Katoliki ni zaidi ya uijuavyo!

Katoliki ni zaidi ya uijuavyo!

Nimesoma hii thread leo hii nikiwa huku Kigali tena eneo hili la kanisa tajwa ambako inadaiwa kanisa lilihusika katika kuwaangamiza wahanga kipindi kile cha mauaji ya 1994.
 

Attachments

  • IMG_20171009_103356.jpg
    IMG_20171009_103356.jpg
    318.4 KB · Views: 33
Na nyingine hii.
 

Attachments

  • IMG_20171009_110640.jpg
    IMG_20171009_110640.jpg
    149.6 KB · Views: 33
Nyongeza nyingine ya kanisa husika.
 

Attachments

  • IMG_20171009_103908.jpg
    IMG_20171009_103908.jpg
    343.8 KB · Views: 34
Ukiwa na mda jaribu kutafuta ujue ushiriki wa kanisa katoliki na papa kwenye vita kuu ya dunia ya pili tena kanisa ndo lililompa nguvu kabisa Musolini kufanya uchaf wake akishirikiana na Hittler
Mii nimepata hii
f97610f7fa633b1a94f427a0c1a782e3.jpg
 
Bible only? Hiyo inaitwa sola scriptura, ni doctrine ya kujitungia, ambayo pia ni unbiblical, bibilia haisemi hivyo. Aaarrrghhh Protestants! When will u come home?
Yes Bible only. I repeat Bible only. Ninasababu nyingi ya kutumia Biblia pekee kwasababu Biblia pekee imejitosheleza. Soma ufunuo 22:18-19.Kama wewe huiamini utakuja kuamini sooner or later and I hope it won't be too late for you to repent
 
Acha basi na wewe kulinganisha papa na habari zingine za ajabu,pls
niwie radhi ndg...nilikuwa najarabu kumuelewesha jamaa aliyekuwa anadharau nguvu na mamlaka ya kanisa katoliki duniani.
 
niwie radhi ndg...nilikuwa najarabu kumuelewesha jamaa aliyekuwa anadharau nguvu na mamlaka ya kanisa katoliki duniani.
Hahaha,jamaa analinganisha Katoliki na kitawi cha Katoliki alipo!
 
Mlicho andika nyinyi ni misale na sheria zenu za kikatoliki. Ndiyo maana kila juma pili mnafuata muongozo wa misale hamna muda wa kuichambua biblia takatifu
Kwaiyo wewe unachambua biblia, unachambua ili iweje
 
Sema tulichopinga Ata kimoja hapa Nikufafanulie
Mojawapo ni hili

Kuiabudu sanamu na kuiomba wakati haisikii, haioni, haipumui, haitembei. Mnazitengeneza wenyewe halafu mnaziabudu. Eti hata wasomi, maprofesa pamoja na elimu zao, hata wengine ni maraisi, hawaoni kuwa siyo sawa kumfananisha Mungu aliye mkuu sana kumfananisha na sanamu iliyochongwa na mwanadamu tu. Hawaoni kuwa Mungu yupo mahali popote na Yesu hayupo msalabani tena maana alikufa akazikwa akafufuka na kupaa mbinguni. Kwanini mnamhuzunisha Bwana kwa kukataa na kupinga ufufuko wake?
 
Kwaiyo wewe unachambua biblia, unachambua ili iweje
Swali zuri sana.
Tunapochambua Biblia tunasoma na kufahamu ni nini mapenzi ya Mungu. Pia tunafahamu namna shetani anavyodanganya ulimwengu ili siku ya mwisho asitupwe pekeyake motoni. Na pia tunafahamu jinsi ya kumshinda shetani ili tuweze kumwona Mungu mbinguni.
 
Swali zuri sana.
Tunapochambua Biblia tunasoma na kufahamu ni nini mapenzi ya Mungu. Pia tunafahamu namna shetani anavyodanganya ulimwengu ili siku ya mwisho asitupwe pekeyake motoni. Na pia tunafahamu jinsi ya kumshinda shetani ili tuweze kumwona Mungu mbinguni.
Basi nisaidie sehemu kwenye biblia ambayo inasema tuichambue ili na mm nianze kuichambua, maana kwa saivi naisoma pale ninapohitaji na kuitafakari na siyo kuchambua
 
Mlicho andika nyinyi ni misale na sheria zenu za kikatoliki. Ndiyo maana kila juma pili mnafuata muongozo wa misale hamna muda wa kuichambua biblia takatifu
Kwa hili naona nikuambie wazi tuu kuwa unahitaji kueleimishwa usifuate wachungaji wa bei rahisi wanaoona kuwa ni rahisi kupora waumini kwa kanisa lingine kuliko dini nyingine. Misale msii haramishe hivyo.Kwa taaarifa yako misale ni km Syllabus. Kwanza makanisha yote yanakwenda na topiki siku hiyo.Na wakienda hadi mwisho wanakuwa wamesoma Biblia yote bila kurudia .Makanisa mengine ni rahisi mchungaji kujisome aapendapo, na ukaenda kanisa lingine jumapili kadhaa ukakuta kasoma apendapo na ni pale pale ulipotoka. wengine wanaruka ruka kwa kuchukua misatari hapa na pela na pale.Mwisho wa mwaka sio rahisi kwa waumini wasiojua kusoma ,vyema wajue wapi hawajasoma.

MIsale ina somo moja la Injili na vipande viwili vya sehemu nyingine ya Biblia kila siku.Kwa hiyo ukihama kanisa ,na kuenda kwingine siku inayofuata unakuta muendelezo wa ule ule.
 
Upo hapa Kigali?Basi,fanya uje hapa Simba supermarket,Kicuciro tupige story ndg yangu!
Kumbe! Kuna muda nilikuwa hapo Simba Supermarket, then nikaenda kutafuta kuku choma pale Camellia Restaurant jirani na KCB bank haikuwepo ikabidi kwenda Green Corner (Nyamirambo) na sasa narudi hotelini kupumzika.
 
Kumbe! Kuna muda nilikuwa hapo Simba Supermarket, then nikaenda kutafuta kuku choma pale Camellian (?) Restaurant jirani na KCB bank haikuwepo ikabidi kwenda Green Corner (Nyamirambo) na sasa narudi hotelini kupumzika.
Karibu Kigali!Binafsi nipo hapa pale Kanombe.....ukiwauliza wenyejiyo,watakufahamisha.
 
Kama Biblia ni kitabu au mali ya wakatoliki mbona mnayapinga yaliyomo ndani yake??
Tunapinga?? Biblia ipo ku-suit nafundisho ya kanisa Katoliki kwa taarifa yako....Na hakuna kanisa nasisitiza hakuna kanisa linalofuata Biblia kama ilivyo kama Kanisa Katoliki...

Biblia si kitabu chenu wala hamjakiandika nyinyi. Usidanganye watu bwana
Biblia haijaandikwa....ila Biblia ni Mkusanyiko wa vitabu na nyaraka mbalimbali...Nyaraka hizo na vitabu vilikusanywa na kuwekwa pamoja(Canon) na Kanisa Moja Takatifu Katoliki la Mitume....

Kama Nadanganya tuambie ni watu gani walihusika na kuiweka biblia , utupe na mwaka ambao biblia ilikamilika.....

Kumbuka mpaka kufikia karne ya 16 kulikuwa na Kanisa Moja tuu duniani(Hilo ndilo kanisa Katoliki) takataka zingine zimeibuka baada ya muasi Martin Luther
 
Back
Top Bottom