Katika kudai Katiba Mpya, tuwe na Katiba Day kila mwaka na iwe ile tarehe ambayo Mzee Warioba aliwasilisha maoni ya Wananchi juu ya Katiba Mpya

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Habari Wakuu,

Katika harakati za kudai Katiba Mpya kutoka kwa watawala, napendekeza moja ya mkakati ni tuwe na siku maalumu ya kitaifa kila mwaka ambapo tutaitumia siku hiyo kutoa elimu kwa umma juu umuhimu wa Katiba Mpya na kuhamasisha madai ya kutaka Katiba Mpya.

Siku hiyo ikifika kila mwaka, wanasiasa, wanaharakati na wananchi kwa ujumla wanafanya makongamano na mikutano nchi nzima kwa lengo la kukumbusha madai ya kupatikana kwa Katiba Mpya.

Pia,, kila mwaka katika siku hiyo, tuwe na kauli mbiu itayotumika kuchagiza madai hayo ya katiba Mpya na ninapendeleza siku ile ambayo Mzee Warioba aliwassilisha maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya ndio iteuliwe kuwa ni siku ya kitaifa ya kila mwaka ya kuadhimisha na kuhimiza madai ya Katiba Mpya.

Ikiwezekana tuanze mwakani na kauli mbiu iwe: Bila Katiba Mpya, huwezi jenga uchumi imara na endelevu.
 
Kuita Siku yakitaifa umefeli.Kitaifa wakati haina uhalali wakisheria
Tafuta jina maalum lakuwavuta wapigania katiba
 
Unasubiri CCM wakupe uhalali wa jambo linalohatarisha wao kuendelea kubaki madarakani! Are you serious?
 
Hiyo katiba inadaiwa na majuha, hakuna mwenye akili timamu anataka katiba
Kukosekana kwa katiba nzuri kumekukosesha haki ya kupata elimu nzuri ambayo ingekufanya, hata majukwaa kama haya uchangie kama mtu mwenye akili timamu.

Ili angalao wanao wawe raia wenye akili timamu, na siyo kama wewe Baba yao, ni vema ukapigania katiba mpya nzuri yenye kuwahakikisha haki yao ya kupata elimu nzuri.
 
Ni muhimu pia Asasi za kiraia zikashiriki ktk kutoa elimu juu ya umuhimu wa katiba mpya. Hii itasaidia jambo hili liwe na sura ya kitaifa kuliko kutegemea nguvu kutoka kwa vyama vya siasa (upinzani)

Sent from my vivo 1820 using JamiiForums mobile app
 
Kukosekana kwa katiba nzuri kumekukosesha haki ya kupata elimu nzuri ambayo ingekufanya, hata majukwaa kama haya uchangie kama mtu mwenye akili timamu.

Ili angalao wanao wawe raia wenye akili timamu, na siyo kama wewe Baba yao, ni vema ukapigania katiba mpya nzuri yenye kuwahakikisha haki yao ya kupata elimu nzuri.
Wewe akili uipate wapi? Hudumia mumeo vizuri
 
Mimi napendekeza iwe siku ambayo Akwilina Akwilini aliyouawa......maana kuuawa kwake ni matokeo ya katiba mbovu...
 
Habari Wakuu,

Katika harakati za kudai Katiba Mpya kutoka kwa watawala, napendekeza moja ya mkakati ni tuwe na siku maalumu ya kitaifa kila mwaka ambapo tutaitumia siku hiyo kutoa elimu kwa umma juu umuhimu wa Katiba Mpya na kuhamasisha madai ya kutaka Katiba Mpya.

Siku hiyo ikifika kila mwaka, wanasiasa, wanaharakati na wananchi kwa ujumla wanafanya makongamano na mikutano nchi nzima kwa lengo la kukumbusha madai ya kupatikana kwa Katiba Mpya.

Pia,, kila mwaka katika siku hiyo, tuwe na kauli mbiu itayotumika kuchagiza madai hayo ya katiba Mpya na ninapendeleza siku ile ambayo Mzee Warioba aliwassilisha maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya ndio iteuliwe kuwa ni siku ya kitaifa ya kila mwaka ya kuadhimisha na kuhimiza madai ya Katiba Mpya.

Ikiwezekana tuanze mwakani na kauli mbiu iwe: Bila Katiba Mpya, huwezi jenga uchumi imara na endelevu.
Rubbish.
 
Back
Top Bottom