Katika kosa ambalo hutakiwi kufanya kama Baba ni Kuogopa Mtoto wako Kupewa Sumu na Mwanamke. Toto jingajinga Fukuza. Usibabaishwe wapuuzi wasiokutii

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,059
Reaction score
79,412
KATIKA KOSA AMBALO HUTAKIWI KUFANYA KAMA BABA NI KUOGOPA MTOTO WAKO KUPEWA SUMU NA MWANAMKE. TOTO JINGAJINGA FUKUZA. USIBABAISHWE WAPUUZI WASIOKUTII

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli!

Wewe ni Mwanaume, sasa ni Baba. Usiwe dhaifu kiasi cha kufanya vitu ili kutafuta validation kuwa wewe ni Baba Bora au wewe ni mwanaume wa shoka. Huo ni utumwa na huo sio uanaume. Na hustahili kuitwa Baba.

Baba au Mwanaume halisi hafanyi mambo kuthibitisha uanaume au ubaba wake. Huko ni kutokujiamini na kama utakuwa mtu WA hivyo wewe ni mwanamke mwenye cover ya kiume.

Usifanye Jambo ili watoto wakuone wewe ni Baba Bora. Nope!
Usifanye mambo Ili mkeo akuone wewe ni mume Bora. Nope!

Mwanaume na Baba hufanya Mambo kwa sababu kuu zifuatazo;
1. Matakwa na Mapenzi yake.
Baba au Mwanaume unatakiwa ufanye mambo kwa sababu ni matakwa na mapenzi yako kufanya hivyo.
Mwanaume lazima uwe na Matakwa yako. Na matakwa yako yanatokana na Sheria zako, miiko yako, heshima na hadhi yako, na Mamlaka yako Kama Baba au Mwanaume.
Hii ndio tunaita Mwanaume ni kichwa.

2. Maslahi na Malengo yake.
Mwanaume na Baba hufanya mambo kwa kujali Kwanza maslahi yake.
Mwanaume lazima upate maslahi tangible (maslahi yanayoonekana) kuliko maslahi yasiyoonekana.
Mfano; Mwanamke asije akakusifia tuu wewe ni mwanaume kweli alafu wewe sifa hizo ambazo sio tangible ukatoa pesa au mali ambayo ni tangible.

Baba au Mwanaume hata akihonga, huwezi mhonga mwanamke kisa uzuri wake ukamhonga gari au nyumba, huo ni ukosefu wa Akili. Ila kama mwanamke huyo kakupa kitu tangible kama amekuzalia m/watoto hapo unaweza kumpa Mali. Huyo ni Mwanaume. Yaani kichwa(akili zinachaji).

Unaposikia wanawake wakisema Yule Kalogwa wanamaanisha ni mwanaume ambaye kichwa hakifanyi KAZI. Mwanaume asiyejali maslahi yake. Kwa sababu Mwanaume kamili lazima ajali maslahi yake kuliko ya mtu yeyote.

3. Heshima yake
Mwanaume au Baba wewe ni Kama serikali. Kama Rais au Mfalme. Heshima ni kuongoza sio kuongozwa. Heshima ya mwanaume ni kufanya vile atakavyo.

Turudi kwenye hoja yetu!

Unapoingia kwenye Ndoa lazima uyajue haya kama Mwanaume, Baba au Baba mtarajiwa; elewa saikolojia hii ya wanawake;
1. Mkeo hutegemea uzuri kama silaha ya kukuchapia na kukujaribu.
Onyesha kuwa wewe unaweza kupata wanawake wazuri kuachana naye. Onyesha kuwa wewe kumchagua yeye sio kwamba hakuna wengine. Isipokuwa ni umempa nafasi na kwake aihesabu kama bahati. Na ajue yakuwa Muda wowote akienda kinyume na matakwa yako utaleta chuma kingine, kibichi(kwani yeye atakuwa ameshazeeka, kawa mkubwa).
Onyesha kuwa wewe ni mwanaume mwenye standards zenye hadhi na sio wale wanaume wanaojiokoteaokotea vitu hovyohovyo.
Ukiwa hivyo hana uwezo wa kukupangia mechi, sijui kukupimia, huo uwezo hana. Na hawezi kuthubutu kuwaza achilia mbali kukuambia.
Onyesha kuwa kuachana naye haitakuumiza kwa sababu hatakupunguzia chochote, zaidi itakula kwake na utakuwa kuvuja kwa pakacha nafuu kwako mchukuzi, utaenda kuchukua Mali mbichi, ndogo kiumri na pisikali New version.
Mwanaume ukiwa Mwanaume hauna hasara. Wewe ni kama Serikali.

2. Atatumia Watoto Kama Fimbo.
Mwanamke kamwe asikufundishe Kumpenda yeye. Pili, asikufundishe kuwapenda Watoto wako.
Mwanaume kamili hafundishwi kupenda. Kwa sababu uanaume ni upendo.

Mwanamke akishaanza kukupa maelekezo ya namna ya kumpenda yeye mwambie wewe ni Mwanaume hufundishwi kupenda. Huko ni kukupanda kichwani. Lakini pia ni dalili ya kukulinganisha na wanaume wengine. Jambo ambalo halikubaliki kwa sisi wanaume wa kitibeli.

Mwanamke akianza kukupa maelekezo ya jinsi ya kuwapenda watoto wako hiyo ni red flag. Hiyo ndio sumu yenyewe.
Kamwe usifuata mafundisho yake. F
Hakuna mwanaume asiyewapenda watoto wake aliowazaa.
Unahudumia watoto wako kutokana na sababu zifuatazo zilizondani ya Upendo kama Baba;
1. Uwezo
Wanaume wote wanapenda watoto wao waishi maisha mazuri. Wasome sehemu nzuri, wakae pazuri. Lakini hufanya kwa uwezo. Mwanamke hawezi kumshinda Mwanaume kwa upendo dunia iende irudi. Ndio maana tunawapenda na kuwatunza Wap(wake zetu) na watoto wetu.

2. Heshima ya Mwanamke kwa Mwanaume.
Kadiri mwanamke anapokuwa na heshima Kwa mwanaume ndivyo mwanaume anavyozidisha utafutaji na huduma kwa mke na watoto.
Ndio maana mchepuko anaweza kupewa huduma zaidi na mwanaume ikiwa anaheshima kuliko mke wa ndani mwenye kiburi.

Heshima kwa mwanaume inathamani kubwa kulilo umzalie vitoto elf vikaidi na wewe uwe na Kiburi.

Wapo wanaume wanatunza watoto wakambo kuliko watoto wao kisa mitoto yao ni mijeuri na haina adabu.

Mwanamke aliyekuzalia akianza kuonyesha tabia zisizoeleweka, na ukaona anawaambia watoto maneno ya Sumu, kamwe usiogope wala usitake kuthibitisha kuwa wewe ni Baba Bora na maneno ya Mama yao ni uongo. Never ever!

Akianza kufanya hayo, thibitisha Yale anayoyasema, kuwa wewe kweli ni mshenzi,
Akisema huhudumii Acha kuhudumia.
Akisema haujali Acha kujali.
Akisema humpendi, Acha kumpenda.

Haiwezekani utoe huduma alafu mtu aseme hauhudumii alafu wewe unaendelea kuhudumia, wanaume hawafanyi hivyo.

Mwambie awaambie chochote hao watoto wake anachotaka kuwaambia.
Na watoto wakija kukuuliza, waambie wao wanaonaje, wakisema ni sahihi waambie ni sahihi. Wakisema hawajui waambie wakikua watajua, bado wadogo. Wakisema mama Yao ni mwongo usiwajibu ila kuwa nao karibu wape haki zao kama Baba.

Usiendeshwe!

Sabato Njema!
Acha nipumzike!

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es Salaam
 
Absolutely right. Baba wa kweli haogopi drama,,, better a heartbroken son than a poisoned legacy. Ukiona toto lichafu akili, delete and protect the bloodline.
 
Mtoto kujazwa unaoita ujinga, ni taswira tosha ya kuonesha baba hayuko katika mambo ya familia. Hivyo ana hali ya kuwa katika hali hiyo, kwani hashiriki katika malezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…