Katika hili, namwamini Shetani

Katika hili, namwamini Shetani

Kwanza kabisa nimshukuru Mungu kwa huruma na neema yake kwa kunifanya mpaka dakika hii naendelea kupumua na kuwa mzima wa afya. Pia kwa mamlaka aliyotupa viumbe wake ya kutawala samaki wa Baharini na ndege wa angani , wanyama na kwa kutuumba kwa mfano wake. MWANZO1:26. Hakika huu ni upendo wa ajabu sana , sifa na utukufu viende kwake.

Mungu huwa hadanganyi kama tunavyojua, lakini kwa nini alimdanganya adam na hawa kuhusu mti wa Tunda la kati kati? , aliwaambia adam na hawa kuwa wakila matunda wa mti wa katikati hakika watakufa. Mwanzo 3:3 " lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema msiyale, msije mkafa.

Kabla ya hapo tukumbuke nyoka alimwambia mwanamke kuwa hatakufa akila mti wa tunda hilo bali watafunguliwa macho yao Na watakua kama Mungu watajua mema na Mabaya .
Mwanzo 3:4 "Nyoka akamwambia mwanadamu hakika hamtakufa. 5. Kwa maana Mungu anajua kwamba, siku mtakapokula matunda ya mti huo, mtafunguliwa macho , nanyi mtakua kama Mungu mtajua mema na mabaya.

Na ni kweli walipokula lile tunda hawakufa kama Mungu alivyosema, kwa hiyo tunaona Mungu alidanganya na shetani aliwaambia kweli kwani walipokula tu hilo tunda wakajua mema na mabaya.kama shetani alivyowaambia.

Mwanzo 3:7 wakafunguliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wako uchi.

Mwanzo 3:22 " Bwana Mungu akasema , basi huyu mtu amekua Kama mmoja wetu , kwa kujua mema na mabaya, na Sasa asije kunyoosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima akala akaishi milele.

Kama Mungu alituumba kwa mfano wake, kwa nini alikua hataki tujue mwema na mabaya? , na kwa nini alikua hataki tutwae mti wa uzima tuishi milele? , alitudanganya alipotuabia katuumba kwa mfano wake? , hapa hatuoni kuwa shetani ni mwema na ananitutakia mema Kwani baada tu ya kula lile tunda akina hawa wakapata fahamu na kujua mema na mabaya kama shetani alivyowaambia?

Kwa nini wanadamu tumekua tishio kwake baada ya kula mti wa ufahamu na kuamua kutupa laana ya kifo?

Mwanzo 6:3 " bwana akasema, roho yangu haitakaa kushindana na mwanadamu milele, Kwa kuwa yeye ni nyama, basi siku zake zitakua miaka Mia na ishirini"

Mmeona Mungu alivyotugeuka? Hataki tufanane nae Tena kama alivyosema, na kaamua kutupa ukomo wa miaka ya kuishi duniani

Hakika wewe ni Mungu , hakuna wa kushindana na wewe .

Sent from my iPhone using JamiiForums

Hawakufa papo kwa papo. They were bound not to die and they would eternally live in case they would not eat the fruits of the forbidden tree. However, they were eventually bound to die after eating the fruits. Yatafakari vizuri haya maneno niliyoyabold!
 
Ngoja niweke kambi hapa ila nna uhakika huu uzi utabadilika na kua uzi wa kushindania ipi dini halali ya zile mbili zinazofanana ila zina uadui mkubwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app

Walikufa kiroho?

Wewe umejulia wapi?

Sio kwamba unatafsiri ili ku-fit your narrative?

Inaitwa cherry picking!

Yaani unachagua kutafsiri hiki unaacha kile sababu tu haki-fit your narrative!

Christians,christians,christians....you will never cease to make me wonder how chameleons have to copy your better chameleons ways!
 
..za....Zee::z...3:z.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Alitoa adhabu ya kifo baadae, lile tunda liliwapa ufahamu kama shetan alivyosema, Adhabu ya kifo alitoa Mungu baada ya kuogopa wana damu mana walikua na ufahamu kama yeye, akaogopa watakula matunda ya mti wa uzima waishi nilele akawafukuza bustanini'

Sent from my iPhone using JamiiForums
MUNGU amwogope mwanadamu??are you serious??
Naona umeamua kumwongelea aisee
 
Tunda lilikuwa jaribio la uaminifu kwa adam kwa Mungu.kumbuka Mungu alimwumba lucifa na alikuwa malaika wa sifa,akamgeuka Mungu akataka kuinyanyua kiti chake juu kuliko mwenye enzi.ndpo alipotupwa chini.Ili hayo yasitokee ndpo alipompa adamu kipimo.
adamu aliambiwa hakika utakufa na ndvyo ilivyo baada ya kula tunda umelele ukaondolewa kwake.bali mpango wa kumkomboa pia uliandaliwa.john 3;14.

kumbuka hi ndyo sayari pekee iliyodanganywa na shetani,huko kwngne walimkataa.ufunuo 7;13-17.
 
Kwa MUNGU miaka elfu moja ni sawa na sekunde tu, na sekunde moja ni sawa na miaka 1000 kwetu uwezekano wa kuwa walikufa pale pale ni mkubwa tu
 
ulimi waupanga

" Nafikiri kosa la Shetani siyo kumdanganya Eve/Hawa bali ni KUFICHUA SIRI ZA MUNGU KWA MWANADAMU. Jiulize kama kweli Adamu alikuwa na maisha ya milele kwanini Mungu apande mti wa Uzima? Apa inaonesha Adamu alipungukiwa vitu viwili ili awe kama Mungu, kwanza ni MAARIFA( Ujuzi wa mema na mabaya) pili ni MAISHA YA MILELE. "
.....................................................

Quoted

Hapana Adamu hakupungukiwa viwili tu, ili afanane na Mungu,
Kuna vitu vingi sana, kama vile

OMNIPRESENCE, yaani Uweza wa kuwa mahali pote, kwa wakati wote.

OMNIPOTENCE, yaani uwezo wa kutenda maajabu kama kuuzuia moto usiwale Shadrach, Meshach na Abernego,
Uweza wa uumbaji NK,

OMNISCIENCE, yaani uwezo wa akili, uelewa, ujuzi, utambuzi, kufikiri na kubuni mambo kwa umahili mkuu sana.

OMNIUNKNOWN, yaani uweza wa mambo ambayo sisi Binadamu, Malaika, na Shetani hatuyafahamu hadi hii leo.
Na uweza huu upo mwingi kuliko huo tunaoujua

Sisi Binadamu hatufahamu hata siku ya Kiama itakuwa lini, wala hatuelewi tutakuwa ktk maumbo gani baada ya kuuacha mwili wetu makaburini, na pia huko Mbinguni kukoje nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tatizo la bible ni aya kupinga aya nyingine huenda inatokana na editing
 
Kwanza kabisa nimshukuru Mungu kwa huruma na neema yake kwa kunifanya mpaka dakika hii naendelea kupumua na kuwa mzima wa afya. Pia kwa mamlaka aliyotupa viumbe wake ya kutawala samaki wa Baharini na ndege wa angani , wanyama na kwa kutuumba kwa mfano wake. MWANZO1:26. Hakika huu ni upendo wa ajabu sana , sifa na utukufu viende kwake.

Mungu huwa hadanganyi kama tunavyojua, lakini kwa nini alimdanganya adam na hawa kuhusu mti wa Tunda la kati kati? , aliwaambia adam na hawa kuwa wakila matunda wa mti wa katikati hakika watakufa. Mwanzo 3:3 " lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema msiyale, msije mkafa.

Kabla ya hapo tukumbuke nyoka alimwambia mwanamke kuwa hatakufa akila mti wa tunda hilo bali watafunguliwa macho yao Na watakua kama Mungu watajua mema na Mabaya .
Mwanzo 3:4 "Nyoka akamwambia mwanadamu hakika hamtakufa. 5. Kwa maana Mungu anajua kwamba, siku mtakapokula matunda ya mti huo, mtafunguliwa macho , nanyi mtakua kama Mungu mtajua mema na mabaya.

Na ni kweli walipokula lile tunda hawakufa kama Mungu alivyosema, kwa hiyo tunaona Mungu alidanganya na shetani aliwaambia kweli kwani walipokula tu hilo tunda wakajua mema na mabaya.kama shetani alivyowaambia.

Mwanzo 3:7 wakafunguliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wako uchi.

Mwanzo 3:22 " Bwana Mungu akasema , basi huyu mtu amekua Kama mmoja wetu , kwa kujua mema na mabaya, na Sasa asije kunyoosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima akala akaishi milele.

Kama Mungu alituumba kwa mfano wake, kwa nini alikua hataki tujue mwema na mabaya? , na kwa nini alikua hataki tutwae mti wa uzima tuishi milele? , alitudanganya alipotuabia katuumba kwa mfano wake? , hapa hatuoni kuwa shetani ni mwema na ananitutakia mema Kwani baada tu ya kula lile tunda akina hawa wakapata fahamu na kujua mema na mabaya kama shetani alivyowaambia?

Kwa nini wanadamu tumekua tishio kwake baada ya kula mti wa ufahamu na kuamua kutupa laana ya kifo?

Mwanzo 6:3 " bwana akasema, roho yangu haitakaa kushindana na mwanadamu milele, Kwa kuwa yeye ni nyama, basi siku zake zitakua miaka Mia na ishirini"

Mmeona Mungu alivyotugeuka? Hataki tufanane nae Tena kama alivyosema, na kaamua kutupa ukomo wa miaka ya kuishi duniani

Hakika wewe ni Mungu , hakuna wa kushindana na wewe .

Sent from my iPhone using JamiiForums
Story za kutunga tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ulimi waupanga

" Nafikiri kosa la Shetani siyo kumdanganya Eve/Hawa bali ni KUFICHUA SIRI ZA MUNGU KWA MWANADAMU. Jiulize kama kweli Adamu alikuwa na maisha ya milele kwanini Mungu apande mti wa Uzima? Apa inaonesha Adamu alipungukiwa vitu viwili ili awe kama Mungu, kwanza ni MAARIFA( Ujuzi wa mema na mabaya) pili ni MAISHA YA MILELE. "
.....................................................

Quoted

Hapana Adamu hakupungukiwa viwili tu, ili afanane na Mungu,
Kuna vitu vingi sana, kama vile

OMNIPRESENCE, yaani Uweza wa kuwa mahali pote, kwa wakati wote.

OMNIPOTENCE, yaani uwezo wa kutenda maajabu kama kuuzuia moto usiwale Shadrach, Meshach na Abernego,
Uweza wa uumbaji NK,

OMNISCIENCE, yaani uwezo wa akili, uelewa, ujuzi, utambuzi, kufikiri na kubuni mambo kwa umahili mkuu sana.

OMNIUNKNOWN, yaani uweza wa mambo ambayo sisi Binadamu, Malaika, na Shetani hatuyafahamu hadi hii leo.
Na uweza huu upo mwingi kuliko huo tunaoujua

Sisi Binadamu hatufahamu hata siku ya Kiama itakuwa lini, wala hatuelewi tutakuwa ktk maumbo gani baada ya kuuacha mwili wetu makaburini, na pia huko Mbinguni kukoje nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
Malaika si wanakaa mbinguni mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hili jina lako la big IQ hufanani kbisa Na unavyoviongea maana hata sijui hapo kigumu kuelewa kwako Ni nini rafiki.Huyo mwanao unaesema ukimkataza kuweka sukari kweny chai akawwka sukari ukamchapa kweny Tukio la Eden ui relate hiviiiii...!!!!Utamchapa mtoto wako kwa sababu ya kutokutii/kiburi.Ndivyo ilivyokuwa kwa Mungu.Mungu alimwadhibu Adam essence ikiwa kwa kukosa utii.Yaani yes alikula tunda lakini issue sio kula tunda issue Ni Adam kula tunda lilikuwa forbidden this means Kulikuwa Na upotofu wa utii kwa Maagizo ya Mungu Na ukumbuke kukosa utii Ni dhambi inayomkera Mungu maana ndo hufanya mwandamu atende dhambi zote.Na hii ndo dhambi iliyomwangusha Lucifer kutoka mbinguni kwa taarifa yako.Ukishakosa utii kwa Mungu Mungu anajua utafanya mengi hivyo anakuondoa patakatifu pake.Sababu Eden ilikuwa eneo takatifu sasa angemwacha maana yake angeruhusu patakatifu pake page uwanja wa dhambi.Ni Kama vile angemwacha lucifer akae mbinguni wakti aliasi.Alimshusha ili kuiweka mbingu mbali Na dhambi.Same alichofanya kwa Adam.Alimfukuza Ili kuiweka Eden mbali Na dhambi.(jibu kwa wale mnaojiuliza kwanini aliwafukuza).Mungu hakuwachukia kina Adam baada ya kutenda dhambi Ila aliichukia dhambi Na aliitaka kuitenga Eden mbali Na uasi.Pili hicho unachosema mzazi kumkataza mwanae kuweka sukari kweny chai,kweny Tukio la Eden iweke hiviiii ili uelewe.!!!!!!Mungu Ni Kama mzazi tena Ni zaidi ya mzazi.Anatupenda mnooo.mfano wako unaweza sema mzazi kamkataza mwanae kuweka sukari kweny chai afu baadae anamchapa Na wewe uko assume sukar Ni Nzuri but kiuhalisia hakuna mzazi asiyempenda mwanae so akimkatalia mwanae kula sukari lazima anajua hiyo sukari japo inaonekana Ni Nzuri lakini kwa mwanae sio Nzuri mfano mwanae Ana kisukari or anything else .Same kwa Mungu pia...Kama Mungu alimkataza Adam asile lile tunda japo tunda kilio kana zuri kwa macho kwa kula Kama shetani alivyomdangnya Hawa lakini Mungu yeye Kama mzazi alijua hakukuwa Na jema from that tunda ndo maana alimkataza.Mungu anatupenda Na anatuwazia mema shetani anatuwazia tuanguke siku zote weka hiyo akilini mwako

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimependa uchambuzi wako mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Well said brother, Papa ni kiongozi wa kanisa la RC na sio kiongozi wa Ukristo, huyo papa angeulizwa pia hicho cheo kakitoa wapi ndani ya Biblia? Kwa ujumla kama ulivyo sema, Wakristu peke yake ndio wanao mkubali papa lakini Wakristo HAPANA, wanamuona kiongozi kama walivyo viongozi wengine tu. So papa sio mfano wa Ukristo popote duniani and by the way RC wameharibu misingi mingi sana ya Ukristo kwenye hi dunia.

Back to the topic, mleta UZI, naomba unielekeze walipo Adam Na Hawa ili na mimi nikawaone and then nami nijiunge na wewe kuhusu ukweli wa shetani na uongo wa Mungu!

Sawaaaaa kabisaaaa.Ila mkuu Mimi Ni "Ke" sijui why wengi Kama mtu hajaniona aone nimeandika mahali anadhani Ni mkaka ahahaha by the way mi mdadA buanaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu take easy,aliposema na tuumbe mtu kwa mfano wetu alimanisha alikuwepo Mungu Baba,Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu.Hapa kuna watu huwa hawaelewi ukiwaambia Yesu alikuwepo wakati wa uumbaji,wao wanasema alianzia pale alipozaliwa na bikira Maria,hawajui maandiko yanelezea kule kuzaliwa na Bikira maria ni Neno kuuvaa mwili akaja kwetu tukauona utukufu,na Neno maana yake ni Yesu.Soma Yohana 1:1 "Hapo Mwanzo alikuwepo Neno,naye Neno alikuwepo kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu.....".Hapa wengi wameachwa ,usicheze na Jehova yeye anajua moyo wako unapokuwa unasoma biblia una nia ya kujifunza au unataka kuikosoa injili,lazima kuna mambo hutayajua au utayajua ndivyo sivyo.
Shetani alitoza siri gani ?Hakuna siri yeyote aliyotoa zaidi ya kuwadanganaya kasome vizuri hapo kwenye kitabu cha Mwanzo.
Angalizo:Waangalieni viongozi wenu wa dini kama kuna pete wanazivaa tofauti na pete za ndoa,waulize hizo pete ni za nini au zina kazi gani.Sitaelezea sana mwenye masikio na asikie.
Duuh mkuuu...Pete tena??

Mbona wanazivaa sana? Ni ishu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuh mkuuu...Pete tena??

Mbona wanazivaa sana? Ni ishu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Pete zinazovaliwa na watumishi wa Mungu tofauti na pete za ndoa ni issue,kuna kitu kipo pale sasa mfuatilie na nyie,mimi nimewaona wengi tu wakristo na wasio wakristo baadaye katika kufuatilia nakuta wanatuhumiwa.Safari ya kuingia mbinguni si ya kucheza inahitaji kujitoa na kujibidiisha kumtafuta Mungu na kujifunza Neno lake na kulitafakari mchana na usiku.
Zimepewa jina la kuzifunika wanaziita pete za bahati,lakini kuna jambo limefichwa.
 
Mkuu naelewa kabisa kwenye hii sura inaongelea Pharaoh kama Mti lakini hoja yangu ni kwamba miti ya Eden kwenye hii sura ya Ezekiel 31 umetumika figuratively ndio najengea hoja kwanini basi muamini Genesis inaongelea mti la kawaida what if ni fumbo kama Ezekiel??

Mfano ukisoma yohana 15:1 Yesu anajiita ni mzabibu mwema (True Vine) na anawafananisha wanafunzi wake kama matawi ya huo mti sasa mtu akisoma kichwa kichwa si atasema Yesu alikuwa mti??

Au twende Isaya 55
12 Maana mtatoka kwa furaha,Mtaongozwa kwa amani;Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo;Na miti yote ya kondeni itapiga makofi.

Je milima inaongea?? Miti inaweza piga makofi?? Je nkikuomba unisaidie ni mti gani unaweza piga makofi utaweza??

Na sio mimi niliyesema kuwa Biblia ni mafumbo/lugha ya picha bali Yesu na manabii wa Agano la kale

Zaburi 78:2
2 Na nifunue kinywa changu kwa mithali,Niyatamke mafumbo ya kale.

Na andiko hili analitimiza Yesu

Mathayo 13:35
34 Hayo yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; wala pasipo mfano hakuwaambia neno;
35 ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema,Nitafumbua kinywa changu kwa mifano,Nitayatamka yaliyositirika tangu awali.

Kama Yesu na manabii walisema kuwa ataongea nasi kwa parables/mafumbo Je kwanini tunataka kutafsiri biblia Laterally?? Ina maana Yesu alipotosha aliposema anatimiza unabii kuwa ataongea kwa mafumbo hivyo maneno yake kwenye Biblia ni figurative sio lateral!!

Nina mifano mingi tu ya Biblia kutumia lugha ya mafumbo ambayo tukisema tutafsiri kama mnavyofanya tunaweza tusipate maana na ndio maana vitabu kma daniel,ezekiel,ufunuo na jeremiah watu hawavielewi sababu wakienda na akili ya kimwili wanaona havieleweki maana kuna story za mtu kuvaa jua, milima kutupwa kuzimu,Maji kucheza mziki n.k

Bottom line Je ni wakati gani Biblia inaposema kitu tutafsiri laterally au figuratively??

Karibu kwa mjadala
Mkuu mimi naungana na unayoyasema kwamba biblia inatumia lugha ya picha ua mafunmbo hilo nakubali ila si kila sehemu,kwa mfano Mungu lipotoa amri kumi aliposema usiibe,usizini,usitamani hapo hakuna fumbo.Pia nakubaliana na wewe ya kwamba Yesu aliwafundishwa kwa mifano kwenye agano jipya hapo uko sahihi lakini kwenye bustani ya Edeni Mungu Baba ndiye alisema na Adam kwa hiyo lile suala la utabili wa Yesu kuwafundisha wa mafumbo haliapply pale Edeni kwani pale alikuwa ni Mungu Baba akiwapa utaratibu wa kuishi kwenye hiyo Bustani.
Lakini pia unapokuwa unasoma biblia tambua kwamba katika agano la kale Mungu Baba ndiyo alionekana zaidi au alihusika sana na wanadamu hii haimanishi Roho Mtakatifu na Yesu hawakuwepo.Katika Agano jipya Yesu alihusika zaidi na baada ya Yesu kupaa anayehusika zaidi katika kipindi chetu ni Roho Mtakatifu.Ndiyo maana Yesu kabla ya kuondoka aliwaambia wafuasi wake ya kwamba sitawaacha yatima nitawaletea msaidizi ambaya ni Roho Mtakatifu huyo mtakuwa naye milele.Hapa kuna ndugu wamepotoshwa eti hii ahadi ya Yesu ilimhusu mtume fulani lakini hawalielewi andiko linasema atakaa nasi milele lakini yule mtume alikufa.
Nakubaliana na maandiko uliyoyatumia suala la miti kuimba hilo siwezi kukupa jibu kwani pia katika kitabu cha Luka Yesu alipoambiwa awanyamazishe wanafunzi wake aliwaambia ,wakinyamaza ataamulu mawe yapige kelele sasa hapo Yesu hakuelezea kama yangukuwa mawe kweli au watu wengine waiokuwa wameamini au vyovyote vile.

Kuhusu swali lako la hapo mwishoni hakuna formula eti hapa utatafasili laterally au figuratively ninachokijua mimi,kwa mtumishi aliyekua Kiroho anapokuwa anatakiwa kufundisha au kuhutubu huenda kumwomba Mungu ampe nini cha kufundisha na huko pia hupewa maandiko,yakija yenye mafumbo yupo mwalimu ambaye ni Roho Mtakatifu atamsaidia,that is why ni muhimu sana kwa mkristo kujazwa Roho Mtakatifu.Yeye hutufundisha na kutufunulia siri zilizofichika.Lakini ukikuta mtu anafundisha kwa mazoe inawezekana akachukua wengine walivyofundisha sisemi kwamba ni mbaya ila kuna tofauti Bwana akikupa ujumbe from scratch na ukifundisha uliousikia sehemu huwa kunatofauti.All in all,watumisi wa kweli hutumika kama vyombo tu,anayefundisha ni Roho Mtakatifu.
 
Tumuumbe mtu kwa mfano wetu? Ina maana kuna anayefanana na Mungu mwingine? Why sio kwa mfano wangu iwe wetu Au ndo akina azazel , somebody atueleweshe hapa au sisi Ndo tumesoma vibaya, lol

Sent from my iPhone using JamiiForums

Mungu yu katika nafsi tatu.By "mfano wetu" alikuw anamaanisha nafsi zake zingine mbili Yaani Kristo Yesu (ambaye Ni neno) Na Mungu roho mtakatifu.Ukisoma wakat wa uumbaji Maandiko yanasema "Na roho ya Mungu ikatulia katika maji (Nafsi ya Mungu roho)then uumbaji ulihusisha neno( Yaani Kristo)Na Mungu baba.So ule uwingi Ni kwamba Mungu alikuwa anashirikisha nafsi zake tatu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom