Katika hili, namwamini Shetani

Katika hili, namwamini Shetani

Nafikiri kosa la Shetani siyo kumdanganya Eve/Hawa bali ni KUFICHUA SIRI ZA MUNGU KWA MWANADAMU. Jiulize kama kweli Adamu alikuwa na maisha ya milele kwanini Mungu apande mti wa Uzima? Apa inaonesha Adamu alipungukiwa vitu viwili ili awe kama Mungu, kwanza ni MAARIFA( Ujuzi wa mema na mabaya) pili ni MAISHA YA MILELE.

Aya mambo mawili ya utimilifu wa Adamu, Mungu aliyafanya fumbo ili Adamu hasiwe nayo ili awe tegemezi kwa bwana Mungu wake. Ili fumbo Mungu aliliweka kama tunda japo siyo tunda kama tunda! Na akamwambia Adamu hasiguse apo maana alijua Adam akifumbua ayo Mafumbo mawili basi hataweza tena kumdhibiti Adamu maana atakuwa na Utimilifu wote.

Kwahiyo shetani alichofanya ni kufichua siri ya Mungu kwa Adamu akiamini Adamu akitimilika basi atapata kiumbe mwingine wa kushirikiana naye kupambana na Utawala wa Mungu. Mungu kwa kutambua hila za Shetani akamfukuza Adamu kwenye ile Bustani ili hasile tunda la pili(kufungua code namba mbili) za kuishi milele.

Kwahiyo Shetani hajasema uongo ni ukweli japo ni ukweli ambao Mungu hakutaka ujulikane kwa Adamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Good

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Lakini ukiangalia vizuri kifo kililazimika kuwepo, jiulize je kisingekuwepo wengine wangezaliwaje? Na dunia hii sasa hivi tungekuaje?
Mkuu kwani uwepo wa kifo ndiyo unafanya wengine wazaliwe?Kifo kisingekuwepo hata haya maswali unayouliza pia yasingekuwepo,kwa kifupi Mungu ahitaji umsaidie kupanga ingekuwaje.Yeye anajua kila kitu,relax acha yeye atawale.
 
Mungu alisema tumuuumbe mtu kwa mfano wetu lakini cha kushangaza akatunyima ufahamu,yaani ni kama vile ali cheat,aliposema tumuumbe mtu kwa mfano WETU inamaana hakuwa peke ake,hata shetani alikuwepo na alishuhudia rafu tuliyochezewa,mpango wa mungu ilikua usitofautiane sana na mbuzi au nguruwe maana wote hamjui mema na mabaya,hii rafu shetani akaona sio poa kabisa,huu sio mpango wetu wa kumuumba kwa mfano wetu,kwahiyo kutoa siri ya mti wa kati ni kama ku insert program ambayo tulistahili ila tukanyimwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wewe ni mpotoshaji,kama wale jamaa tabia zao husoma maandiko hawayamalizii,umesema Mwanzo 3:22 mimi nakuomba uendelee usome mpaka Mwanzo 3:24
"Na basi akamfukuza huyo mtu, akaweka upande wa mashariki wa bustani ya Edeni+ makerubi+ na upanga unaowaka ambao ulikuwa unajizungusha-zungusha ili kuilinda njia ya kwenda kwenye ule mti wa uzima. "
Mungu alimwambia Adam hakika siku utakayokula tunda utakufa,kwa hiyo Neno litokalo kinywani mwa Bwana lazima litimie,hivyo angewaacha kwenye bustani wangekula tunda la uzima na kuishi milele.Na sababu aliyowafukuza ni ili wasiweze kula tunda la uzima wakaishi milele kitu ambacho kingefanya kile alichowaambia mwanzo kisitimie ndiyomaana aliweka malaika kuilinda njia ya kwenda kwenye mti wa uzima,Mungu huliangalia Neno lake apate kulitimiza.

Nakuuliza tena wewe ni Mkristo?Je ni msom,aji wa biblia mara kwa mara?Je umejazwa Roho Mtakatifu?
mkuu naomba namba yako aisee wewe unaweza nisaidia issue zangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wewe mleta kwani adam na hawa wapo mpaka leo? siwalikufa? au tatizo ni kwakuwa ilichukua muda wao kufa ulitaka Mungu awambie mtakufa baada ya kipindi fulani mana sio kwamba Mungu aliwambia mtakufa hapo hapo aliwaambia tu mkila mtakufa na kweli mwisho wa siku walikufa
Swala la kufa lilikuja kama adhabu baada ya kula tunda,aliposema ukila tunda la mti wa kati hakika utakufa ni kama wew umwambie mwanao ukiweka sukari kwenye chai nitakuchapa,akaja mtu akamwambia chai inatakiwa iwekwe sukari,alipoweka sukari ukaja ukamchapa,kwahiyo hapo sio swala la ahadi yako ya kumchapa kutimia ila hiyo adhabu ya kumchapa ni haki?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona kuna haja ya somo la theolojia kuwa mandatory kwa wakristo wote hivi mpaka leo kuna watu wanaamini tunda lilioliwa ni Tunda as Tunda??

Jamani lugha iliyotumika hapa ni figurative yaani lugha ya picha ila haina maana ni mti kma hii miti yetu au tunda kama haya matunda yetu kama watu mnadai hii miti ya Eden ni miti ya kawaida naomba mnielezee hii sura

Ezekiel 31:9
9 Nalimfanya kuwa mzuri kwa wingi wa matawi yake; hata miti yote ya EDEN, iliyokuwa ndani ya bustani ya Mungu, ilimwonea wivu.

18 Umefanana na nani, hivi katika utukufu na ukuu, kati ya miti ya EDEN? Lakini utashushwa pamoja na miti ya EDEN, hata pande za chini za nchi; utalala kati ya hao wasiotahiriwa; pamoja na hao waliouawa kwa upanga.

SWALI
Je ni miti gani ya Eden imepelekwa kuzimu wakati kuzimu ni kwa ajili ya shetani na wafuasi wake??

Je miti inaweza kuoneana wivu kama wanadamu?

Je miti inaweza kuhukumiwa na Mungu kisa inaKIBURI yaani miti ina character za kibinadamu?

Biblia ni figurative otherwise mkisema mti ni mti wa kawaida basi mnisaidie hayo maswali angu hapo juu!!

Sasa kama biblia imeandika ni tunda unataka sisi tuseme sio tunda Bali walikula chips? Ulitaka tulifafanue vip hilo tunda? , Sasa kumbe hata biblia huiamini so which is which ?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu kwani uwepo wa kifo ndiyo unafanya wengine wazaliwe?Kifo kisingekuwepo hata haya maswali unayouliza pia yasingekuwepo,kwa kifupi Mungu ahitaji umsaidie kupanga ingekuwaje.Yeye anajua kila kitu,relax acha yeye atawale.

Aaaaag lol , good answer

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mungu alisema tumuuumbe mtu kwa mfano wetu lakini cha kushangaza akatunyima ufahamu,yaani ni kama vile ali cheat,aliposema tumuumbe mtu kwa mfano WETU inamaana hakuwa peke ake,hata shetani alikuwepo na alishuhudia rafu tuliyochezewa,mpango wa mungu ilikua usitofautiane sana na mbuzi au nguruwe maana wote hamjui mema na mabaya,hii rafu shetani akaona sio poa kabisa,huu sio mpango wetu wa kumuumba kwa mfano wetu,kwahiyo kutoa siri ya mti wa kati ni kama ku insert program ambayo tulistahili ila tukanyimwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu take easy,aliposema na tuumbe mtu kwa mfano wetu alimanisha alikuwepo Mungu Baba,Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu.Hapa kuna watu huwa hawaelewi ukiwaambia Yesu alikuwepo wakati wa uumbaji,wao wanasema alianzia pale alipozaliwa na bikira Maria,hawajui maandiko yanelezea kule kuzaliwa na Bikira maria ni Neno kuuvaa mwili akaja kwetu tukauona utukufu,na Neno maana yake ni Yesu.Soma Yohana 1:1 "Hapo Mwanzo alikuwepo Neno,naye Neno alikuwepo kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu.....".Hapa wengi wameachwa ,usicheze na Jehova yeye anajua moyo wako unapokuwa unasoma biblia una nia ya kujifunza au unataka kuikosoa injili,lazima kuna mambo hutayajua au utayajua ndivyo sivyo.
Shetani alitoza siri gani ?Hakuna siri yeyote aliyotoa zaidi ya kuwadanganaya kasome vizuri hapo kwenye kitabu cha Mwanzo.
Angalizo:Waangalieni viongozi wenu wa dini kama kuna pete wanazivaa tofauti na pete za ndoa,waulize hizo pete ni za nini au zina kazi gani.Sitaelezea sana mwenye masikio na asikie.
 
Mungu alisema tumuuumbe mtu kwa mfano wetu lakini cha kushangaza akatunyima ufahamu,yaani ni kama vile ali cheat,aliposema tumuumbe mtu kwa mfano WETU inamaana hakuwa peke ake,hata shetani alikuwepo na alishuhudia rafu tuliyochezewa,mpango wa mungu ilikua usitofautiane sana na mbuzi au nguruwe maana wote hamjui mema na mabaya,hii rafu shetani akaona sio poa kabisa,huu sio mpango wetu wa kumuumba kwa mfano wetu,kwahiyo kutoa siri ya mti wa kati ni kama ku insert program ambayo tulistahili ila tukanyimwa

Sent using Jamii Forums mobile app

Tumuumbe mtu kwa mfano wetu? Ina maana kuna anayefanana na Mungu mwingine? Why sio kwa mfano wangu iwe wetu Au ndo akina azazel , somebody atueleweshe hapa au sisi Ndo tumesoma vibaya, lol

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sasa kama biblia imeandika ni tunda unataka sisi tuseme sio tunda Bali walikula chips? Ulitaka tulifafanue vip hilo tunda? , Sasa kumbe hata biblia huiamini so which is which ?

Sent from my iPhone using JamiiForums
Hakuna aliyepinga Biblia au mada yako ila point is haikumaanisha tunda au mti kama hii ya sasa yaani apple au embe ila ni lugha ya fumbo tu, maana nimeona kila anayechangia anaongelea miti na matunda ya kimwili ndio maana ikabidi niweke hiyo rai that's why nikasema kma walimaanisha ni miti kama miti yetu mbona Ezekiel 31 inaelezea miti ya Eden ina wivu? Miti ina kiburi?? Miti itahukumiwa kuzimu??

Bible ni figurative
 
N.:0:::/:"0p/szs0z0s000.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Swala la kufa lilikuja kama adhabu baada ya kula tunda,aliposema ukila tunda la mti wa kati hakika utakufa ni kama wew umwambie mwanao ukiweka sukari kwenye chai nitakuchapa,akaja mtu akamwambia chai inatakiwa iwekwe sukari,alipoweka sukari ukaja ukamchapa,kwahiyo hapo sio swala la ahadi yako ya kumchapa kutimia ila hiyo adhabu ya kumchapa ni haki?

Sent using Jamii Forums mobile app
sasa hayo ni mawazo yako wewe sio mawazo ya MUNGU, na Mungu si mwanadamu hata aseme uwongo hivyo alichosema ndicho alichomaanisha hayo mengine umeyatunga wewe kwababu umetafuta shauri la kupingana na neno lake
 
Hakuna aliyepinga Biblia au mada yako ila point is haikumaanisha tunda au mti kama hii ya sasa yaani apple au embe ila ni lugha ya fumbo tu, maana nimeona kila anayechangia anaongelea miti na matunda ya kimwili ndio maana ikabidi niweke hiyo rai that's why nikasema kma walimaanisha ni miti kama miti yetu mbona Ezekiel 31 inaelezea miti ya Eden ina wivu? Miti ina kiburi?? Miti itahukumiwa kuzimu??

Bible ni figurative
Mkuu ni kweli the bible is figurative but not all the time,shida ambayo pia nimeiona kwako nikuchukua kisehemu cha maandiko kama wale jamaa ambao hupotosha wakristo kwa kipande cha maandiko.Nikushauri hiyo Ezekiel 31:9,mimi nikushauri uisome kuanzia Ezekiel 31:1-9 hapo utaelewa,hii tabia ya kuchukua kisehemu wakati maelezo yalikuwa mengi ndiyo chanzo cha kutokuelewa na kupotosha.Nakubaliana na wewe lugha iliyotumika katika eneo hilo ni ya mfano(au ukitaka picha kama ulivyosema lakini biblia imesema mfano) ,kwa hiyo tunda la Edeni linabaki kuwa tunda wala si fumbo,ni kweli kwenye biblia kuna mafumbo ila hapo Edeni tunda ni tunda na si vinginevyo.
Tuangalie Ezekiel 31:1-9 nimechukua maandiko kutoka online bible sababu ya muda

31:1 Na ikazidi kutukia kwamba katika mwaka wa kumi na moja, katika mwezi wa tatu, siku ya kwanza ya mwezi huo, neno la Yehova likanijia, na kusema: 2 “Mwana wa binadamu, mwambie Farao mfalme wa Misri na umati wake,+“ ‘Umefanana na nani katika ukuu wako? 3 Tazama! Mwashuru, mwerezi katika Lebanoni,+ wenye matawi ya kupendeza,+ wenye kifuniko chenye majani mengi kinachotoa kivuli, na wenye kimo kirefu,+ hivi kwamba kilele chake kilikuwa kati ya mawingu.+ 4 Ni maji yaliyoufanya uwe mkubwa;+ kilindi cha maji kiliufanya urefuke. Pamoja na vijito vyake kilikuwa kikienda kuzunguka pande zote mahali ulipopandwa; nacho kiliipeleka mifereji yake kwenye miti yote ya shambani. 5 Ndiyo sababu ulikuwa mrefu zaidi kwa kimo kuliko miti mingine yote ya shambani.+“ ‘Na matawi yake yalizidi kuongezeka, na matawi yake yaliendelea kuwa marefu zaidi kwa sababu ya maji mengi kwenye mifereji ya maji.+ 6 Viumbe vyote vinavyoruka vya mbinguni vilifanya viota+vyao kwenye matawi yake, na wanyama wote wa mwituni walizaa chini ya matawi yake,+ na mataifa yote yenye hesabu kubwa ya watu yalikuwa yakikaa katika kivuli chake. 7 Nao ukawa wenye kupendeza katika ukuu wake,+ katika urefu wa majani yake, kwa maana mizizi yake ilikuwa juu ya maji mengi. 8 Mierezi mingine haikulingana nao katika bustani ya Mungu.+ Nayo miberoshi, haikufanana nao kwa habari ya matawi yake. Na miaramoni yenyewe haikuwa kama huo katika matawi yake. Hakuna mti mwingine wowote katika bustani ya Mungu uliofanana nao katika uzuri wake.+ 9 Niliufanya kuwa mzuri katika wingi wa majani yake,+ na miti mingine yote ya Edeni iliyokuwa katika bustani ya Mungu wa kweli ikawa ikiuonea wivu.’+

Ukisoma kwa makini hapo mwanzoni Farao alikuwa anaulizwa umefanana na nani?Kufanana na kitu si kuwa kitu halisi ni lugha ya mfano,maandiko yakaendelea kwamba "Tazama ,Mwashuru(nchi ya Syria au Wasiria) imefanana na mti wa mwerezi ambao unapatikana katika nchi ya LEBANONI,kwa hiyo ulichochukua kwenye Ezekiel 31:9 kilitanguliwa na hayo uliyoyaacha amabyo yanaonyesha nchi ilifananishwa na mti,na ndiyo maana ikasemwa hata miti ya kwenye bustani ya Edeni iliuonea wivu huu mti wa mwerezi.Ni lugha ya mfano kuelezea jamabo lakini haijaondoa kwamba tunda la Edeni siyo Tunda na kwamba ni fumbo.

Ushauri wangu kwako mtu akikuletea andiko ikiwezekana nenda nyuma na mbele ya andiko hilo paragraph walau mbili au zaidi utaujua ukweli.Kwa hiyo lugha ya pale ni ya mfano,na miti mingine maana yake ni mataifa au watu wa mataifa fulani,kwa hiyo taifa linaweza kuhukumiwa na kwenda kuzimu(hapa namanisha wananchi wa taifa fulani) kwa hiyo wewe ukibaki kwenye je mti unaweza kuhukumiwa umejipotosha mwenyewe.Mwanzoni mwa Ezekiel 31 walianza na farao mtawala wa misri umefananishwa na nini?
Na kama ulikuiwa hujui syria ilikuwa nchi nzuri imara na yenye nguvu kabla ya vita,lakini kwa sasa sihitaji kukueleza juu ya Syria fuatilia mwenyewe.Biblia siyo kitabu cha hadithi za kufikirika,na wanaotumia akili zao kukikosoa kuna siku watakaa kimya.
 
Swala la kufa lilikuja kama adhabu baada ya kula tunda,aliposema ukila tunda la mti wa kati hakika utakufa ni kama wew umwambie mwanao ukiweka sukari kwenye chai nitakuchapa,akaja mtu akamwambia chai inatakiwa iwekwe sukari,alipoweka sukari ukaja ukamchapa,kwahiyo hapo sio swala la ahadi yako ya kumchapa kutimia ila hiyo adhabu ya kumchapa ni haki?

Sent using Jamii Forums mobile app

Na hili jina lako la big IQ hufanani kbisa Na unavyoviongea maana hata sijui hapo kigumu kuelewa kwako Ni nini rafiki.Huyo mwanao unaesema ukimkataza kuweka sukari kweny chai akawwka sukari ukamchapa kweny Tukio la Eden ui relate hiviiiii...!!!!Utamchapa mtoto wako kwa sababu ya kutokutii/kiburi.Ndivyo ilivyokuwa kwa Mungu.Mungu alimwadhibu Adam essence ikiwa Ni kukosa utii.Yaani yes alikula tunda lakini issue sio kula tunda issue Ni Adam kula tunda lililokuwa forbidden.Maana hii ilimaanisha Kulikuwa Na upotofu wa utii kwa Maagizo ya Mungu Na ukumbuke kukosa utii Ni dhambi inayomkera Mungu maana ndo hufanya mwandamu atende dhambi zote.Na hii ndo dhambi iliyomwangusha Lucifer kutoka mbinguni.Ukishakosa utii kwa Mungu,Mungu anajua utafanya mengi hivyo anakuondoa patakatifu pake.Sababu Eden ilikuwa eneo takatifu sasa angemwacha maana yake angeruhusu patakatifu pake pawe uwanja wa dhambi.Ni Kama vile angemwacha lucifer akae mbinguni wakati aliasi.Wengine wangejifunza nini?kuwa Ni sawa Kuasi?Dhambi huwa Ina gharama so Alimshusha ili kuiweka mbingu mbali Na dhambi.Same alichofanya kwa Adam.Alimfukuza Ili kuiweka Eden mbali Na dhambi.(jibu kwa wale mnaojiuliza kwanini aliwafukuza).Mungu hakuwachukia kina Adam baada ya kutenda dhambi Ila aliichukia dhambi Na aliitaka kuitenga Eden mbali Na uasi.Pili hicho unachosema mzazi kumkataza mwanae kuweka sukari kweny chai,kweny Tukio la Eden iweke hiviiii ili uelewe.!!!!!!Mungu Ni Kama mzazi tena Ni zaidi ya mzazi.Anatupenda mnooo.mfano wako unaweza sema mzazi kamkataza mwanae kuweka sukari kweny chai afu baadae anamchapa Na wewe una assume sukar Ni Nzuri kwa chai,yes.But kiuhalisia hakuna mzazi asiyempenda mwanae so akimkatalia mwanae kula sukari lazima anajua hiyo sukari japo inaonekana Ni Nzuri lakini kwa mwanae sio Nzuri mfano mwanae Ana kisukari or anything else .Same kwa Mungu pia...Kama Mungu alimkataza Adam asile lile tunda japo tunda lilionekana zuri kwa macho kwa kula Kama shetani alivyomdangnya Hawa lakini Mungu yeye Kama mzazi alijua hakukuwa Na jema from that ndo maana alimkataza.Mungu anatupenda Na anatuwazia mema shetani anatuwazia mabaya siku zote weka hiyo akilini kwako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ni kweli the bible is figurative but not all the time,shida ambayo pia nimeiona kwako nikuchukua kisehemu cha maandiko kama wale jamaa ambao hupotosha wakristo kwa kipande cha maandiko.Nikushauri hiyo Ezekiel 31:9,mimi nikushauri uisome kuanzia Ezekiel 31:1-9 hapo utaelewa,hii tabia ya kuchukua kisehemu wakati maelezo yalikuwa mengi ndiyo chanzo cha kutokuelewa na kupotosha.Nakubaliana na wewe lugha iliyotumika katika eneo hilo ni ya mfano(au ukitaka picha kama ulivyosema lakini biblia imesema mfano) ,kwa hiyo tunda la Edeni linabaki kuwa tunda wala si fumbo,ni kweli kwenye biblia kuna mafumbo ila hapo Edeni tunda ni tunda na si vinginevyo.
Tuangalie Ezekiel 31:1-9 nimechukua maandiko kutoka online bible sababu ya muda

31:1 Na ikazidi kutukia kwamba katika mwaka wa kumi na moja, katika mwezi wa tatu, siku ya kwanza ya mwezi huo, neno la Yehova likanijia, na kusema: 2 “Mwana wa binadamu, mwambie Farao mfalme wa Misri na umati wake,+“ ‘Umefanana na nani katika ukuu wako? 3 Tazama! Mwashuru, mwerezi katika Lebanoni,+ wenye matawi ya kupendeza,+ wenye kifuniko chenye majani mengi kinachotoa kivuli, na wenye kimo kirefu,+ hivi kwamba kilele chake kilikuwa kati ya mawingu.+ 4 Ni maji yaliyoufanya uwe mkubwa;+ kilindi cha maji kiliufanya urefuke. Pamoja na vijito vyake kilikuwa kikienda kuzunguka pande zote mahali ulipopandwa; nacho kiliipeleka mifereji yake kwenye miti yote ya shambani. 5 Ndiyo sababu ulikuwa mrefu zaidi kwa kimo kuliko miti mingine yote ya shambani.+“ ‘Na matawi yake yalizidi kuongezeka, na matawi yake yaliendelea kuwa marefu zaidi kwa sababu ya maji mengi kwenye mifereji ya maji.+ 6 Viumbe vyote vinavyoruka vya mbinguni vilifanya viota+vyao kwenye matawi yake, na wanyama wote wa mwituni walizaa chini ya matawi yake,+ na mataifa yote yenye hesabu kubwa ya watu yalikuwa yakikaa katika kivuli chake. 7 Nao ukawa wenye kupendeza katika ukuu wake,+ katika urefu wa majani yake, kwa maana mizizi yake ilikuwa juu ya maji mengi. 8 Mierezi mingine haikulingana nao katika bustani ya Mungu.+ Nayo miberoshi, haikufanana nao kwa habari ya matawi yake. Na miaramoni yenyewe haikuwa kama huo katika matawi yake. Hakuna mti mwingine wowote katika bustani ya Mungu uliofanana nao katika uzuri wake.+ 9 Niliufanya kuwa mzuri katika wingi wa majani yake,+ na miti mingine yote ya Edeni iliyokuwa katika bustani ya Mungu wa kweli ikawa ikiuonea wivu.’+

Ukisoma kwa makini hapo mwanzoni Farao alikuwa anaulizwa umefanana na nani?Kufanana na kitu si kuwa kitu halisi ni lugha ya mfano,maandiko yakaendelea kwamba "Tazama ,Mwashuru(nchi ya Syria au Wasiria) imefanana na mti wa mwerezi ambao unapatikana katika nchi ya LEBANONI,kwa hiyo ulichochukua kwenye Ezekiel 31:9 kilitanguliwa na hayo uliyoyaacha amabyo yanaonyesha nchi ilifananishwa na mti,na ndiyo maana ikasemwa hata miti ya kwenye bustani ya Edeni iliuonea wivu huu mti wa mwerezi.Ni lugha ya mfano kuelezea jamabo lakini haijaondoa kwamba tunda la Edeni siyo Tunda na kwamba ni fumbo.

Ushauri wangu kwako mtu akikuletea andiko ikiwezekana nenda nyuma na mbele ya andiko hilo paragraph walau mbili au zaidi utaujua ukweli.Kwa hiyo lugha ya pale ni ya mfano,na miti mingine maana yake ni mataifa au watu wa mataifa fulani,kwa hiyo taifa linaweza kuhukumiwa na kwenda kuzimu(hapa namanisha wananchi wa taifa fulani) kwa hiyo wewe ukibaki kwenye je mti unaweza kuhukumiwa umejipotosha mwenyewe.Mwanzoni mwa Ezekiel 31 walianza na farao mtawala wa misri umefananishwa na nini?
Na kama ulikuiwa hujui syria ilikuwa nchi nzuri imara na yenye nguvu kabla ya vita,lakini kwa sasa sihitaji kukueleza juu ya Syria fuatilia mwenyewe.Biblia siyo kitabu cha hadithi za kufikirika,na wanaotumia akili zao kukikosoa kuna siku watakaa kimya.
Mkuu naelewa kabisa kwenye hii sura inaongelea Pharaoh kama Mti lakini hoja yangu ni kwamba miti ya Eden kwenye hii sura ya Ezekiel 31 umetumika figuratively ndio najengea hoja kwanini basi muamini Genesis inaongelea mti la kawaida what if ni fumbo kama Ezekiel??

Mfano ukisoma yohana 15:1 Yesu anajiita ni mzabibu mwema (True Vine) na anawafananisha wanafunzi wake kama matawi ya huo mti sasa mtu akisoma kichwa kichwa si atasema Yesu alikuwa mti??

Au twende Isaya 55
12 Maana mtatoka kwa furaha,Mtaongozwa kwa amani;Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo;Na miti yote ya kondeni itapiga makofi.

Je milima inaongea?? Miti inaweza piga makofi?? Je nkikuomba unisaidie ni mti gani unaweza piga makofi utaweza??

Na sio mimi niliyesema kuwa Biblia ni mafumbo/lugha ya picha bali Yesu na manabii wa Agano la kale

Zaburi 78:2
2 Na nifunue kinywa changu kwa mithali,Niyatamke mafumbo ya kale.

Na andiko hili analitimiza Yesu

Mathayo 13:35
34 Hayo yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; wala pasipo mfano hakuwaambia neno;
35 ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema,Nitafumbua kinywa changu kwa mifano,Nitayatamka yaliyositirika tangu awali.

Kama Yesu na manabii walisema kuwa ataongea nasi kwa parables/mafumbo Je kwanini tunataka kutafsiri biblia Laterally?? Ina maana Yesu alipotosha aliposema anatimiza unabii kuwa ataongea kwa mafumbo hivyo maneno yake kwenye Biblia ni figurative sio lateral!!

Nina mifano mingi tu ya Biblia kutumia lugha ya mafumbo ambayo tukisema tutafsiri kama mnavyofanya tunaweza tusipate maana na ndio maana vitabu kma daniel,ezekiel,ufunuo na jeremiah watu hawavielewi sababu wakienda na akili ya kimwili wanaona havieleweki maana kuna story za mtu kuvaa jua, milima kutupwa kuzimu,Maji kucheza mziki n.k

Bottom line Je ni wakati gani Biblia inaposema kitu tutafsiri laterally au figuratively??

Karibu kwa mjadala
 
Hivi wewe faiza aliyekwambia Papa ndo mwakilishi wa ukristo Ni nani?mbona unapendaga kuwa Na kimbelembele kweny mambo hata usiyoyajua?so akisema papa ndo unadhani Ni Kweli ?sasa kwa taarifa yako papa anasikilizwa Na wakatoliki tu tena wakatoliki baadhi sio wote.Asilimia kubwa ya madhehebu ya kikristo yako against papa.Wewe kusema papa ndo anawakilisha ukristo Ni sawa Na Mimi MKRISTO Leo niseme sheikh wenu sheikh yahya ndo anaewakilisha uislamu huku Tanzania Na yale majini aliyokuwa anatumia basi Dini yenu waislamu wote inakubali kutumia majini.Upunguze kiherehre kwa vitu usivyovijua especially Dini za watu unaboaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Well said brother, Papa ni kiongozi wa kanisa la RC na sio kiongozi wa Ukristo, huyo papa angeulizwa pia hicho cheo kakitoa wapi ndani ya Biblia? Kwa ujumla kama ulivyo sema, Wakristu peke yake ndio wanao mkubali papa lakini Wakristo HAPANA, wanamuona kiongozi kama walivyo viongozi wengine tu. So papa sio mfano wa Ukristo popote duniani and by the way RC wameharibu misingi mingi sana ya Ukristo kwenye hi dunia.

Back to the topic, mleta UZI, naomba unielekeze walipo Adam Na Hawa ili na mimi nikawaone and then nami nijiunge na wewe kuhusu ukweli wa shetani na uongo wa Mungu!
 
Na kama ulikuiwa hujui syria ilikuwa nchi nzuri imara na yenye nguvu kabla ya vita,lakini kwa sasa sihitaji kukueleza juu ya Syria fuatilia mwenyewe.Biblia siyo kitabu cha hadithi za kufikirika,na wanaotumia akili zao kukikosoa kuna siku watakaa kimya.
Mkuu wewe ni mtu makini sana sitegemei ufanye hizi errors zitasusha credibility yako..... Syria na Assyria ni vitu viwili tofauti kwenye Biblia Syria ni nchi Aram na Assyria kwa sasa ni Uturuki na Iraq kaskazini ni eneo dogo sana la Syria ndio lipo Assyrian empire hivyo hakuna correlation yeyote kati ya Assyria empire na syria kuanzia jamii ya watu mpaka ardhi.

Kingine unasema hakuna hadithi za kusadikika ukimaanisha kila kitu ni historical facts si ndio?? Sasa niliuliza swali humu nilikosa majibu nikasema mbinu ya kisayansi ya kujua umri wa miamba/fossils yaani biometric dating inaonyesha kuna mafuvu yana umri wa miaka zaidi ya elfu 50,000 wakati hii story mnayojadili ya Adam na Hawa ni miaka elfu 6 pekee iliopita sasa. Mimi naamini Biblia ila napinga utafsiri wa LATERAL maana mtu akiuliza kivipi Adam awe mtu wa kwanza kama mnavyotafsiri humu if kuna mafuvu mazee kuliko Yeye?? Hapa mtasema sayansi inapotosha wakati huo huo mafuvu ya pharaoh anaosadikiwa na wanatheolojia kuwepo wakati wa EXODUS yaani pharaoh Ramses II kwa kutumia mbinu hii hii anaelezwa kufa 1213 BC umri ambao unakubaliana na Biblia!!

Kwahiyo hii system ikitumika ipo consitent na characters wengine wanaotajwa na Biblia hivyo inaprove kuwa ADAM hakuwa mtu wa kwanza duniani?? Sasa ukisema hakuna hadithi ya kusadikika je huoni hata hii hadithi ya Adam na Eve kuwa watu wa kwanza ni kusadikika based on historical facts?

Bottom line ni kwamba hadithi za Biblia ni za Biblia tu haziwezi kuwa proven kisayansi na kihistoria ukitaka tufanye hivyo tutapata errors nyingi so labda niseme tu ukijenga hoja kuhusu Biblia basi baki kwenye Biblia ila ukianza kuforce na kuiback na historical facts basi hapo tutakwama mahali.

Otherwise we ni mtu makini sana ila nilitaka tu kuweka rekodi sawa,

Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom