Katibu Mkuu wa CCM, Aondoke?

Kweli hakuna siri...hata ya mabadiliko makubwa ya baraza baada ma mkutano wa leo si tushayasikia....Tusubiri tuone ka Mzee wa Richmond atapona..
 
Quote: Mtanzania
Mkandara,

Nafikiri kwenye suala la Msekwa kulikuwa na siri kubwa maana hata hapa JF tulishindwa kabisa kutabiri.

Habari haikutoka mpaka baada ya kikao cha CC.

Mtanzania, si kweli jina la Msekwa lili leak a weak ago.... tatizo watu hawakuliwekea maanani..
__________________

Mwanakijiji bora umewapasha, lakini sijui kwanini kila mtu anadiriki kusema kwamba habari za Msekwa hazijawahi kutamkwa na yeyote wakati gazeti la Raia Mwema lilimtaja katika stori yake ya kwanza japo jina lilikua ndani naamkini WAHARIRI walimua makusudi kufanya hivyo ili kuepusha kumharibia kwani alikua mmoja wa watu waliochangia makala katika gazeti hilo.

http://www.raiamwema.co.tz/07/10/31/1.php

Jambo jingine litakalozingatiwa na Mkutano Mkuu ni nafasi ya Makamu Mwenyekiti, inayoshikiliwa sasa na John Malecela.

Malecela hakuwania nafasi ya u- NEC na kuna kila dalili kwamba anaweza kubadilishwa. Baadhi ya majina ambayo yamekuwa yakitajwa ni ya pamoja na Pius Msekwa na mkewe, Anna Abdallah; Sumaye, Kinana na wengine wanamtaja hata Mangula, wote wakionekana kutokua ndani ya kundi maarufu la wanamtandao lililotajwa kusaidia ushindi wa Rais Kikwete.
Malecela amekalia umakamu kwa kipindi kirefu na dhahiri kwa hali ya mambo ilivyo kurejea kwake katika nafasi hiyo kuna utata. Wakati ule wa awamu ya tatu, inaelezwa, kwamba ilihitaji nguvu ya ziada ya Mwenyekiti Mkapa kutetea uteuzi wake, japo baadaye ilikuja kuonekana kuwa nafasi hiyo ilistahili mtu kama Malecela.

Nafuu, pengine ya Malecela (hata kama akiukosa umakamu) na wazee wenzake kama Cleopa Msuya, imo katika sehemu ya mabadiliko ya katiba ya CCM yanayopendekezwa ya kuwafanya wazee kama hao kuwa wanachama wa kudumu wa NEC.

Kwa sasa wanachama hao dumu ni pamoja na Rashidi Kawawa, Mwinyi, Mkapa na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk Salmin Amour.
 
GAzeti la Mwananchi la Novemba 2, 2007, siku tatu baada ya kutoka kwa toleo la kwanza la Raia Mwema, liliandika:

Awali, jina la Msekwa halikuwa miongoni mwa wadadisi wa masuala ya kisiasa, huku majina yaliyokuwa yakipigiwa chapuo ni Mbunge wa zamani wa Ngara, Pius Ngeze, Mbunge wa Sumbawanga, Paul Kimiti, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.


Nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM inashikiliwa na Makamba nayo inaelezwa kuwa huenda ikakumbwa na mabadiliko, huku nafasi kubwa ikitolewa kwa Naibu Katibu wake, Kapteni Jaka Mwambi na Spika mstaafu wa Bunge la Afrika Mashariki, Kanali Abdulrahman Kinana na nafasi ya Mwambi huenda

ikishikiliwa na Mbunge wa Songea, Dk Emmanuel Nchimbi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM.

Na hii si pekee, kwani Mwandishi Taseni ameandika pia katika gazeti la Citizen kwamba hakuna mtu hata mmoja aliyemtaja Msekwa. Hii ni dalili mbaya sana ya waandishi kutokua makini na kusoma habari za wengine, lakini pia ni aibu kwani habari kuhusu Msekwa baada ya kuandikwa na Raia Mwema ziliwekwa humu JF. Lakini kwa waandishi wengi makini walikua wakijua kuhusu Msekwa hasa baada ya JK kupelekewa majina matatu la Mangula, Sumaye na Msekwa, na hivyo kwa wanaomjua Msekwa walijua fika ndiye anayetakiwa. Lakini pia, Msekwa alitafutwa na IKULU katikati ya Oktoba, 2007 kwa juhudi zote na alikwishajulishwa kama atakua tayari kushika wadhifa huo na yeye kukubali, kuendelea kukitumikia chama chake. WAANDISHI MAKINI walifahamu na humu JF kuna mahali ilitajwa kuhusu majina matatu akiwamo Msekwa.
 
GAzeti la Mwananchi la Novemba 2, 2007, siku tatu baada ya kutoka kwa toleo la kwanza la Raia Mwema, liliandika:



Na hii si pekee, kwani Mwandishi Taseni ameandika pia katika gazeti la Citizen kwamba hakuna mtu hata mmoja aliyemtaja Msekwa. Hii ni dalili mbaya sana ya waandishi kutokua makini na kusoma habari za wengine, lakini pia ni aibu kwani habari kuhusu Msekwa baada ya kuandikwa na Raia Mwema ziliwekwa humu JF. Lakini kwa waandishi wengi makini walikua wakijua kuhusu Msekwa hasa baada ya JK kupelekewa majina matatu la Mangula, Sumaye na Msekwa, na hivyo kwa wanaomjua Msekwa walijua fika ndiye anayetakiwa. Lakini pia, Msekwa alitafutwa na IKULU katikati ya Oktoba, 2007 kwa juhudi zote na alikwishajulishwa kama atakua tayari kushika wadhifa huo na yeye kukubali, kuendelea kukitumikia chama chake. WAANDISHI MAKINI walifahamu na humu JF kuna mahali ilitajwa kuhusu majina matatu akiwamo Msekwa.

Halisi,

Asante kwa ufafanuzi, mimi kama nilivyoandika mwanzoni sikuwahi kuliona jina la Msekwa likitajwa mpaka alipotangazwa. Hata hapa JF sikuona mtu akilijadili hilo jina, huenda wengi tulipitwa na hiyo habari.

Hayo majina matatu JK alipelekewa na nani? Nani alipendekeza hayo majina matatu kwa JK?
 
Leo saa tano wakubwa wanakutana NEC Dom ndani ya white house- tupeni jina la katibu mkuu????????????
Pongezi kwa JK na CCM kwa kuvuka salama salmini mkutano huu kwa manufaa ya nchi.
 
Mkandara,

Nafikiri kwenye suala la Msekwa kulikuwa na siri kubwa maana hata hapa JF tulishindwa kabisa kutabiri.

Habari haikutoka mpaka baada ya kikao cha CC.

Taarifa ziliandikwa mapema kabisa kwenye vyombo vya habari na sababu za uteuzi huo.
Iliandikwa, wanaangalia mtu ambaye hawezi kuwa hatari kwenye uteuzi wa wagombea uraisi 2015.

Wakasema wakimweka Sumaye atahatarisha nafasi ya watu, ikaonekana Msekwa kwa umri wake hawezi kuwa na ndoto ya uraisi hivyo anafaa kwenye nafasi hiyo kwani hatogombea!

Ndo hayo yaliyoandikwa siku kadhaa kabla ya iteuzi!!!
 
Kama nilivyojenga hoja wiki kadhaa zilizopita ninaamini kabisa kuna uwezekano kuwa Makamba atang'oka...
 
Lt Makamba bado anafaa sana kuendelea kushika nafasi ya Ukatibu Mkuu. Utendaji wake upo katika kiwango cha juu kupita wakati wote wa uongozi wake kwa sasa. Tatizo ni mitazamo hasi ya wengi, ambao hupenda kusikia yale yaliyo kwenye nafsi zao tu. Mpaka sasa ameweza kuwazindua watendaji wengi goi goi ndani ya CCM kuanzia ngazi za matawi, ambao walikuwa wameanza kujisahau katika utendaji wao wa kila siku. Kitaifa ameendelea vema kusimamia matakwa ya CCM katika awamu ya kuziba mpasuko huko Visiwani.

Hapana shaka ataendeleza vema mazungumzo ya kufikia muafaka ambao utakuwa na manufaa kwa pande zote mbili.

Hoja za Upinzani kuhusu Ufisadi na mafisadi ameweza kuzijibu kwa ufasaha kabisa na kisiasa zaidi, na hakuna mjadala kwa hilo.

Kibunango haka kaslogan "SAVE WATER DRINK BEER" Ingawa nimekuwa nakikaona katika ISIDINGO kamenivunja mbavu maana siku moja ndugu yangu alipatwa na haka kagonjwa ka kipindupindu a.k.a. kigeugeu
Akasema nikipona sitakunywa tena maji yeye aliyaita maji ya vingunguti, nikamuuliza utakunywa nini, akasema nitakunywa beer tu. Sasa na wewe umenikumbusha hoja moja kwamba kuokoa maji kwa kunywa beer je beer inatengenezwa kwa kutumia nini? Ukipata jibu basi kumbuka hujasevu kitu.
 
Kama ni hivyo,kacheza karata yake ya mwisho vizuri. Kauli kuwa akibwagwa hata wapinzani watamcheka inanguvu sana ndani ya Chama kwa sasa. Swali ni jee style yake ya kazi atawezana na Mzee Msekwa?
 
Swali ni jee style yake ya kazi atawezana na Mzee Msekwa?


But who is Msekwa? Huyu wala sio mjumbe wa secrtariat yao! Halafu Msekwa mpaka anaona amependelewa sana maana ameibuliwa kutoka kwenye jalala la takataka ambapo alishatupwa!
 
Makamba -secretary general

Amos Makala-FEdha

Kidawa-Oganizainesheni

Membe-Mahusiano ya mambo ya nje

Source:Nchimbi
 
Makamba -secretary general

Amos Makala-FEdha

Kidawa-Oganizainesheni

Membe-Mahusiano ya mambo ya nje

Source:Nchimbi
 
Hata kama JK angetaka kubadili watu wamevujisha mno mapema hadi kwenye magazeti, kwa hiyo ameamua kuwaumbua. Nadhani hataki kuonekana anafanya kazi kwa kufuata maoni ya magazetini. Maoni yangu.
 
JK kabadili serious issues kuwa mchezo na kuwaita wachapa kazi akina Slaa kwamba ni watani wake . Kumweka Makamba ni kukomaza upuuzi wa mawazo ya aina hiyo .
 
Hata kama JK angetaka kubadili watu wamevujisha mno mapema hadi kwenye magazeti, kwa hiyo ameamua kuwaumbua. Nadhani hataki kuonekana anafanya kazi kwa kufuata maoni ya magazetini. Maoni yangu.

Mbona uteuzi wake wote umefuata magazeti? Hata Msekwa alitajwa na Raia Mwema! Hakuna aliyeteuliwa na Kikwete ambaye hakutajwa kabla. Hii ndiyo staili ya Kikwete...mambo yake yanatabirika kirahisi, yanavuja kama zinavyovuja siri za wizi serikalini mwake, na ndiyo itakayommaliza mapema rafiki yangu JK.
 
Posted Date::11/6/2007
Kikwete amrejesha Makamba kundi la vigogo CCM
* Kusaidiwa na makapteni wawili
* Kingunge, Sumaye nje Kamati Kuu

* Waliotemwa sekretarieti kupangiwa kazi

* Salim, Msuya waula, nane kuteuliwa

Na Midraji Ibrahim, Dodoma
Mwananchi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekamilisha kupanga safu ya uongozi wake, huku Katibu Mkuu, Yusuf Makamba akifanikiwa kubaki kwenye nafasi yake na mwanasiasa wa siku nyingi, Kingunge Ngombale-Mwiru akitupwa nje ya Kamati Kuu (CC) ambamo amedumu kwa kipindi kirefu.

Kingunge ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano Jamii), alipendekezwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete kwa halmashauri kuu, lakini akadondoshwa kwenye kura.

Kigogo mwingine aliyeangushwa ni Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ambaye katika kura za NEC aliibuka na ushindi mnono.

Akizungumza baada ya kikao hicho jana mjini hapa, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, alisema Mwenyekiti wa chama aliwaeleza wajumbe kwamba waliokuwemo sekretarieti iliyopita watapangiwa kazi nyingine na kwamba isichukuliwe kuwa walishindwa kazi.

Watendaji wote waliokuwemo kwenye Sekretarieti iliyopita wameondolewa isipokuwa Makamba anayeendelea kuwa Katibu Mkuu. Waliondolewa ni Naibu Katibu Mkuu, Jaka Mwambi, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Aggrey Mwanri na Mweka Hazina, Rostam Aziz.

Awali, taarifa zilisambaa kwamba Rostam alikuwa amejiuzulu nafasi hiyo kutokana na shughuli zake za biashara, lakini alipoulizwa alisema kuondolewa kwake ni uamuzi wa Mwenyekiti wa chama.

Katika sekretarieti mpya, Naibu Katibu Mkuu anakuwa Mbunge wa Newala, Kapteni George Mkuchika, Uchumi na Fedha imechukuliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana, Amos Makalla, Itikadi na Uenezi anakuwa Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Kapteni John Chiligati na Katibu wa Siasa na Mambo ya Nje ni Benard Membe, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa.


Upande wa Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu, Ramadhan Saleh Feruzi, anaendelea na wadhifa huo.

Wajumbe Kamati Kuu ni Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, Mbunge wa Viti Maalum, Pindi Chana, Naibu Spika wa Bunge, Anna Makinda, Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, Mbunge wa Handeni, Dk Abdallah Kigoda, Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.

Majina mengine yaliyodondoshwa upande wa Bara ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Guninita John Guninita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Adam Kimbisa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, William Kusila, Dk Rehema Nchimbi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Mizengo Pinda na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira.

Upande wa Zanzibar waliopitishwa ni Waziri Kiongozi mstaafu, Dk Gharib Bilal, Naibu Waziri Miundombinu, Dk Maua Daftari, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Muhammed Seif Khatib, Fatma Saidi Ali, Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Omar Yusuf Mzee na Waziri wa Biashara, Viwanda na Utalii, Samia Suluhu Hassan.

Waliokuwa wamependekezwa na kudondoshwa ni Mwajuma Majid Abdallah, Ali Mzee Ali, Machano Othman Saidi, Salim Hamad Saleh, Usi Yahya Haji, Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansoor Yusuf Himid, Haroun Ali Suleiman na Hamad Masauni Yusuf.

Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Mwenyekiti anatakiwa kupendekeza majina yasiyozidi 30, majina 15 kutoka kila upande wa muungano; ili yachaguliwe majina saba kutoka kila upande na miongoni mwa watakaochaguliwa wanawake wasipungue wawili.

Kulingana na Katiba ya CCM, Mwenyekiti wake anaruhusiwa kuchagua wajumbe 10 kuingia kwenye NEC. Walioteuliwa ni Mawaziri Wakuu mstaafu, Cleopa David Msuya na Salim Ahmed Salim.

Msekwa alisema, Rais Kikwete alisema hakuteua kujaza nafasi zote kwa sababu anaendelea kuangaza wengine wanaoweza kumsaidia.

Pia, Rais Kikwete alisema kikao cha halmashauri kuu kijacho kitafanyika Butiama, Mara kwa ajili ya kumuenzi Baba wa Taifa, Marehemu Mwalimu Julius Nyerere na kwamba maandalizi ya kikao hicho yatafuatiliwa kwa karibu na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono.
 
Back
Top Bottom