Katibu Mkuu Nchimbi, zuia walioanza kampeni mapema ndani ya chama chako kabla ya muda

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,103
22,551
Salaam, Shalom!!

Hongera kwa kuaminiwa na chama chako kwa nafasi ya Katibu Mkuu.

Kuna vurugu na wimbi linaendelea la watu ndani ya chama chako kuanza compaign mapema Kwa GIA ya kuchangishana na kuwachukulia fomu wagombea wa nafasi mbalimbali, Hasa ubunge na Ile ya juu zaidi ilhali muda Bado, taratibu na KANUNI za chama zinakinzana na jitihada hizo.

Umejinasibu ni mtu wa misimamo, waonye hadharani waache mara Moja, wasiposikia WAKATWE Majina Yao huko mbeleni.

Karibuni 🙏
 
Kwa nini mnaziogopa kampeni si ndo zinajemga chama.

Kuna mtu tukiwa bado tunafuta machozi na vitambaa mikononi yeye akawa anasema hizi ni homa za 2025.
 
Kwa nini mnaziogopa kampeni si ndo zinajemga chama. Kuna mtu tukiwa bado tunafuta machozi na vitambaa mikononi yeye akawa anasema hizi ni homa za 2025.
Utaratibu na KANUNI zinasemaje?
 
Azuie na kampeni za kumrudisha mama?

Yeye mwenyewe kishaanza kampeni kumkampenia mama atapata wapi guts kuzuia wengine ?
 
Azuie na kampeni za kumrudisha mama?

Yeye mwenyewe kishaanza kampeni kumkampenia mama atapata wapi guts kuzuia wengine ?
KANUNI za chama zinaruhusu vikundi mbalimbali kuchangisha Fedha hadharani kumchukulia fomu mgombea Kwa nafasi ambayo Bado haijatangazwa na chama?
 
Zinasema Chukua Chako Mapeeemaaa,

Acha wachukie vyao Mkuu.
Amejinasibu ni mtu wa misimamo,

Asome KANUNI na taratibu za chama waziwazi ikiwa jambo Hilo linalofanyika ni halali au haramu!!
 
Salaam, Shalom!!

Hongera Kwa kuaminiwa na chama chako Kwa nafasi ya KM.

Kuna vurugu na wimbi linaendelea la watu ndani ya chama chako kuanza compaign mapema Kwa GIA ya kuchangishana na kuwachukulia fomu wagombea wa nafasi mbalimbali, Hasa ubunge na Ile ya juu zaidi ilhali muda Bado, na KANUNI zinakinzana na jitihada hizo.

Umejinasibu ni mtu wa misimamo, waonye waache mara Moja, wasiposikia WAKATWE huko mbeleni.

Karibuni
Aanze kwa kumkemea m/kiti wake aliyekaa kimya baada ya wakuu wa shule za sekondari kujikomba na kuchangishana fedha kwa ajili ya fomu yake ya kugombea Urais kabla ya muda.
 
Ha
Aanze kwa kumkemea m/kiti wake aliyekaa kimya baada ya wakuu wa shule za sekondari kujikomba na kuchangishana fedha kwa ajili ya fomu yake ya kugombea Urais kabla ya muda.
Hayo ndo madhara ya kofia mbili za mkt.

Mkt anaruhusiwa kugombea kupitia kofia ingine, jambo ambalo KM hawezi.
 
Marekani uchaguzi unafanyika December mwaka huu ila watu walishaanza kampeni tangu mwaka jana, hili Nchimbi anapaswa kuliiga.
 
Marekani uchaguzi unafanyika December mwaka huu ila watu walishaanza kampeni tangu mwaka jana, hili Nchimbi anapaswa kuliiga.
Kwa vyanzo vipi vya mapato tulivyonavyo?
 
Salaam, Shalom!!

Hongera Kwa kuaminiwa na chama chako Kwa nafasi ya KM.

Kuna vurugu na wimbi linaendelea la watu ndani ya chama chako kuanza compaign mapema Kwa GIA ya kuchangishana na kuwachukulia fomu wagombea wa nafasi mbalimbali, Hasa ubunge na Ile ya juu zaidi ilhali muda Bado, taratibu na KANUNI za chama zinakinzana na jitihada hizo.

Umejinasibu ni mtu wa misimamo, waonye hadharani waache mara Moja, wasiposikia WAKATWE Majina Yao huko mbeleni.

Karibuni
MKOA WA RUKWA Utadhani UCHAGUZI ni mwezi wa 10 Mwaka 2024 kwani hata VIONGOZI wa Chama wanawasaidia Walioanza kampeni mapema Jimbo la NKASI na Kwela Wanachama Wasiotii Utaratibu wa Chama wapo vijijini Wanapiga kampeni hata MAJINA yao tunayo

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Hilo ni jambo zuri sana linalopaswa kuigwa na maeneo mengine yote.
 
Ha
Hayo ndo madhara ya kofia mbili za mkt.

Mkt anaruhusiwa kugombea kupitia kofia ingine, jambo ambalo KM hawezi.
Basi akae na atulie campaign kaianza yeye mapema kabla ya wakati. Lakini hata yeye mwenyewe anapaswa kupitia mchakato uleule walioupitia wenzake kipindi wakigombea Urais kwa mara ya kwanza. Hii aliyopo alidandia tren ikiwa kwenye mwendo.
 
Utaratibu na KANUNI zinasemaje?
Huo utaratibu wanaosema wamejiwekea wenyewe Mbona hauko kwenye katiba yao?
Huo utaratibu ni applicable kwa Rais aliyechaguliwa na watu na sio aliyerithi kiti!! Samia anatakiwa ashondanishwe na wengine ili apatikane mshindi wa kupeperusha bendera yenu.
 
Ni Kweli kabisa. Ikiwa anatosha, akubali changamoto, ashindanishwe, apigiwe kura nk nk!!
 
Back
Top Bottom