Emmanuel Nchimbi anafaa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, anaweza kujenga chama, kudhibiti nidhamu ya chama, akiwemo yule bwana mdogo

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,003
20,662
Emmanuel Nchimbi ni mwanasiasa anayemudu mapambano, anayejua historia ya chama na misingi yake.

Kwa kujenga chama na kuondoa makundi, ni yeye pekee ndiye ana uwezo mkubwa wa kuishika vilivyo nafasi hiyo. Ni fundi wa mikakati, na Siasa za saiti, hata ikibidi Siasa za mapambano.

Namshauri SSH amteue Emmanuel Nchimbi, ni chaguo Bora.

Nchimbi amepambana na wanasiasa wahuni ndani ya chama, na hatashindwa kupambana na wahuni wengine ambao wamepenyapenya kwenye chama na kupata vinafasi.

Screenshot_20231127-080408_1.jpg

Pia soma: Breaking News: - Dkt. Emmanuel Nchimbi ateuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM
 
Emmanuel Nchimbi ni mwanasiasa anayemudu mapambano, anayejua historia ya chama na misingi yake.

Kwa kujenga chama na kuondoa makundi, ni yeye pekee ndiye ana uwezo mkubwa wa kuishika vilivyo nafasi hiyo. Ni fundi wa mikakati, na Siasa za saiti, hata ikibidi Siasa za mapambano.

Namshauri SSH amteue Emmanuel Nchimbi, ni chaguo Bora.

Nchimbi amepambana na wanasiasa wahuni ndani ya chama, na hatashindwa kupambana na wahuni wengine ambao wamepenyapenya kwenye chama na kupata vinafasiView attachment 2828195
Labda wewe bado mtoto, EN gani unayesema ataunganisha makundi? Huyuhuyu 2015 alikuwa na kundi lake baada ya Lowassa kukatwa alitoka na kundi lake wakaenda nje ya ukumbi na kuanza kuimba...
"Tunaaaaaaani na Lowaaaaaasaaaaa!"
Leo unasema hana makundi? Wako pamoja na Sophia Simba etc.
 
Uteuzi usitokee humu Jamii forum ndiyo makosa yanayofanyika wacha TISS na vetting itumike na Mwenyekiti ajipe muda, ushawishi wa humu jamii kwenye uteuzi ni fake na hawa mara Nchimbi mara nani wanatumiwa na watu wao. CCM tuwe makini. CCM ina hazina kubwa mno ya viongozi,tusikurupuke tena kwa majina makubwa yanayopenyezwa na machawa.
 
Emmanuel Nchimbi ni mwanasiasa anayemudu mapambano, anayejua historia ya chama na misingi yake.

Kwa kujenga chama na kuondoa makundi, ni yeye pekee ndiye ana uwezo mkubwa wa kuishika vilivyo nafasi hiyo. Ni fundi wa mikakati, na Siasa za saiti, hata ikibidi Siasa za mapambano.

Namshauri SSH amteue Emmanuel Nchimbi, ni chaguo Bora.
Naunga mkono hoja, this is the right man!, the right choice!.
P
 
Back
Top Bottom