KATIBA MPYA: Umri wa Rais uwe kuanzia miaka 30

Pointi IPI?
Tatizo
Point ipi Kijana?

Tatizo una sample vijana unaowawaza wewe binafsi kwa mtazamo wa taifa huko ni kujidanganya. Ukweli ni huu; wapo vijana smart sana tatizo mfumo huu mbovu tulio nao rafiki.
Kindly nitajie mmoja
 
Acheni utoto.

Ina maana hii nchi kabla ya Nyerere Kambarage Julius kuwa Rais / Waziri Mkuu viongozi waliokuwa machifu au watemi walikuwa wazee wa huo umri?

Hawa wazee wamejitengenezea pension center tu hakuna usahihi au ukweli wowote kuwa Urais umri mkubwa ndio kigezo.
 
Na pia napendekeza Mabalozi wa Taifa letu wateuliwe kuanzia miaka 23 na kuendelea.

Itapendeza Rais kijana, Mawaziri vijana na N .Mabalozi vijana.
Sipatii picha stori za weekend j3
Huyu anahadithia za maison mwingine kidimbwi
 
Utoto?

Machifu/Watemi walichaguliwa na nani? Unazungumzia mfumo upi?

Sasa kama hivi, huweki hoja, unaweka kejeli. Umri unaweza kuchuja haya ingawa si lazima. Msela pia hapewi nchi, sababu za msingi zipo pia.

Uzuri ni kuwa, hutabaki na mawazo hayo hayo miaka michache ijayo Mungu akijaalia uhai na uzima.
 
Uzuri nimependekeza KATIBA MPYA itambue umri wa Rais ni kuanzia miaka 30.

Wewe kama CCM au CHADEMA ukiona umri mkubwa ndio unaofaa hupingwi kwa chochote na sioni haja au hoja ya ninyi kunipinga.

Unajua wazee wengi hawataki mabadiliko hususani walio kwenye vyama vya siasa na vyama vinavyoendana na hayo mambo.

Nimeamua kutoa hoja ya Machifu/ Watemi sababu kuu ni kuwa mfumo wa kumpata Rais umekopwa kutokea huko kwa hao Machifu/ Watemi; Rais hachaguliwi bali anateuliwa na watu wachache kwa niaba ya wengi mfanano na mfumo uliopo Tanzania.

Umri wa Urais uendelee kuwa kuanzia miaka 30 na kuendelea.
 
Au sio Tanganyika ilipata Uhuru ulioandikwa kwenye vitabu 1961; kwa haki na kweli si sahihi mwaka tajwa.
Nilikuwa najaribu kutoa justification ya umri wa Hayati JK Nyerere kuanza kuwa Rais manake niiliona kuwa jamaa la Chadema lilikuwa linapotosha kuwa Nyerere alianza kuwa Rais akiwa na miaka 30
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…