Omusolopogasi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2017
- 7,105
- 18,005
Wana-CHADEMA,
Mwenyekiti wenu alikamatwa usiku wa kuamkia kongamano la katiba mpya kule Mwanza akiwa na wanachama na viongozi wengine. Tangu akamatwe, habari ya kongamano imekufa!
Kwa sababu serikali inasema imemkamata kwa sababu nyingine na wala siyo suala la katiba mpya, kwa nini viongozi wengine waliobaki wa CHADEMA wasiendelee na kongamano? Vinginevyo inaonekana kuwa lilikuwa ni kongamano la Mbowe tu. Na kila kutapokuwa na vuguvugu lolote, Mbowe atakuwa anakamatwa ili kulizima. Inaonekana Mbowe akikamatwa tu, kila kitu kinaishia hapo! Na hii inahamasisha serikali kuendelea kumshikilia Mbowe.
Katibu Mkuu wa CHADEMA - John Mnyika - na viongozi wengine - Tundu Lissu - mnalionaje hili? Kunyamaza kwenu kunam-expose Mbowe kama the sole instigator. Inaonekana Mbowe alikuwa anawaburuza juu ya hili. Serikali imekwisha sema katiba mpya siyo sababu. Kwa nini sasa kondamano lisiendelee?
Angekamatwa Mandela na akina Winnie, Thabo, Zuma...wakaamua kukaa kimya, leo hii pengine bado kungekuwa na White minority rule na ubaguzi Afrika Kusini.
Tafakarini, na chukuweni hatua.