Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,582
- 113,785
Wanabodi,
Hizi kelele za wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kuhusu hii IGA ya DPW na Bandari zetu, sio za kuzipuuzia!. Katiba hii mbovu tuliyonayo!, Sheria zetu mbovu tuliyonayo, mikataba mibovu ya kimataifa tunayoingia, mwisho wa siku tunajikuta tumepigwa!, tunafunguliwa mashitaka, tunashindwa, tunapigwa tozo za mabilioni ya fedha!, ambazo ni lazima tulipe.
Haya yote ni matokeo ya kazi ya wanasheria wabovu na baadhi yao vilaza!. Leo nimeianza siku kwa bad news kutoka Marekani, Tanzania tumeshindwa kesi, tunadaiwa tozo ya dola za Marekani zaidi ya Millioni 100!, na lazima tulipe!.
Soma taarifa hii hapa chini
Paskali

- Kama Tanzania tulipitisha sheria kuwa kwenye uwekezaji hakuna mashauri yoyote ya nje ya nchi!. Mashauri yote ni hapa nchini kutumia sheria za Tanzania!, sasa haya mashauri yanaendelea vipi kupelekwa nje?.
- Hii maana yake ni ama tuna sheria mbovu, ama tuna wanasheria wabovu wanaotunga sheria mbovu, zinazotupa mikataba mibovu, na mwisho wa siku tunaishia kupigwa na kutozwa matozo ya ajabu ajabu!.
- Huku kila siku kushindwa kesi za kimataifa na kupigwa tozo nako ni ama tuna sheria mbovu za mikataba mibovu ama kama sheria ni nzuri, then tuna wanasheria wabovu wasio na uwezo wa kushauri the right thing to do!, hivyo serikali yetu inavunja mikataba kitutusa na mwisho wa siku tunaishia kuumizwa kwa kushindwa kesi na kupigwa tozo!.
- Kabla ya kuvunja mkataba wowote, serikali yetu inaomba ushauri wa kisheria kufanya kitu kinachoitwa mitigation, wanasheria hawa huishauri vibaya serikali yetu, mwisho wa siku, tunaishia kuumizwa!.
- Issues ya Richmond, Dowans, tukaunda tume, ikatoa matokeo kwa mbwembe kuwa Richmond ni kampuni hewa hata tukivunja mkataba, hatutashitakiwa popote!.
- Tukamfanya Edward Lowassa ni mbuzi wa kafara, tukavunja mkataba!.
- Tukashitakiwa tukashindwa, tukapigwa tozo!. Waliotushauri tuvunje mkataba wakajiapiza "over my dead body!, hatulipi". Tulilipa kisiri siri every cent!. Hawa wanasheria walifanywa nini?
- Mitambo ya Richmond ikanunuliwa na Simbion, tukaingia nao mkataba ule ule na tukawalipa!.
- Chuma JPM, alipoingia tukavunja mkataba wa Simbion, tukashitakiwa, tukashindwa, tukapigwa tozo, Chuma JPM, akagoma hatulipi!
- Mama kaingia, tumelipa fasta fasta, kimya kimya!. Wanasheria waliotufikisha hapa walifanywa nini?!.
- Tulipotunga sheria mbovu, watu humu tulishauri Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts?, leo baada ya kutuletea hii IGA mbovu, watu tumeeleza matatizo yake kibao!.
- Wanasheria hawa hawa, Bunge letu hili hili wanaipitisha hivyo hivyo ilivyo, wanaiambia serikali yetu hii IGA ni nzuri, safi na haina matatizo yoyote!.
- Wanasheria hawa wanao tufikisha hapa, tukiwaita ni wanasheria wabovu au vilaza, itakuwa ni kuwaonea?.
- Tanzania tutaendelea kufanywa shamba la bibi na kichwa cha Mwendawazimu na wanasheria wabovu na vilaza wa aina hii hadi lini?!.
Paskali