Kati ya tecno cammon 16 primier vs oppo a93 Ipi bora?

Kati ya tecno cammon 16 primier vs oppo a93 Ipi bora?

Amanijua

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2014
Posts
1,776
Reaction score
1,636
Guys habari za kazi?

Naombeni ushauri wa kitaalamu.

Nahitaji kununua simu bajeti yangu ni laki 6..

Katika pita pita zangu nimeona hizi simu 2 ambazo bajeti yangu inaendana nazo:

Ni ipi nichukue kati ya hizo au kama kuna simu nzuri zaidi itakayoweza kuendana na bajeti yangu nipeni mwongozo.

Nipo mwanza.
 
Camon 16 premier ina uwezo mzuri kdgo kuliko Oppo A93 kwenye processor na ina 90hz refresh rate. Lakini Oppo A93 ina amoled screen ambayo inakuwa na quality kubwa zaidi. Sema kwenye oppo utapata updates za kupandisha android version na hyo tecno itabaki na hyo hyo android 10 yake, labda wa update kwenda android 11. Lakini sio uhakika.

Mm binafsi ningechukua hyo Oppo. Ila kuna xiaomi redmi note 10 imetoka juzi juzi hapa. Uwezo wake ni mzuri pia na ni 450,000 aliexpress. Or redmi note 10 Pro ambayo inazizidi hzo simu zote hapo sana kwa laki 7.
 
Mkuu Go for Galaxy A52, much better kuliko zote mbili. Ama nunua Redmi note 10 kama alivyo shauri mdau hapo juu.

A52 Nimecheki online kwa hapa Tanzania hadi laki 7 unapata, I hope madukani inaweza kuwa rahisi zaidi, ila hata kwa hio laki 7 compare na hizo mbili ni simu nzuri zaidi.

Kwa A52 utapata camera kali yenye Ois kitu ambacho huwezi kikuta midrange za kichina, ni water proof ip67, kioo kizuri cha Amoled, perfomance pia si Haba sd 720G inapita zote hizi.

Helio G90T kwenye Camon haina thamani ya laki 6, mfano Xiaomi Alii tumia toka 2019 na Bei yake ilikuwa ni chini ya laki 5, same kwa hio OPPO P95 pia ni soc ya kizamani. Plus ni mediatek.
 
Mkuu Go for Galaxy A52, much better kuliko zote mbili. Ama nunua Redmi note 10 kama alivyo shauri mdau hapo juu....
A52 nilicheki kwenye maduka mtaani huku nikaona inacheza kwenye 750k mpka 850k
 
Na vipi kati ya samsung galaxy a21s na infinix note 8i ipi ipo mkini kwa kutumika
Chukua samsung hyo kwasabab ya software. Software ya samsung ni bora mara 100 kuliko ya infinix. Infinix sikuhz zina ads hadi kwenye homescreen ni balaa.
 
A52 nilicheki kwenye maduka mtaani huku nikaona inacheza kwenye 750k mpka 850k
Hata online kuna watu wanauza hivyo,

Sema huyu kama tapeli

Ila ni simu mpya ndo imeingia, ndo wakati wa kuchanganya wateja huu.
 
Hata online kuna watu wanauza hivyo,

Sema huyu kama tapeli

Ila ni simu mpya ndo imeingia, ndo wakati wa kuchanganya wateja huu.
A52 tena ya 5G auze kwa laki 7? Hao si wale jamaa wanaweka picha za simu OG alafu ukienda kuchukua unakuta ni simu feki imewekwa kwenye box la OG. Ila huwezi jua maana nilishawahi bahatisha pixel 3a kwenye box kwa laki 4 na nusu hvi
 
Mkuu "soc" ni nini ningependa kujua
SOC - System on chip. Ni integrated circuit yenye components mbali mbali.

Mtu akisema SOC anamaanisha processor ya simu kiujumla. Kwakua simu sikuhzi processor chip yake inakua na graphics chip, processor yenyew, modem kwaajili ya network na mambo mengine huwa wanaiita SOC.
 
A52 tena ya 5G auze kwa laki 7? Hao si wale jamaa wanaweka picha za simu OG alafu ukienda kuchukua unakuta ni simu feki imewekwa kwenye box la OG. Ila huwezi jua maana nilishawahi bahatisha pixel 3a kwenye box kwa laki 4 na nusu hvi
Wameandika mkoani wanatuma, probably matapeli wa online, ila box halijaandikwa 5g, kuna watu wa najua A52 zote ni 5g.
 
Mkuu "soc" ni nini ningependa kujua
Kama Alivyo sema mdau simu haiji na processor, gpu, modem, wifi kivyake vyake kama computer, Bali vinakuja kwenye package moja inaitwa soc.

Ukitoa processor, gpu na modem pia soc hujumlisha
-encoder na decoder za video hapa ndo unakuta simu ina play kila video, mp4, avi, mkv etc
-Isp za camera,
-Npu kwa ajili ya Artifical intelligence
-wifi
-bluetooth
-memory controller kwa ajili ya ram na storage etc.

Kifupi mkuu ukikosea kuchagua soc umeshakosea kuchagua simu maana hata mambo yaliyobakia hayawezi ku compensate,

Mfano simu imewekwa camera kali lakini soc ni mbaya ina maana Isp itakuwa ndogo na ile camera haitapiga picha vizuri na picha haitatoka vizuri.

Vice versa pia ni kweli, unaweza kuta simu ya kichina camera wala sio nzuri ila soc yake nzuri, hivyo watu wanaweka Gcam, ile Gcam inachukua advantage ya Isp nzuri ya soc na kutoa picha nzuri.

Isp ni kifupi cha image signal processor,
 
Chukua samsung hyo kwasabab ya software. Software ya samsung ni bora mara 100 kuliko ya infinix. Infinix sikuhz zina ads hadi kwenye homescreen ni balaa.
Hivi hakuna ya kuzistop hizo add
 
Hivi hakuna ya kuzistop hizo add
Unaweza badilisha launcher ya simu. Ingia playstore tafta nova launcher na install hyo kitu. Itaondoa hyo takataka ya infinix kwenye homescreen na hakuna ads tena
 
Back
Top Bottom