Kati ya Jasusi na Commando, yupi ni mtu hatari sana anayepaswa kuogopwa?

Commando hua akizingua anatumwa jasusi kumaliza show, ila jasusi akizingua hua anatumwa jasusi mwingine mwenye skills ambazo ziko tofauti na alizojifunza yeye

Kuna mauaji yakijasusi yalifanyika huko marekani ambayo mpaka leo hawajajua nini kilichomuua yule jasusi

Mtu alikutwa amefariki kwenye begi dogo la nguo, baada ya kufanya utafiti wakagundua begi hilo limefungwa na zipu iliyopo ndani yake, yaani ni kama yule marehemu aliingia mwenyewe kwenye begi halafu akajifungia kwa ndani na zipu ya ndani ya begi, watafiti walijaribu kufanya research pengine kulikua na mtu aliyekua anagombana nae lakini hawakuweza kupata ushahidi wowote ambao ungeonesha harakati za marehemu kupambana dhidi ya adui, napia walijiuliza hata kama kulikua na mtu aliemuingiza humu kwenye begi je zipu iliyopo ndani ya begi aliifunga vipi?

cctv camera zilikuwepo lakini hakuna tukio lolote ambalo ziliweza kunasa. Walichukua vipimo kwenye ule mwili kubaini pengine labda jamaa alikufa kwa kukosa pumzi baada ya kujifungia kwa muda mrefu ndani ya begi lakini walikosa uthibitisho huo

Madaktari walijaribu kupima huenda jamaa alipewa sumu lakini mwili wake haukuonesha dalili yoyote ya sumu wala tatizo lolote

Daktari mmoja ambaye mwili wake ulikua unafanana na marehemu alijaribu kuingia kwenye lile begi pamoja na jopo la watu wakijaribu kumsaidia lakini ilishindikana yaani hakutosha kuenea kwenye lile begi

Jamaa alizikwa lakini hakuna aliyeweza kujua nini kilichomuua

Sasa angekua commando ndio ametumwa kutekeleza mauaji hayo angeshikwa kiboya sana kwasababu hayanaga akili zaidi ya miguvu

Sent using unknown device
JF bhana,commando hama akili sio anatumia nguvu ah ah ah,hivi humu mna refer macommando wa wapi hao

Sent using Brain
 
Wengi wanajibu tu ilimradi amejibu au anatumia uelewa wake tu kujibu, kwa ufupi Sana naomba nieleze kidogo,
Komando Ni mwanajeshi wa cheo chochote alifuzu mafunzo maalumu, komando Ni jeshi kamili( single army unity) pia Ni ukamilifu( full package) yeye lazima afuzu mafunzo ya military intelligence, martial& combat karate, air, infantry and navil( SEAL), anauwezo wa kupeleleza, kushambulia, kupigna, kuteka, kuokoa mateka n.k komando kutokana na uwezo huo huweza kutumika na taasisi mbalimbali za kijasusi

Jasusi Ni mtu anayejifunza kutafuta, kufatilia, kutathmini, kuandaa taarifa fulani au tukio fulani!! Ktk kazi ya ujasusi vyote hutumika nguvu na akili pia japo ndani ya ujasusi Kuna vitengo vingi Sana, vipo mahususi kwa kukusanya data, kufatilia data, kuua, kupoteza ushahidi n.k hivyo jasusi lazima apate basic ya physical training( martial arts and combat karate)
Ujasusi upo sehemu zote jeshini na uraiani,. Lakini komando Ni special force ndani ya jeshi !!
Upo wakati TISS huhitaji msaada was komando na pia huhitaji military intelligence lkn jeshi huwa halihitaji msaada wa TISS !!!! Kwa ufupi Sana naomba niishie hapa zaidi tunaweza vuka mipaka
Hatimae mkuu umetoa jibu sahihi..wengi huko juu wametiririka imaginations zao tu.
Shukrani chief, ulipoishia panatosha kabisa

Sent using Brain
 
Si kila Commando ni Jasusi lakini kila Jasusi ni Commando. Nadhani ushapata jibu lako hapo.
Sidhani kama hii ni kweli. Inategemea mazingira ya ujasusi. Kwa mfano yule jasusi aliyeiba siri za nuclear Marekani zikaenda Russia hakuwa na background ya askari. Yeye alikuwa msomi aliyebobea. Hata sisi hawa wazee wenye vipara wanafanya research, could be very dangerous
 
Guys!

Mnasemaje?! Ndugu yangu Malcom Lumumba... long time no see brother from another mother; na mdogo wako Wick; hivi mchecheto walionao FBI dhidi ya Russia ni hofu dhidi ya Makomando wa Russia au hofu dhidi ya Majasusi wa Russia, especialy Illegals alias Non-Official Cover Agents (as used by CIA)?!

Acha Jasusi aitwe Jasusi!! Nchi zote duniani hujilinda dhidi ya Majasusi kutoka nchi adui na sio Makomando kutoka nchi adui!!!

Leo hii taifa adui likiamua kuua rais wa nchi adui yake, watakachofanya ni kutanguliza majasusi kuchora mchezo mzima!

Kutegemeana na aina ya ulinzi na time to mission execution, Majasusi wanaweza kumaliza mchezo kimyakimya au Makomando wanaweza kutumika baada ya Majasusi kuwa wameshafanya kazi ya awali!!!

Vifo vyote visivyoeleweka duniani vinafanywa na majasusi!

ISIS wakivutiwa na roho ya Papa Francis (God Forbid) hawatatumia Makomandoo hata kama wangekuwa nao bali watatumia Majasusi... tena usishangae Majasusi wenyewe wakawa wapo pale kama Masister!!

US wakiitamani roho ya Vladimir Putin, hawatatumia Makomandoo bali watatumia Majasusi!

Hawa hawatumii nguvu bali akili tu ingawaje haimaanishi Makomandoo wanatumia zaidi nguvu kuliko akili!

Mnakumbuka ambacho Majasusi wa Mossad walikifanya kwa Wadie Haddad, Mastermind wa utekaji wa ndege ya Israel iliyokuwa inaelekea Paris (From Operation Entebbe Saga)?!

Pamoja na ujanja wake wote lakini Haddad alikuja kufa kwa ugonjwa wa leukemia uliotokana na kula biskuti ambazo Majasusi wa Mossad walizifanyia mambo!!!

Kwanza, kabla ya kifo chake, kila hospitali aliyoenda alionekana hana tatizo wakati mtu alikuwa anateketea huku akijiona!!!

Na hata uhusika wa Mossad kwenye kifo cha Haddad ulikuja kufahamika miaka mingi baadae na kabla ya hapo, ilionekana tu amekufa kwa ugonjwa wa kushangaza huku kila mmoja akisema lake ingawaje kama ilivyotarajiwa, wengi waliionyeshea kidole Mossad lakini hapakuwa na ushahidi!!!

Na tusisahau, ingawaje ni Makomando wa IDF ndio walifanya rescue mission lakini hayo yalifanyika baada ya Mossad kukamilisha kazi yao!!

Hao ndio Majasusi!!!

Hata kwenye military zone, ni lazima Majasusi ndio hutangulia... of course, hawa watakuwa ni Military Intelligence Officers!

Huwezi tu kutanguliza Makomando eti kwa sababu tu wanaweza kuua hata kwa kutumia kidole! Pasipo na intelligence ya kutosha, wanaweza kuuawa kama kuku pamoja na ukomando wao!!!

Use'nge zaidi, wanaweza kuuawa hata na Jasusi wa Kike aliye na military training ya kawaida kabisa kwa sababu kama nilivyosema hapo awali, Jasusi anatumia nguvu only when the operation goes south!

Tatizo la Majasusi ni moja!! Wanaweza kutumika hata majasusi 10 only to eliminate Bashite asiye na military training yoyote! Na hii ni kwa sababu huwa hawataki kuacha alama!! Matokeo yake, mission planning to execution huwa inachukua muda mrefu!!

Sasa wakati wanaweza kutumika Majasusi hata 10 just to eliminate Bashite, upande wa Makomando anaweza kutumika mmoja tu atakayevamia hata ofisini, ambapo wala usishangae baada ya kukamilisha mission akaanza kufukuzwa barabarani na raia baada ya mchezo kugundulika kabla hajapotea eneo la tukio!!

Itoshe tu kusema kwamba, Commando anaogopeka wakati wa vita ili hali Jasusi anaogopeka hata wakati wa kufungua champagne!!
 
Sidhani kama hii ni kweli. Inategemea mazingira ya ujasusi. Kwa mfano yule jasusi aliyeiba siri za nuclear Marekani zikaenda Russia hakuwa na background ya askari. Yeye alikuwa msomi aliyebobea. Hata sisi hawa wazee wenye vipara wanafanya research, could be very dangerous
You're 100% Right!!!
 
Guys!
Mnasemaje?! Ndugu yangu Malcom Lumumba... long time no see brother from another mother; na mdogo wako Wick; hivi mchecheto walionao FBI dhidi ya Russia ni hofu dhidi ya Makomando wa Russia au hofu dhidi ya Majasusi wa Russia, especialy Illegals alias Non-Official Cover Agents (as used by CIA)?!

Mimi nimefurahi sana kukuona ndugu yangu, natumai unaendelea vizuri huko uliko.
 
Kuna tofauti kubwa kati tya JASUSI na KOMANDO. Jasusi ni mtu aliyefundishwa kukutafuta, kuchambua, kuandika, kutathmini taarifa za kiusalama. Pili kuzitumia taarifa za kiusalama kwa manufaa ya mfadhili wake. Ni kazi inayohitaji uwezo mkubwa wa akili ili kujua taarifa ipi ni ya kiusalama na yenye faida kwa mfadhili na nchi. Uwezo wa kuzitumia kwa manufaa na nani anafaa kutumiwa kwa kujua au kutojua.

Komando ni mtu aliyepitia mafunzo maalum (ndo maana USA wanaitwa WANAJESHI MAALUM - Special Force). Kazi yake kuu ni kufanyakazi ngumu zinazohitaji taaluma maalum. Mara nyingi huenda sehemu wakiwa tayari na taarifa kamili toka kwa Jasusi!

Komando lazima mafunzo yawe magumu (physically) ilhali kwa Jasusi sio lazima. Mafunzo ya Jasusi ni magumu (Mentally) ilhali Komando hapana. Jasusi anafundishwa tu kujimudu kutoka msombweni pindi mambo yakichacha. Komando ni ufunguo wa kuyafungua matatizo.

Naamini Nimeeleweke

Bazazi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kula ka like kangu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Guys!

Mnasemaje?! Ndugu yangu Malcom Lumumba... long time no see brother from another mother; na mdogo wako Wick; hivi mchecheto walionao FBI dhidi ya Russia ni hofu dhidi ya Makomando wa Russia au hofu dhidi ya Majasusi wa Russia, especialy Illegals alias Non-Official Cover Agents (as used by CIA)?!

Acha Jasusi aitwe Jasusi!! Nchi zote duniani hujilinda dhidi ya Majasusi kutoka nchi adui na sio Makomando kutoka nchi adui!!!

Leo hii taifa adui likiamua kuua rais wa nchi adui yake, watakachofanya ni kutanguliza majasusi kuchora mchezo mzima! Kutegemeana na aina ya ulinzi na time to mission execution, Majasusi wanaweza kumaliza mchezo kimyakimya au Makomando wanaweza kutumika baada ya Majasusi kuwa wameshafanya kazi ya awali!!!

Vifo vyote visivyoeleweka duniani vinafanywa na majasusi! ISIS wakivutiwa na roho ya Papa Francis (God Forbid) hawatatumia Makomandoo hata kama wangekuwa nao bali watatumia Majasusi... tena usishangae Majasusi wenyewe wakawa wapo pale kama Masister!! US wakiitamani roho ya Vladimir Putin, hawatatumia Makomandoo bali watatumia Majasusi!

Hawa hawatumii nguvu bali akili tu ingawaje haimaanishi Makomandoo wanatumia zaidi nguvu kuliko akili! Mnakumbuka ambacho Majasusi wa Mossad walikifanya kwa Wadie Haddad, Mastermind wa utekaji wa ndege ya Israel iliyokuwa inaelekea Paris (From Operation Entebbe Saga)?!

Pamoja na ujanja wake wote lakini Haddad alikuja kufa kwa ugonjwa wa leukemia uliotokana na kula biskuti ambazo Majasusi wa Mossad walizifanyia mambo!!! Kwanza, kabla ya kifo chake, kila hospitali aliyoenda alionekana hana tatizo wakati mtu alikuwa anateketea huku akijiona!!! Na hata uhusika wa Mossad kwenye kifo cha Haddad ulikuja kufahamika miaka mingi baadae na kabla ya hapo, ilionekana tu amekufa kwa ugonjwa wa kushangaza huku kila mmoja akisema lake ingawaje kama ilivyotarajiwa, wengi waliionyeshea kidole Mossad lakini hapakuwa na ushahidi!!!

Na tusisahau, ingawaje ni Makomando wa IDF ndio walifanya rescue mission lakini hayo yalifanyika baada ya Mossad kukamilisha kazi yao!!

Hao ndio Majasusi!!!

Hata kwenye military zone, ni lazima Majasusi ndio hutangulia... of course, hawa watakuwa ni Military Intelligence Officers! Huwezi tu kutanguliza Makomando eti kwa sababu tu wanaweza kuua hata kwa kutumia kidole! Pasipo na intelligence ya kutosha, wanaweza kuuawa kama kuku pamoja na ukomando wao!!! Use'nge zaidi, wanaweza kuuawa hata na Jasusi wa Kike aliye na military training ya kawaida kabisa kwa sababu kama nilivyosema hapo awali, Jasusi anatumia nguvu only when the operation goes south!

Tatizo la Majasusi ni moja!! Wanaweza kutumika hata majasusi 10 only to eliminate Bashite asiye na military training yoyote! Na hii ni kwa sababu huwa hawataki kuacha alama!! Matokeo yake, mission planning to execution huwa inachukua muda mrefu!!

Sasa wakati wanaweza kutumika Majasusi hata 10 just to eliminate Bashite, upande wa Makomando anaweza kutumika mmoja tu atakayevamia hata ofisini, ambapo wala usishangae baada ya kukamilisha mission akaanza kufukuzwa barabarani na raia baada ya mchezo kugundulika kabla hajapotea eneo la tukio!!

Itoshe tu kusema kwamba, Commando anaogopeka wakati wa vita ili hali Jasusi anaogopeka hata wakati wa kufungua champagne!!
Ufafanuzi mzuri Sana!
 
NAONA WATU WANAONGEA KISHABIKI.

... Hawa ni watu wawili tofauti, Commando ni para military na ni mara chache kidogo kuwa Jasusi complete ila Ujasusi hufundishwa pia.
... Jasusi hawezi kwenda katika ukomando, ametrainiwa na Intelligence husika ila Commando anaweza akapelekwa katika ujasusi.


UKISIKIA MTU COMMANDO MPE HESHIMA YAKE.
 
Back
Top Bottom