Ukimya ni silaha ya hatari anayotumia Samia aidha kwa kujua au kutokujua

hermanthegreat

JF-Expert Member
Mar 2, 2021
853
2,037
Silence is polite, silence gets people’s attention, further more, silence at the wrong time could be crushing weakness.

Tunaweza kufahamu ujinga wa mtu kwa kutazama anachokiongea. Tunaweza kufahamu huyu mtu anawaza Nini au alikuwa anawaza nini kwa kusikiliza anachokiongea.

Hivyo mtu akikaa kimya anakuwa ni hatari kwani tunashindwa kumuelewa. Tunaweza kudhani ana akili. Tunaweza kudhani ni mpole. Au tunaweza kudhani ana mawazo mazuri.

Mtu mkimya kwenye kundi la watu wanaozungumza anaweza kuwa mtu hatari zaidi na wa kuogopwa.

Ukimya wa Samia unavuta attention ya watu, pia unapunguza vitu vingi sana.

Sakata la bandari ni kubwa mno bila silaha yake hiyo lingekuwa na hali mbaya zaidi, aidha anakaa kimya kwa woga au aibu lakini hiyo Ina msaada kwake, itamfanya angalau awe na mvuto kwa wananchi japo kidogo.
 
Keshaongea mara nyingi tu, mara ya mwisho kuongea alienda kuongelea kanisani 😂😂

Anaongea sana tu ila kwa kutapatapa.
 
She is FAILURE aibu imemshika anajidanganya na ujasiri wakufundishwa.

Hili dili amelipika mwenyewe tokea mwanzo so anajua lengo lake ni wizi na si kingine
 
Silence is polite , Silence gets people’s attention, further more , silence at the wrong time could be crushing weakness.

Tunaweza kufahamu ujinga wa mtu kwa kutazama anachokiongea.
Tunaweza kufahamu huyu mtu anawaza Nini au alikuwa anawaza Nini kwa kusikiliza anachokiongea.

Hivyo mtu akikaa kimya anakuwa ni hatari kwani tunashindwa kumuelewa.

Tunaweza kudhani ana akili​

Tunaweza kudhani ni mpole.​

Au tunaweza kudhani ana mawazo mazuri​

Mtu mkimya kwenye kundi la watu wanaozungumza anaweza kuwa mtu hatari zaidi na WA kuogopwa.

Ukimya wa Samia unavuta attention ya watu , pia unapunguza vitu vingi sana .

sakata la bandari ni kubwa mno bila silaha yake hiyo lingekuwa na hali mbaya zaidi , aidha anakaa kimya kwa woga au aibu lakini hiyo Ina msaada kwake, itamfanya angalau awe na mvuto kwa wananchi japo kidogo.
mimi sijaongea tangu nibalehe!!! matokeo yske madem wananitongoza na sijuinifanyeje?
 
Silence is polite , Silence gets people’s attention, further more , silence at the wrong time could be crushing weakness.

Tunaweza kufahamu ujinga wa mtu kwa kutazama anachokiongea.
Tunaweza kufahamu huyu mtu anawaza Nini au alikuwa anawaza Nini kwa kusikiliza anachokiongea.

Hivyo mtu akikaa kimya anakuwa ni hatari kwani tunashindwa kumuelewa.

Tunaweza kudhani ana akili​

Tunaweza kudhani ni mpole.​

Au tunaweza kudhani ana mawazo mazuri​

Mtu mkimya kwenye kundi la watu wanaozungumza anaweza kuwa mtu hatari zaidi na WA kuogopwa.

Ukimya wa Samia unavuta attention ya watu , pia unapunguza vitu vingi sana .

sakata la bandari ni kubwa mno bila silaha yake hiyo lingekuwa na hali mbaya zaidi , aidha anakaa kimya kwa woga au aibu lakini hiyo Ina msaada kwake, itamfanya angalau awe na mvuto kwa wananchi japo kidogo.
Najalibu kuwaza ingekuwaje kama Magufuli angeamua kukaa kimya sakata la kina Kangi Lugola kwenda kusaini lile limkataba kule Singapore? alifanya vibaya kuliwahi kabla halijatoka na kumchafua?

Samia anakaa kimya cos imeonekana wazi kuwa yeye ndiye mwenye lile limkataba na kwa masikitiko zaidi hawezi kuja kutuambia kuwa hakuwa anajua chochote wakati kibali ametoa yeye!

Kukaa kimya kwa Samia juu ya mkataba huu mbovu hakuna faida kwa Taifa letu labda kuna faida kwake binafsi tu na sio kwa afya ya Taifa letu! na sio lazima aongee kwa maana Zuhura si yupo? si atoe tu statement mkataba wa mashirikiano umevunjika?
 
Kukaa kimya ni sawa, tatizo unakaa kimya kwa muda gani na kwasababu gani? Kaa kimya kimkakati, soma mazingira na kisha baada ya muda fulani vuja ukimya uje na majibu na suluhisho ili maisha yaendelee. Hata kama majibu na masuluhisho hayo hayatawafurahisha wengi, lakini angalau umevunja ukimya na umetoa majibu. Lakini kukaa kimya milele, bila majibu, bila suluhisho, ni dalili mbaya sana kwa kiongozi. Ni dalili ya kushindwa kupata suluhisho na itapelekea watu wengine kutengeneza majibu ya kufikirika au majibu wanayoyataka wao.

Sifa mojawapo ya kiongozi bora ni kutoa majibu na masuluhisho ya maswali na changamoto za wananchi na walio chini yake. Kiongozi kazi yake ni 'kuongoza', hivyo kutotoa majibu ni kupoteza sifa ya kuwa kiongozi (bora), ni sawa kuwa 'kiongozi asiyeongoza' - haipendezi kuwa kiongozi bila kuongoza kwa vitendo.

Kiongozi asiyeongoza (asiyetoa majibu na masuluhisho) atawafanya walio chini yake na wananchi kujiongoza wenyewe (Kutafuta majibu/masuluhisho ya changamoto zao) na wataanza kuhoji umuhimu wa uwepo kiongozi wao, wataanza kujiuliza maswali, kwamba kama tuna matatizo na tunahangaika wenyewe kuyatatua kiongozi wetu anafanya nini?
 
Back
Top Bottom