Siasa za MAGA, MATAGA na Mwamba Tuvushe ni hatari sana. Ni siasa za kinazi

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,233
12,740
Trump alikuwa na slogan yake ya Make America Great Again(MAGA). Baadaye wafuasi wake wakaanza kuitwa MAGA. Hawa jamaa huwaambii kitu kuhusu Trump. Kwao Trump ni kama Malaika au demigod. Kwao Trump hakosei(licha ya kukabiliwa na kesi kama 91). Hawa ndiyo mwezi wa kwanza mwaka 2021 walivamia bunge la Marekani kupinga matokeo ya uchaguzi, wakitaka kumnyonga makamu wa rais. Maga si wanachama wa republican tena, ni wanachama wa Trump. Ni waabudu watu. Wamekiteka republican kiasi kwamba mwanarepublican yeyote hawezi kutoboa iwapo anaenda kinyume na Trump. MAGA ni wa abudu mtu.

Hapa Tanzania wafuasi kindaki ndaki wa Magufuli walipachikwa jina MATAGA(Make Tanzania Great again). Waliitwa hivyo kuwafananisha na MAGAs. Hawa nao ulikuwa huwaambii kitu kuhusu Magufuli. Walimuabudu.

Sasa kuna hawa Mwamba Tuvushe. Hawa huwaambii kitu kuhusu Mbowe. Kwao Mbowe ni kama malaika asiyekosea. Kwao Mbowe hata akiwa mwenyekiti wa chama hadi kifo chake ni sawa tu. Kwao Mbowe hata afanye kosa gani( kama kumuingiza Lowassa na kumpa ugombea urais) ni sawa na wanaompinga ndiyo wabaya. Hawa nao wanamuabudu Mbowe. Kwao ni kama Messiah(Kristo)

Siasa hizi zilikuwepo kwa watu waliomuamini Hitler. Magumu ya Ujerumani baada ya WWI yaliwafanya wanachama wa nazi waamini Hitler ni kama Kristo(Messiah). Wakawa tayari kufanya kila alilowaambia. Wengi wa Wajerumani hawakuwa watu wabaya wa kuchoma binadamu wenzao kwenye matanuri. Lakini kwa kumfuata Kristo wao huyo waliweza kufanya ukatili wa ajabu kabisa.

Siasa za kuabudu watu ni hatari sana. Tuziepuke.
 
Jamii ikiwa na changamoto kubwa iliyokubuhu na utawala uliopo unaonekana kupuuzia ndipo sasa inamtarajia mkombozi asiyejulikana atatoka wapi ila akipatikana tu wanaishi naye maana ni vigumu kumpata. Haijalishi ana uelewa mdogo, elimu kidogo, upeo na busara ilimradi tu asemee matatizo yao makuu hapo anakuwa populist.

Na kunakuwepo sababu za msingi za kukubaliana nae hata kama ukizichunguza kwa kina ukagundua zina kasoro. Ndio maana wakombozi huchota maelfu ya watu na huwa na wafuasi lialia na machawa. Na humo hujitokeza watu smart wa kuendesha objectives zao mbaya.
Mfano aliyeleta hoja ya kuwachoma Wayahudi kwenye concentration camps ni Reinhard Heydrich, Joseoh Gobbels akawa Waziri wa Propaganda akaeneza cause yao kwa uwezo mkubwa ikakubalika na raia wengi na wale wachache waliokataa kazi ikawa kwa Gestapo na SS ya Heinrich Himmler kuwanyamazisha. Kufumba na kufumbua hamna uhuru tena hapo mpaka wafanye makosa ndio mrudi mstari myoofu.

Populism huwa inafeli kwa utekelezwaji au matokeo ya kutekeleza. Huwa haidumu sababu ni fake
 
Back
Top Bottom