Kati ya Ford Ranger Double Cabin na Land Cruiser Double Cabin, lipi ni gari bora zaidi kwa kazi za "porini"?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,857
6,600
Ingawa yote ni magari ya kazi, nahisi kuna linalomudu zaidi mazingira ya "kipori pori" kuzidi "jenzake".

Muda mrefu litakuwa likitumika Kanda ya Ziwa na mara chache Nyanda za Juu Kusini, hasa Rukwa na Katavi.

SIFA ZA GARI LINALOHITAJIKA:
1. Double Cabin Pick Up

2. Limudu safari ndefu za mara kwa mara

3. Limudu barabara za aina zote: lami, vumbi, na hata zenye utelezi nyakati za mvua

4. Liwe na uwezo wa kubeba mizigo midogo mara kwa mara na wakati mwingine muda mrefu - kutoka Mkoa mmoja hadi mwingine au mingine

5. Lililo na uwezekano wa kudumu
muda mrefu.


Lipi linakidhi hivyo vigezo kati ya FORD RANGER na LAND CRUISER?

Kuna lililo bora zaidi kuzidi hayo machaguo mawili?

 
Ngoja waje wazoefu watakushauri vizuri.

Ila ukipata pure Land cruiser double cabin from Japan hutokuja kujutia pesa yako.
πŸ™πŸ™πŸ™

Nimepachagua South Africa kwa sababu nataka nifike kuliona kabla ya kulilipia. Japan nahisi itakuwa gharama kubwa kuzidi South Africa. Hata wanafamilia wengi wa humu Jamii Forum wanaliafiki hilo, kwamba kuna unafuu endapo nitalichukulia South Africa.
 
land cruiser hana mpinzani
 
cruiser kwenye maintenance ni cheap kuliko ford, interms of spare parts na mafundi ila kwenye durability ford ranger Hana mpinzani
 
Siyo vizuri kuilinganisha hiyo Toyota Landcruiser pick up na Ford Ranger kwa shughuli za porini! Toyota Landcruiser ni mnyama wa porini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…