Dkt. Biteko: Dkt. Samia anakerwa na kukatika kwa Umeme, ni lazima tuzalishe umeme zaidi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema Serikali imeamua kwa dhati kuendeleza vyanzo vya umeme wa Jotoardhi ili kuhakikisha nchi inazalisha umeme wa kutosheleza mahitaji ya wananchi wake.

Amesema chanzo hicho cha umeme kitaongeza nguvu katika vyanzo vilivyopo vya Maji na Gesi Asilia.

Dkt. Biteko amesema hayo tarehe 20 Februari, 2024 mara baada ya kukagua vyanzo vya Jotoardhi vya Kiejo-Mbaka (60MW) na Ngozi (MW 70) mkoani Mbeya akifuatana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Juma Homera.

Dkt. Biteko amesema "Miradi hii ya Jotoardhi sasa lazima ianze, tutaanza na megawati 10 hapa Kiejo-Mbaka na Ngozi tutaanza na megawati 30 huku nyingine zikifuata, na hii inajumuisha miradi mingine kama wa Jua wa Kishapu (150 MW) ambao umeanza kutekelezwa, miradi ya umeme wa upepo ukiwemo wa Makambako na mradi wa Malagarasi ambao mkandarasi ameshasaini mkataba tayari kwa kuanza kazi."

Amewaelekeza watendaji wa Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC) kufanya kazi zinazoleta matokeo na si stori kwani Serikali inatafuta fedha za kutekeleza miradi hiyo na wajibu wa watendaji wa Taasisi hiyo ni kuhakikisha miradi hiyo inafanikiwa.

Dkt. Biteko ameongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka kuona watanzania wanapata huduma bora katika sekta zote, wanatolewa kwenye umaskini, anataka vitendo na siyo maneno, anataka kuona watu wahudumiwa na kufuatwa walipo, wanasikilizwa shida zao na kutatuliwa.

Ameongeza kuwa, Rais, Dkt. Samia anataka utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali iangalie miaka mingi mbele na si muda mfupi hivyo ametoa uhakika kwa wananchi kuwa miradi hiyo ya Jotoardhi itatekelezwa.

Kuhusu changamoto ya umeme, amesema kuwa, imetokana na vyanzo vya umeme nchini kwa muda mrefu kujikita kwenye makundi matatu tu ambayo ni maji (570MW), Mafuta na Gesi Asilia.

Amesema kwa sasa, vyanzo vya umeme vinatokana na Gesi Asilia na Maji ambavyo bado havitoshelezi mahitaji kutokana na kuzidi kukua kwa maendeleo, idadi ya watu kuzidi kuongezeka, miji kukua na umeme sasa kuwa ni hitaji muhimu na si anasa.

Amesema pamoja na kutegemea megawati 235 kutoka mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) na megawati 27 kutoka Rusumo, maboresho ya mitambo mingine ya umeme yanaendelea katika vituo mbalimbali.

Aidha, amesena kuwa, Serikali imeshaamua kutekeleza vyanzo vingine vya umeme ikiwemo vya Jotoardhi, Jua na Upepo kwani vipo na kinachohitajika ni kuvipa nguvu,

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amepongeza viongozi wa Mkoa wa Mbeya kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo pamoja na ushirikiano uliopo kati ya viongozi wa Serikali na Wabunge wa Mkoa huo.

Awali, Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Mathew Mwangomba, amesema kampuni hiyo ina miradi mitano ya kipaumbele nchini ambayo ni Kiejo-Mbaka, Ngozi, Songwe, Ruhoi na Natron.

Ameeleza kuwa, kwa Mkoa wa Mbeya miradi ya kipaumbele ni Ngozi na Kiejo-Mbaka ambapo mradi wa Ngozi unatarajiwa kuzalisha megawati 70 na Kiejo-Mbaka unatarajiwa kuzalisha megawati 60.

Katika mradi wa Ngozi, amesema kuwa, utatekelezwa kwa awamu huku awamu ya kwanza ikitarajiwa kuzalisha megawati 30 na fedha zimeshapatikana ili kuhakiki rasilimali ya Jotoardhi kwenye eneo hilo.

Ameongeza kuwa, mradi huo wa awali utakaozalisha megawati 30 utagharimu Dola za Marekani milioni 144 sawa na shilingi bilioni 369.

Kuhusu mradi wa Kiejo-Mbaka, amesema kuwa, unatarajiwa kuzalisha megawati 60 ambapo zitaanza kuzalishwa megawati kumi (10) ambazo utekelezaji wake utagharimu Dola za Marekani milioni 75.64 sawa na shilingi Bilioni 175.88.

Ameongeza kuwa, katika kuhakikisha nishati ya Jotoardhi inapatikana Tanzania, TGDC imechonga visima vifupi vya mita 300 ambavyo viliwezesha kupatikana kwa temperature takriban 75 na hii ikithibitisha kwamba kuendelea kuchimbwa kwa visima hivyo kuanzia mita 1500 hadi 1900 itapatikana temperature ya kutosha kuweza kuzalisha umeme.

Vilevile amesema kuwa, nishati ya Jotoardhi ina umuhimu mkubwa nchini kwani ni hakika, endelevu na salama hasa katika kipindi hiki ambacho dunia inapambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amemhakikishia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kuwa, Mbeya inamuunga mkono Rais, Dkt. Samia katika kulinda vyanzo vyote ya umeme vinavyogundulika pamoja na utunzaji wa mazingira ambayo yanapelekea vyanzo hivyo kuzalisha umeme kwa ufanisi.

Pia amempongeza Dkt. Biteko kwa ubunifu wake katika kuendeleza vyanzo vipya vya umeme ukiwemo wa Jotoardhi.
 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema Serikali imeamua kwa dhati kuendeleza vyanzo vya umeme wa Jotoardhi ili kuhakikisha nchi inazalisha umeme wa kutosheleza mahitaji ya wananchi wake...
Biteko, acha utoto, sema kama mwanaume mtu mzoma. Sema wananchi wanakelwa na si Samia. Acha utoto wa kijinga
 
FB_IMG_1708286062208.jpg
 
Tumechoka mambo ya kipuuzi tunataka umeme.

Jembe kwenye utawalawake sijui alipigaje umeme ukawa haukatiki kipumbavu kama ivi.
Watu wanacheza na maisha yetu kirahisi sana.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema Serikali imeamua kwa dhati kuendeleza vyanzo vya umeme wa Jotoardhi ili kuhakikisha nchi inazalisha umeme wa kutosheleza mahitaji ya wananchi wake.

Amesema chanzo hicho cha umeme kitaongeza nguvu katika vyanzo vilivyopo vya Maji na Gesi Asilia.

Dkt. Biteko amesema hayo tarehe 20 Februari, 2024 mara baada ya kukagua vyanzo vya Jotoardhi vya Kiejo-Mbaka (60MW) na Ngozi (MW 70) mkoani Mbeya akifuatana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Juma Homera.

Dkt. Biteko amesema "Miradi hii ya Jotoardhi sasa lazima ianze, tutaanza na megawati 10 hapa Kiejo-Mbaka na Ngozi tutaanza na megawati 30 huku nyingine zikifuata, na hii inajumuisha miradi mingine kama wa Jua wa Kishapu (150 MW) ambao umeanza kutekelezwa, miradi ya umeme wa upepo ukiwemo wa Makambako na mradi wa Malagarasi ambao mkandarasi ameshasaini mkataba tayari kwa kuanza kazi."

Amewaelekeza watendaji wa Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC) kufanya kazi zinazoleta matokeo na si stori kwani Serikali inatafuta fedha za kutekeleza miradi hiyo na wajibu wa watendaji wa Taasisi hiyo ni kuhakikisha miradi hiyo inafanikiwa.

Dkt. Biteko ameongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka kuona watanzania wanapata huduma bora katika sekta zote, wanatolewa kwenye umaskini, anataka vitendo na siyo maneno, anataka kuona watu wahudumiwa na kufuatwa walipo, wanasikilizwa shida zao na kutatuliwa.

Ameongeza kuwa, Rais, Dkt. Samia anataka utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali iangalie miaka mingi mbele na si muda mfupi hivyo ametoa uhakika kwa wananchi kuwa miradi hiyo ya Jotoardhi itatekelezwa.

Kuhusu changamoto ya umeme, amesema kuwa, imetokana na vyanzo vya umeme nchini kwa muda mrefu kujikita kwenye makundi matatu tu ambayo ni maji (570MW), Mafuta na Gesi Asilia.

Amesema kwa sasa, vyanzo vya umeme vinatokana na Gesi Asilia na Maji ambavyo bado havitoshelezi mahitaji kutokana na kuzidi kukua kwa maendeleo, idadi ya watu kuzidi kuongezeka, miji kukua na umeme sasa kuwa ni hitaji muhimu na si anasa.

Amesema pamoja na kutegemea megawati 235 kutoka mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) na megawati 27 kutoka Rusumo, maboresho ya mitambo mingine ya umeme yanaendelea katika vituo mbalimbali.

Aidha, amesena kuwa, Serikali imeshaamua kutekeleza vyanzo vingine vya umeme ikiwemo vya Jotoardhi, Jua na Upepo kwani vipo na kinachohitajika ni kuvipa nguvu,

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amepongeza viongozi wa Mkoa wa Mbeya kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo pamoja na ushirikiano uliopo kati ya viongozi wa Serikali na Wabunge wa Mkoa huo.

Awali, Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Mathew Mwangomba, amesema kampuni hiyo ina miradi mitano ya kipaumbele nchini ambayo ni Kiejo-Mbaka, Ngozi, Songwe, Ruhoi na Natron.

Ameeleza kuwa, kwa Mkoa wa Mbeya miradi ya kipaumbele ni Ngozi na Kiejo-Mbaka ambapo mradi wa Ngozi unatarajiwa kuzalisha megawati 70 na Kiejo-Mbaka unatarajiwa kuzalisha megawati 60.

Katika mradi wa Ngozi, amesema kuwa, utatekelezwa kwa awamu huku awamu ya kwanza ikitarajiwa kuzalisha megawati 30 na fedha zimeshapatikana ili kuhakiki rasilimali ya Jotoardhi kwenye eneo hilo.

Ameongeza kuwa, mradi huo wa awali utakaozalisha megawati 30 utagharimu Dola za Marekani milioni 144 sawa na shilingi bilioni 369.

Kuhusu mradi wa Kiejo-Mbaka, amesema kuwa, unatarajiwa kuzalisha megawati 60 ambapo zitaanza kuzalishwa megawati kumi (10) ambazo utekelezaji wake utagharimu Dola za Marekani milioni 75.64 sawa na shilingi Bilioni 175.88.

Ameongeza kuwa, katika kuhakikisha nishati ya Jotoardhi inapatikana Tanzania, TGDC imechonga visima vifupi vya mita 300 ambavyo viliwezesha kupatikana kwa temperature takriban 75 na hii ikithibitisha kwamba kuendelea kuchimbwa kwa visima hivyo kuanzia mita 1500 hadi 1900 itapatikana temperature ya kutosha kuweza kuzalisha umeme.

Vilevile amesema kuwa, nishati ya Jotoardhi ina umuhimu mkubwa nchini kwani ni hakika, endelevu na salama hasa katika kipindi hiki ambacho dunia inapambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amemhakikishia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kuwa, Mbeya inamuunga mkono Rais, Dkt. Samia katika kulinda vyanzo vyote ya umeme vinavyogundulika pamoja na utunzaji wa mazingira ambayo yanapelekea vyanzo hivyo kuzalisha umeme kwa ufanisi.

Pia amempongeza Dkt. Biteko kwa ubunifu wake katika kuendeleza vyanzo vipya vya umeme ukiwemo wa Jotoardhi.

Kama anakerwa na kukatika umeme aanze kwa kulala mbele na waziri mwenye dhamana
 
Hivi watanzania tuna shida sana.

Kwanini tunafanywa watoto sana?

Kwahiyo sasa

1. Tatizo sio upungufu wa maji tena?

2. Tatizo sio Maharage na J Makamba?

3. Tatizo sio watu wanazima makusudi ili wauze majenereta?

4. Tatizo sio miundo mbinu tena?

Ila sasa wamepata pa kutokea baada ya kauli ya Azim Dewji!!
 
Back
Top Bottom