Jeshi la Polisi laadhimisha Mapinduzi kwa kushiriki michezo mbalimbali

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
"FAMILIA ZETU ZINASHIRIKI KAZI ZETU KWA NAMNA MBALIMBALI"
IMG-20240112-WA0106.jpg

IMG-20240112-WA0105.jpg

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeadhimisha "Police Family Day" kwa kushiriki shughuli mbalimbali na michezo na familia zao.

Akifungua sherehe za maadhimisho ya "Police Family Day" Januari 12, 2024 katika uwanja wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mbeya, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Benno Malisa amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kutambua umuhimu wa kujumuika na familia na kufurahi pamoja.

Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi Benjamin Kuzaga amesema kuwa, Jeshi hilo linaenzi maadhimisho ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kushiriki kazi mbalimbali na kushiriki michezo mbalimbali.
IMG-20240112-WA0102.jpg

Aidha, Kamanda Kuzaga ameongeza kuwa mbali na michezo, wameandaa hafla ambayo itashirikisha wadau wa Jeshi la Polisi, vikundi vya ulinzi shirikishi na wananchi kwa lengo la kufanya tathmini ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi.

Sambamba na hayo, Kamanda Kuzaga amesisitiza na kuahidi kuendelea kushirikiana na wananchi katika kuzuia uhalifu kwani usalama uliopo ni kutokana na jitihada za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na wananchi wa Mkoa wa Mbeya.
 
Back
Top Bottom