Katavi: DC Jamila asitisha zoezi la uwekezaji mpaka taratibu ziwekwe wazi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462

Wananchi wa Kijiji cha Mtisi, Kata ya Sitalike Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi wamemgomea mwekezaji anayetaka kuwekeza katika maeneo ambayo yapo karibu na mto ambapo maeneo hayo ndio tegemeo la kuhifadhi chanzo cha maji ya mto huo.

Bosco Chamtepa, Mwajuma Bashiri na Abel Mazuke wamesema maeneo hayo ambayo muwekezaji anataka kuwekeza si sahihi kwani yapo karibu na mto huku wakidai taratibu za uwekezaji hazikuwekwa wazi kwa wananchi wa kijiji hicho.

George Alphonce na Nestori Damas ni wenyeviti wa vitongoji katika kijiji cha Mtisi wamesema taarifa za uwekezaji wa eneo hili hawajapendezwa nao licha ya vikao na mikutano ya kijiji kuketi ili kujua taratibu zilizotumika kumruhusu muwekezaji huyo.

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf ameagiza zoezi hilo la muwekezaji kuwekeza katika maeneo hayo ambayo yapo karibu na mto yasitishwe mpaka hapo watakapojiridhirisha kama taratibu za uwekezaji zilifuatwa katika eneo hilo.

Muwekezaji huyo kutoka nchi ya China anatarajia kuwekeza katika eneo hilo ambalo liko karibu na mto kwa kufanya shughili za uchimbaji wa madini yaliyopo katika eneo hilo.
 
Back
Top Bottom